Mbowe kuwania ubunge | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe kuwania ubunge

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Feb 18, 2009.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,419
  Likes Received: 81,465
  Trophy Points: 280
  Mbowe kuwania ubunge

  Mwandishi Wetu Februari 18, 2009
  Raia Mwema~Muungwana ni Vitendo​

  Hoja ya ufisadi kuimaliza CCM kwenye majimbo Mara, Manyara, Kigoma, Kilimanjaro

  MIVUTANO ya makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajia kufanikisha jitihada za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhitimisha vyema mpango wake wa kuongeza idadi ya wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  CHADEMA imejipanga kujiimarisha zaidi katika ngazi ya ubunge kutokana na kile kinachobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, chama chenye wabunge wengi ndicho kinachounda Serikali.

  Na kutokana na masharti hayo ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kutoka chama kingine na kile kitakachounda Serikali, yaani chenye wabunge wengi.

  Mwenendo wa kisiasa nchini unabainisha kuwa nguvu za chama hicho zimeongezeka na msingi wa ongezeko hilo ni utendaji wa wabunge wa chama hicho ndani ya Bunge, na tayari katika baadhi ya majimbo ambako chama hicho hakina wabunge dalili zinaonyesha mafaniko.

  Kutokana na hali hiyo, taarifa zaidi zinabainisha kuwa huenda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akaingia katika kinyang’anyiro cha ubunge na hivyo kutorejea katika kinyang’anyiro cha urais, kama ilivyokuwa mwaka 2005.

  Taarifa hizo zinaendelea kubainisha kuwa uamuzi wa chama hicho kuwa na mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani utaegemea zaidi Katiba ya chama hicho.

  Katiba ya chama hicho inatoa fursa kwa mwanachama yeyote wa chama hicho kugombea nafasi ya urais. Hata hivyo, mbali na uwezekano wa chama hicho kuteua mgombea mwingine wa urais badala ya Mbowe, fursa nyingine iliyokuwapo ni kuunga mkono mgombea urais wa chama kingine cha upinzani.

  Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe aligombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, baada ya kuamua kutotetea nafasi yake ya ubunge. Mbowe alikuwa mbunge wa Hai na alikuwa kati ya wabunge machachari katika Bunge lililokuwa chini ya Spika, Pius Msekwa.

  Taarifa zilizotufikia zinabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa makundi yanayovutana CCM na hususan ngazi ya majimbo ya uchaguzi wa wabunge kuinufaisha CHADEMA.

  Uchunguzi wetu unabainisha kuwa takriban katika kila mikoa na hata katika majimbo mengi ya uchaguzi Tanzania Bara, CCM imegawanyika katika makundi kama ilivyokuwa katika Jimbo la Uchaguzi la Tarime.

  Katika Jimbo la Tarime, CCM iligawanyika katika kambi mbili zilizokuwa zikiongozwa na Christopher Gachuma na Kisiery Chambiri.

  Kutokana na mgawanyiko huo na kutokana na ukweli kwamba CCM ilihitaji mgombea mmoja kutoka kundi mojawapo, kambi ambayo ilishindwa kutoa mgombea ilitoa ushirikiano kwa mgombea wa CHADEMA.

  Hali hiyo ya mgawanyiko Tarime ndiyo iliyopo katika baadhi ya majimbo, ambayo ni pamoja na Vunjo, ambalo kwa sasa mbunge wake ni Aloyce`Kimaro.

  Uchunguzi wetu umebaini kuwa msimamo wa Kimaro katika vita dhidi ya ufisadi ndiyo chanzo cha kuibuka kwa kundi linalompinga. Kimaro amekuwa mstari wa mbele kushinikiza hatua zichukuliwe dhidi ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa au yeye mwenyewe (Mkapa) atoe maelezo kwa umma kuhusu tuhuma zinazomkabili.

  Kutokana na msimamo huo, inaelezwa kuwa wameibuka baadhi ya wana-CCM wanaomkingia kifua Mkapa, ambao pia wamejipanga kwa kushirikiana na mitandao mingine ndani ya CCM kumng’oa mbunge huyo.

  Mbali na Vunjo, majimbo mengine ambayo CCM haiko salama ni pamoja na baadhi yaliyomo mkoani Mbeya, ikielezwa kuwa baadhi ya kambi ndani ya CCM zimeandaa wagombea watakaochuana na wabunge wa CCM kwa tiketi ya chama hicho katika kura za maoni.

  Majimbo mengine ambayo wabunge wa sasa wa CCM wameandaliwa wapinzani kutoka katika makundi pinzani ndani ya chama hicho ni pamoja na Nzega mkoani Tabora, ambalo Mbunge wake ni Lucas Selelii, Lupa mkoani Mbeya, ambalo mbunge wake ni Victor Mwambalaswa, ambako taarifa zinabainisha kuwa huenda mbunge wa zamani wa Jimbo hilo, Njelu Kasaka, akajitokeza kumpinga.

