Mbowe, Lowassa kuwanadi wagombea wa CHADEMA nchi nzima


Dreka

Dreka

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Messages
5,749
Likes
6,856
Points
280
Dreka

Dreka

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2017
5,749 6,856 280
Wewe ndo kila anachotaka ufanye unafanya but c mimi hapa and sitakuja kuwa mtumwa wa namna hiyo
Una impact gan mkuu kwa serikali iliyopo madarakani ?

naamini kwa matumizi yetu ya majina fake hapa jf ni ushahidi tosha kuwa huna uthubutu wa kupinga agizo lolote la serikali hadharani.
 
MZEE MSASAMBEGU

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Messages
2,749
Likes
2,386
Points
280
MZEE MSASAMBEGU

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2013
2,749 2,386 280
Una impact gan mkuu kwa serikali iliyopo madarakani ?

naamini kwa matumizi yetu ya majina fake hapa jf ni ushahidi tosha kuwa huna uthubutu wa kupinga agizo lolote la serikali hadharani.
Ogopa sana kitu kinachoitwa passive resistance..wakati wa ukoloni wakoloni walikuwa wanawachukua watumwa na kuwatumikisha kwenye mashamba yao mfano kulima,kupanda,kupalilia and kuvuna... Mfano wa mbinu moja ambayo ni passive resistance watumwa walikuwa wanazichemsha mbegu kabda ya kuzipanda and wakoloni hio hawakulijua ila mwisho wa siku ilifahamika tu...ogopa sana kitu kinachoitwa passive resistance...ni hatari sana kuliko active resistance ambayo inaonekana we ndo unaiamini sana..hadi hapo nafkiri ushanielewa
 
Dreka

Dreka

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Messages
5,749
Likes
6,856
Points
280
Dreka

Dreka

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2017
5,749 6,856 280
Ogopa sana kitu kinachoitwa passive resistance..wakati wa ukoloni wakoloni walikuwa wanawachukua watumwa na kuwatumikisha kwenye mashamba yao mfano kulima,kupanda,kupalilia and kuvuna... Mfano wa mbinu moja ambayo ni passive resistance watumwa walikuwa wanazichemsha mbegu kabda ya kuzipanda and wakoloni hio hawakulijua ila mwisho wa siku ilifahamika tu...ogopa sana kitu kinachoitwa passive resistance...ni hatari sana kuliko active resistance ambayo inaonekana we ndo unaiamini sana..hadi hapo nafkiri ushanielewa
Sawa
lakini naomba tuwe realistic, hivi tangu viongozi wameanza kujifanyia mambo wanavyotaka chini ya serikali za ccm, kuna jambo lipi unadhani ni threat kwa serikali hii ya magufuli ambalo litatokana na passive resistance ?


Mimi binafsi ni Pro Active resistance.
 
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2012
Messages
4,568
Likes
2,220
Points
280
Ufipa-Kinondoni

Ufipa-Kinondoni

JF-Expert Member
Joined Jan 3, 2012
4,568 2,220 280
pic+chadema.jpg


Viongozi wa juu wa Chadema , Freeman Mbowe na Edward Lowassa wataongoza kampeni za uchaguzi mdogo wa nafasi za udiwani kwenye kata 43.

Chama hicho kimeunda Kamati za Kitaifa 10, zitakazoongeza nguvu, hamasa na mikakati ya kampeni za uchaguzi wa marudio kwenye nafasi hizo kuanzia kesho hadi siku ya uchaguzi.

Timu hizo ambazo zitafanya kazi kwa kushirikiana na kamati zingine za hamasa katika ngazi za kanda, mikoa, majimbo, kata na matawi katika maeneo yenye uchaguzi huo, zitaongozwa na Mwenyekiti wa Chama Taifa, Freeman Mbowe.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho Tumaini Makene imeeleza kuwa Mbowe ataanza kuzindua kampeni kesho katika Kata ya Saranga, jijini Dar es Salaam.

