Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Martin George

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
1,695
1,470
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema aliyekuwa mwanachama wao ndugu Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote ndani ya chama chao tokea alipojiunga akitokea CCM.

Chanzo: Gazeti la Nipashe!

My take:
"Sizitaki mbichi hizi", Sungura akagumia
===============

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema kuwa aliyekuwa mwanachama wao, Lawrence Masha hakuwa na msaada wowote ndani ya chama hicho.

Amesema kuwa kuondoka kwa Masha katika Chama hicho hakijatikisika chochote bali kinazidi kuimariki na kupokea wanachama wengi wapya, hivyo kuondoka kwa mtu asiyekuwa na msaada ndani ya chama hicho si tatizo.

“Alikuwa hatusaidii chochote ndani ya maji, kwani ulishawahi kumsikia amefanya chochote akiwa chadema? acha amfuate babu yake, acha aondoke zake, sisi hatujapoteza chochote, hata alipokuwa waziri alifanya nini, acha aende kwenye biashara zake Uingereza maana tunasikia anawekeza kule,”amesema Mbowe

Aidha, Masha alitangaza uamuzi wa kuondoka Chadema kupitia taarifa yake iliyosambazwa kupitia vyombo vya habari na mitandao ya kijamii ya kuamua kuachana na Chadema huku akisema chama hicho kinasafari ndefu ya kuweza kutwaa dola.
 
Yaani mpaka atoke mtu ndo mumlipue?

Yale yale ya akina Kigwangallah kutaka TAKUKURU wamkamate Nyalandu kwa kugawa vitalu hovyo wakati wanajua viligawiwa Ikulu - sawa tu na sasa tender za bombadier as well as ujenzi wa uwanja wa Chato zilivyosimamiwa na mkuu mwenyewe. Utashangaa miaka 8 ijayo mtu kama Prof. Mbarawa anatakiwa kuchunguzwa na kuhojiwa na vyombo. Unafiki huu ndo asili ya Watanzania
 
Si ajabu hata Dkt. Slaa wanamwona hakuwa na msaada wowote kwa CHADEMA.

Ila nakumbuka jinsi huyo Masha alivyosifiwa humu wakati wa ule uchaguzi wa TLS [ambao wachache wetu tulisema hauna umuhimu wala athari zozote zile za maana nchini].

Watu walimsifia kuwa eti yeye na Lissu walicheza gemu kama Pele halafu baadaye huyo Masha akajitoa katika kugombea huo urais usio na athari yoyote ya maana nchini.

Leo kajitoa huko CHADEMA....wameanza kumponda!

Oh well, it's par for the course, anyway!
 
Kwani TLS ni Chadema?au nimekuelewa vibaya?

Oh yeah...TLS hii ya hawa 'team Mange kasema' ni tawi la CHADEMA.

Hukuwaona walivyofurahi Lissu alipochaguliwa?

Yaani ungedhani ni ujio mpya wa Yesu jinsi walivyofurahia....wakati mwisho wa siku hakuna lolote la maana hiyo TLS inachoweza kufanya kuhusu jambo lolote lile la maana hapa nchini.
 
Nakumbuka jinsi huyo Masha alivyosifiwa humu wakati wa ule uchaguzi wa TLS [ambao wachache wetu tulisema hauna umuhimu wala athari zozote zile za maana nchini].

Watu walimsifia kuwa eti yeye na Lissu walicheza gemu kama Pele halafu baadaye huyo Masha akajitoa katika kugombea huo urais usio na athari yoyote ya maana nchini.

Leo kajitoa huko CHADEMA....wameanza kumponda!

Oh well, it's par for the course, anyway!

Halafu watakuja kutuambia kuwa kina Lowassa hawakuwa na msaada wowote, something has happened to CHADEMA and it ain't sweet!
 
Back
Top Bottom