  Lakini mbali na makundi hayo, baadhi ya majimbo ambayo CHADEMA inatarajiwa kutoa ushindani ni pamoja na Mbeya Vijijini, ambako mbunge wake wa sasa Luckson Mwanjale alipata ushindi wa asilimia 35 ya waliopaswa kupiga kura.

  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Freeman Mbowe huenda akaenda kugombea ubunge katika jimbo lake la zamani la Hai ambalo kwa sasa mbunge wake ni Fuya Kimbita.

  Mkurugenzi wa masuala ya Bunge Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema, kuhusu uwezekano wa Mbowe kuwania ubunge pamoja na mikakati ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.  Mkurugenzi wa masuala ya Bunge Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema
  ‘‘Ni mapema mno kusema kuwa Mwenyekiti wetu (Mbowe) atakwenda kugombea ubunge na kutogombea urais. CHADEMA ni chama kinachofuata demokrasia wagombea huchukua fomu na kupitishwa na mkutano mkuu. Hatua hizo zote bado hazijafikiwa,’’ alisema Mrema, ambaye naye taarifa zinabainisha kuwa huenda akagombea ubunge katika jimbo mojawapo mkoani Kilimanjaro.

  Lakini mbali na kutokuwa muwazi katika suala hilo, Mrema alisema Operesheni Sangara imekifanya chama hicho kutambua nafasi na nguvu zake ndani ya jamii ya Watanzania.

  ‘‘Ipo mikoa ambayo tuna uhakika wa kuongeza idadi ya wabunge. Kwa mfano, mkoani Mara tunataraji kutwaa majimbo saba. Na mikoa mingine tunayotarajia kupata wabunge ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza.’’

  Alisema mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na baadhi ya mikoa mingine idadi ya wabunge wa chama hicho wanataraji itaongezeka kutokana na mwitikio wa wananchi kuhusu utendaji wa chama hicho.

  Taarifa nyingine zilizotufikia zinabainisha kuwa hivi karibuni taasisi moja ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifanya utafiti katika majimbo 10 nchini ili kubaini kama wabunge wa sasa wanaweza kung’olewa au la.

  Baadhi ya majimbo yaliyohusishwa na utafiti wa taasisi hiyo ni pamoja na Karatu, ambalo Mbunge wake ni Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA), Kigoma Kaskazini-Kabwe Zitto (CHADEMA), Urambo Mashariki-Samuel Sitta (CCM), Mbozi Mashariki-Godfrey Zambi (CCM), Simanjiro-Christopher ole Sendeka (CCM), Mpanda Kati-Saidi Arfi (CHADEMA) na Moshi Mjini-Philemon Ndesamburo.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, baadhi ya majimbo imebainika kuwa ni vigumu kuwang’oa wabunge wa sasa kwa kura kupitia uchaguzi huru na wa haki.

  Utafiti katika majimbo hayo unaelezwa kulenga kusaidia kundi fulani katika siasa kutokana na kuonekana dhahiri kuyahusu majimbo yenye wabunge wanaokera baadhi ya wanasiasa, hususan wale wanaoguswa na tuhuma mbalimbali za ufisadi zilizoanikwa hadharani katika miaka ya karibuni.
   
 2. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #2
  Feb 18, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 0
  It makes alot of sense kama finally mkuu amekubali hili, sasa huko kwenye urais wamuachie rais wangu Dr. Slaa.
   
 3. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #3
  Feb 18, 2009
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  chama chenye wabunge wengi ndicho kinaunda serikali?sasa kiongozi wa serikali anakuwa rais yuleyule hata kama anatoka chama chenye wabunge wachache au itakuwaje?hiki kipengele cha katiba nilikuwa sikijui wakuu anaejua anijuze.
  nampongeza mbowe akichukua uamuzi wa kugombea ubunge.kama ninavyosema siku zote urais wamuachie kikwete maana ni dhahiri atashinda tu 2010.
  lipumba,mrema,baregu,mbatia,makaidi...mnangoja nini na nyinyi?
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mtyarajiwa,
  Mkuu hata mimi nilikuwa sijui hilo kumbe katiba yetu ni sawa na ile ya Marekani inaposikia swala hili.. Safi sana....
  nakumbuka mwaka 2005 ktk uchaguzi niliwahi kuuliza swali hili nikaambiwa kuwa rais wa Tanzania huchaguliwa kutokana na Popular vote (kura za urais) badala ya Electro vote (kura za wabunge).. nikashangaa sana... maanake kama Chadema wangechukua majimbo mengi ya Ubunge bado Kikwete angekuwa rais kwa kuchukua kura 80%..