Makene ametaja watakaoongoza timu hizo zilizopangwa kwa makundi A hadi G, kuwa ni Mwenyekiti wa Chama Taifa Freeman Mbowe, Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa, Makamu Mwenyekiti Taifa (Bara), Profesa Abdallah Safari, Makamu Mwenyekiti wa Chama Taifa (Zanzibar) Said Issa Mohamed, Katibu Mkuu wa Chama Dk. Vincent Mashinji.

Amewataja wengine watakaoongoza timu hizo kuwa ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Bara), John Mnyika, Naibu Katibu Mkuu wa Chama (Zanzibar), Salum Mwalimu.

Amesema timu hizo zitasaidiwa kwa ukaribu na timu zingine tatu chini ya uratibu na mikakati ya mabaraza ya chama, ikiwamo Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha), Baraza la Vijana wa Chadema (Bavicha) na Baraza la Wazee wa Chadema.

Timu hizo zitazunguka katika maeneo yote ya uchaguzi wa kata hizo 43, lengo ni kuwafikia wananchi wote kuelekea uchaguzi huo.

“Chadema tutaweza kuwafikia na kuzungumza na wananchi katika majimbo 37, halmashauri 36, mikoa 19 nchi nzima.

“Chama kimedhamiria kuweka ushindani mkubwa na kushinda kata hizo 43 ambazo chama kimeweka wagombea, tunaamini ushindi upo na ndiyo maana tunakutana na wananchi kuwahamasisha na kuwasikiliza wanataka nini ” amesema Makene.
 
MZEE MSASAMBEGU

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2013
Messages
2,749
Likes
2,386
Points
280
MZEE MSASAMBEGU

MZEE MSASAMBEGU

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2013
2,749 2,386 280
Sawa
lakini naomba tuwe realistic, hivi tangu viongozi wameanza kujifanyia mambo wanavyotaka chini ya serikali za ccm, kuna jambo lipi unadhani ni threat kwa serikali hii ya magufuli ambalo litatokana na passive resistance ?


Mimi binafsi ni Pro Active resistance.
Mkuu mimi najizungumzia mimi kama mimi...now nipo nafanya passive resistance ambayo ni hatari sana...matokeo yake nafikir yataoneka mbeleni...tunatumia I'd fake so ni ngumu kujuana huyu ni nani and ana effect gani
 
Dreka

Dreka

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2017
Messages
5,749
Likes
6,856
Points
280
Dreka

Dreka

JF-Expert Member
Joined Oct 27, 2017
5,749 6,856 280
Mkuu mimi najizungumzia mimi kama mimi...now nipo nafanya passive resistance ambayo ni hatari sana...matokeo yake nafikir yataoneka mbeleni...tunatumia I'd fake so ni ngumu kujuana huyu ni nani and ana effect gani
Hapo nimekusoma sasa

Tuko pamoja
 
Jumong S

Jumong S

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2013
Messages
3,598
Likes
2,667
Points
280
Jumong S

Jumong S

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2013
3,598 2,667 280
Kila la kheri!!! Ila CDM isisahau kujenga na Ofisi ya hadhi ya kitaifa....

Zama zimebadilika...wasiwe kama muonekano wa Dr Louis Shika!!
 
kirikou1

kirikou1

JF-Expert Member
Joined
Nov 8, 2016
Messages
3,389
Likes
4,096
Points
280
Age
26
kirikou1

kirikou1

JF-Expert Member
Joined Nov 8, 2016
3,389 4,096 280
Mzee wa kolomije akiona amezidiwa lazima aagize marufuku mikusanyiko
 
Paul Alex

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2012
Messages
3,030
Likes
4,726
Points
280
Paul Alex

Paul Alex

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2012
3,030 4,726 280
Dar es Salaam. Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu kesho ataungana na viongozi wa Chadema kwenye kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani utakaofanyika katika kata 43 nchi.

Akizungumza leo Novemba 11, kwenye ufunguzi wa kampeni hizo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe amesema amempokea Nyalandu na ataungana naye kwenye mkutano mwingine kama huo utakaofanyika Mtwara mjini hapo kesho.

