Mbowe leo

mibiki mitali

JF-Expert Member
Feb 5, 2018
238
392
Anaitwa Wakili msomi Dickson Matata, ukipenda muite XABI ALONSO, yaani 'midifida kisheti'. Jopo la mawakili wamempa jina la 'kiungo mkata umeme', Ni kiunganishi benchi la mbele la akina Kibatala na mstari wa nyuma ya upekuzi wa nyaraka na sheria mbalimbali wakati wote wa kesi.


Wakili Dickson Matata, very sharp kwenye kuleta nyaraka kwenye dawati la mbele. Pia, leo amefanya kazi kubwa sana kuhakikisha makarao wanapisha 'benchi' nzima walilokuwa wamejiweka wengi, familia na wapiganaji wenzetu waliokuwa nje wameingia ndani..


saa 6 mchana mawakili wa serikali wanaingia kwenye ukumbi wa mahakama.

Watuhumiwa wanaingia na kuketi kwenye benchi kabla ya kupanda kizimbani..

Jaji anaingia

kesi inatajwa kesi namba 16 ya 2021

watuhumiwa wanapanda kizimbani..



kama binadamu tungenyimwa midomo basi Kuna watu wasingeteseka kabisa, maana wanatumia pen na karatasi kuwasiliana kuliko midomo yao, si Mwingine ni Wakili Msomi Jonathan Mndeme, msanifu wa upande wa utetezi muda wa wote, yupo serious muda wote ku' note kila Jambo..



Wakili wa serikali Robert Kidani anatawatambulisha mawakili wenzake..

1. Robert Kidando
2. Nassoro Katuga
3. Ignas Mwanuka
4. Esther Martin
5. Tulumanywa Majigo
6.
7.
8.


Wakili Peter Kibatala anawatambulisha mawakili wenzake wa utetezi.. Orodha yao nilikutajia awali.. Nairejea..


Mawakili wote hawa wanasimama kwa niaba ya mshtakiwa wa nne, Freeman Mbowe..

mshtakiwa wa pili atawakilishwa na wakili John Mallya..

Mshtakiwa wa tatu atawakilishwa na wakili Dickson Matata..
 
Back
Top Bottom