  Sasa ukitazama Marekani Gore alishinda kwa Popular vote against Bush lakini kutokana na kura za wabunge wao, Bush alichukua madaraka pamoja na kwamba mara nyingi huwezi kupata ushindi wa Wabunge wengi ikiwa mgombea wako wa Urais ni mchovu..
  Kutokana na mfumo huu wa katiba basi ipo kila sababu ya Mbowe kujipanga wilayani kisha asimamishwe kama mgombea mwenye mvuto wa urais..Tatizo langu kubwa kwa Dr. Slaa kusimama Urais ni uwezekano wa kupoteza jimbo lake.. hivyo ukimwondoa Mbowe ukamweka Dr. Slaa ni sawa na kutoa fedha mfuko wa nyuma ukaziweka mfuko wa mbele ktk suruali moja..
  Chadema inahitaji majimbo yote hasa haya ambayo hadi leo wanayashika...kumwondoa mgombea mmoja kamka Dr. Slaa ni lazima wawe na hakika na mgombea watakaye mweka kutopoteza jimbo hilo..
   
  Last edited: Feb 18, 2009
 5. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #5
  Feb 18, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hata huko hapati, kwani nae ni fisadi kidogo?
   
 6. Zero

  Zero JF-Expert Member

  #6
  Feb 18, 2009
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 301
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Rais anachaguliwa kwa popular vote.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Hoja ya ufisadi kuimaliza CCM kwenye majimbo Mara, Manyara, Kigoma, Kilimanjaro

  MIVUTANO ya makundi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajia kufanikisha jitihada za Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhitimisha vyema mpango wake wa kuongeza idadi ya wabunge katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

  CHADEMA imejipanga kujiimarisha zaidi katika ngazi ya ubunge kutokana na kile kinachobainishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa, chama chenye wabunge wengi ndicho kinachounda Serikali.

  Na kutokana na masharti hayo ya Katiba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kutoka chama kingine na kile kitakachounda Serikali, yaani chenye wabunge wengi.

  Mwenendo wa kisiasa nchini unabainisha kuwa nguvu za chama hicho zimeongezeka na msingi wa ongezeko hilo ni utendaji wa wabunge wa chama hicho ndani ya Bunge, na tayari katika baadhi ya majimbo ambako chama hicho hakina wabunge dalili zinaonyesha mafaniko.

  Kutokana na hali hiyo, taarifa zaidi zinabainisha kuwa huenda Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe, akaingia katika kinyang’anyiro cha ubunge na hivyo kutorejea katika kinyang’anyiro cha urais, kama ilivyokuwa mwaka 2005.

  Taarifa hizo zinaendelea kubainisha kuwa uamuzi wa chama hicho kuwa na mgombea wake wa urais katika Uchaguzi Mkuu mwakani utaegemea zaidi Katiba ya chama hicho.

  Katiba ya chama hicho inatoa fursa kwa mwanachama yeyote wa chama hicho kugombea nafasi ya urais. Hata hivyo, mbali na uwezekano wa chama hicho kuteua mgombea mwingine wa urais badala ya Mbowe, fursa nyingine iliyokuwapo ni kuunga mkono mgombea urais wa chama kingine cha upinzani.

  Katika Uchaguzi Mkuu wa 2005, Mbowe aligombea urais kwa tiketi ya CHADEMA, baada ya kuamua kutotetea nafasi yake ya ubunge. Mbowe alikuwa mbunge wa Hai na alikuwa kati ya wabunge machachari katika Bunge lililokuwa chini ya Spika, Pius Msekwa.

  Taarifa zilizotufikia zinabainisha kuwa kuna uwezekano mkubwa kwa makundi yanayovutana CCM na hususan ngazi ya majimbo ya uchaguzi wa wabunge kuinufaisha CHADEMA.

  Uchunguzi wetu unabainisha kuwa takriban katika kila mikoa na hata katika majimbo mengi ya uchaguzi Tanzania Bara, CCM imegawanyika katika makundi kama ilivyokuwa katika Jimbo la Uchaguzi la Tarime.

  Katika Jimbo la Tarime, CCM iligawanyika katika kambi mbili zilizokuwa zikiongozwa na Christopher Gachuma na Kisiery Chambiri.

  Kutokana na mgawanyiko huo na kutokana na ukweli kwamba CCM ilihitaji mgombea mmoja kutoka kundi mojawapo, kambi ambayo ilishindwa kutoa mgombea ilitoa ushirikiano kwa mgombea wa CHADEMA.

  Hali hiyo ya mgawanyiko Tarime ndiyo iliyopo katika baadhi ya majimbo, ambayo ni pamoja na Vunjo, ambalo kwa sasa mbunge wake ni Aloyce`Kimaro.