‘’Kila anayeondoka chama tawala anaitwa fisadi, potelea mbali wamempokea na wengine wengi watahamia kuleta mabadiliko’’ amesema na kuongeza

"Mabadiliko hayaji ghafla yanakuja taratibu na ujio wao ndiyo mwanzo wa mabadiliko tulipoanza na tulipo sasa kuna tofauti kubwa" amesema Mbowe.

Amefafanua kwamba haungi mkono nchi kuwa na wezi, lakini anashauri sheria iachwe iamue haki badala ya kuingiliwa kama inavyofanyika kwa mahakama.Huku akidai kwamba watawala wana hofu ndiyo maana hawataki ushauri.

Amesema wataendelea kupigania haki ya kupigania haki ya kufanya mikutano ya kisiasa na ipo siku wataingia mtaani kuidai bila kuogopa vifaru.

Amesema huu siyo wakati wa kuogopa na kukaa kimya ni wakati wa kusimama na kutetea haki ya kufanya siasa.

Kuhusu uchumi kusinyaa amesema ni kweli umesinyaa na inaonekana wazi jinsi maisha yalivyo wananchi, wafanyabiashara, watawala wote wanalia njaa hakuna mwenye nafuu.

Meya wa Manispaa ya Ubungo, Boniface Jacob amesema anahitaji kuongeza nguvu ya kuleta maendeleo katika manispaa hiyo, hivyo mgombea udiwani kata ya Saranga Ephram Kinyafu anatosha.

Naye Mjumbe wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Kanda ya Pwani Frederick Sumaye amehoji kuhusu hali za wananchi kuendelea kuwa mbaya.
"Tumeamua na tunamaanisha wakati huu ushindi ni lazima, na mtakaotupa ushindi ni nyie wananchi" amesema Sumaye.
 
Endeleaaa

Endeleaaa

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
1,318
Likes
405
Points
180
Endeleaaa

Endeleaaa

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
1,318 405 180
Hapo ndio utaona tofauti ya ccm na chadema. Mwenyekiti Taifa kwenda kwenye kampeni ndogo ya udiwani kupambana na mwenyekiti wa wilaya wa ccm.
 
Asprin

Asprin

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2008
Messages
55,801
Likes
34,934
Points
280
Asprin

Asprin

JF-Expert Member
Joined Mar 8, 2008
55,801 34,934 280
Hapo ndio utaona tofauti ya ccm na chadema. Mwenyekiti Taifa kwenda kwenye kampeni ndogo ya udiwani kupambana na mwenyekiti wa wilaya wa ccm.
Nadhani unajisahaulisha tu kuwa mwenyekiti wako aligeuza shughuli za kijeshi kuwa za kichama kwa kuwapokea madiwani hewa waliowanunua toka CDM kule Arusha...

Wakati mwenyekiti wa huku anapambana madiwani wake wachaguliwe... mwenyekiti mwingine anapokea madiwani walionunuliwa

Ushasahau kauli takatifu ya mwenyekiti.... "Wako wapi wale watu wako??... Wapumbavu kabisa"
 
Kajolijo

Kajolijo

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Messages
2,328
Likes
2,558
Points
280
Age
31
Kajolijo

Kajolijo

JF-Expert Member
Joined May 30, 2016
2,328 2,558 280
Halafu mkishindwa uchaguzi mseme mmeibiwa.
 
O

Opyempye Nchee

JF-Expert Member
Joined
Oct 19, 2017
Messages
209
Likes
97
Points
45
O

Opyempye Nchee

JF-Expert Member
Joined Oct 19, 2017
209 97 45
Mjiandae kumpokea na Mh. Magufuri
 
B

Benny Haraba

JF-Expert Member
Joined
Dec 7, 2012
Messages
3,706
Likes
1,909
Points
280
Age
56
B

Benny Haraba

JF-Expert Member
Joined Dec 7, 2012
3,706 1,909 280
Mbowe kama mbunge ile sheria ya kutofanya shughuli za kisiasa nje ya jimbo lako haimuhusu ?
Mkulu mbona anafanya siasa tena home sweet home Mara kwa mara
 

Forum statistics

Threads 1,213,802
Members 462,292
Posts 28,490,656