  Uchunguzi wetu umebaini kuwa msimamo wa Kimaro katika vita dhidi ya ufisadi ndiyo chanzo cha kuibuka kwa kundi linalompinga. Kimaro amekuwa mstari wa mbele kushinikiza hatua zichukuliwe dhidi ya Rais mstaafu, Benjamin Mkapa au yeye mwenyewe (Mkapa) atoe maelezo kwa umma kuhusu tuhuma zinazomkabili.

  Kutokana na msimamo huo, inaelezwa kuwa wameibuka baadhi ya wana-CCM wanaomkingia kifua Mkapa, ambao pia wamejipanga kwa kushirikiana na mitandao mingine ndani ya CCM kumng’oa mbunge huyo.

  Mbali na Vunjo, majimbo mengine ambayo CCM haiko salama ni pamoja na baadhi yaliyomo mkoani Mbeya, ikielezwa kuwa baadhi ya kambi ndani ya CCM zimeandaa wagombea watakaochuana na wabunge wa CCM kwa tiketi ya chama hicho katika kura za maoni.

  Majimbo mengine ambayo wabunge wa sasa wa CCM wameandaliwa wapinzani kutoka katika makundi pinzani ndani ya chama hicho ni pamoja na Nzega mkoani Tabora, ambalo Mbunge wake ni Lucas Selelii, Lupa mkoani Mbeya, ambalo mbunge wake ni Victor Mwambalaswa, ambako taarifa zinabainisha kuwa huenda mbunge wa zamani wa Jimbo hilo, Njelu Kasaka, akajitokeza kumpinga.

  Lakini mbali na makundi hayo, baadhi ya majimbo ambayo CHADEMA inatarajiwa kutoa ushindani ni pamoja na Mbeya Vijijini, ambako mbunge wake wa sasa Luckson Mwanjale alipata ushindi wa asilimia 35 ya waliopaswa kupiga kura.

  Taarifa zaidi zinaeleza kuwa Freeman Mbowe huenda akaenda kugombea ubunge katika jimbo lake la zamani la Hai ambalo kwa sasa mbunge wake ni Fuya Kimbita.

  Mkurugenzi wa masuala ya Bunge Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema, kuhusu uwezekano wa Mbowe kuwania ubunge pamoja na mikakati ya chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.  Mkurugenzi wa masuala ya Bunge Halmashauri wa CHADEMA, John Mrema
  ‘‘Ni mapema mno kusema kuwa Mwenyekiti wetu (Mbowe) atakwenda kugombea ubunge na kutogombea urais. CHADEMA ni chama kinachofuata demokrasia wagombea huchukua fomu na kupitishwa na mkutano mkuu. Hatua hizo zote bado hazijafikiwa,’’ alisema Mrema, ambaye naye taarifa zinabainisha kuwa huenda akagombea ubunge katika jimbo mojawapo mkoani Kilimanjaro.

  Lakini mbali na kutokuwa muwazi katika suala hilo, Mrema alisema Operesheni Sangara imekifanya chama hicho kutambua nafasi na nguvu zake ndani ya jamii ya Watanzania.

  ‘‘Ipo mikoa ambayo tuna uhakika wa kuongeza idadi ya wabunge. Kwa mfano, mkoani Mara tunataraji kutwaa majimbo saba. Na mikoa mingine tunayotarajia kupata wabunge ni pamoja na Dar es Salaam, Mwanza.’’

  Alisema mikoa ya Kigoma, Kilimanjaro, Arusha na baadhi ya mikoa mingine idadi ya wabunge wa chama hicho wanataraji itaongezeka kutokana na mwitikio wa wananchi kuhusu utendaji wa chama hicho.

  Taarifa nyingine zilizotufikia zinabainisha kuwa hivi karibuni taasisi moja ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ilifanya utafiti katika majimbo 10 nchini ili kubaini kama wabunge wa sasa wanaweza kung’olewa au la.

  Baadhi ya majimbo yaliyohusishwa na utafiti wa taasisi hiyo ni pamoja na Karatu, ambalo Mbunge wake ni Dk. Wilbroad Slaa (CHADEMA), Kigoma Kaskazini-Kabwe Zitto (CHADEMA), Urambo Mashariki-Samuel Sitta (CCM), Mbozi Mashariki-Godfrey Zambi (CCM), Simanjiro-Christopher ole Sendeka (CCM), Mpanda Kati-Saidi Arfi (CHADEMA) na Moshi Mjini-Philemon Ndesamburo.

  Kwa mujibu wa utafiti huo, baadhi ya majimbo imebainika kuwa ni vigumu kuwang’oa wabunge wa sasa kwa kura kupitia uchaguzi huru na wa haki.

  Utafiti katika majimbo hayo unaelezwa kulenga kusaidia kundi fulani katika siasa kutokana na kuonekana dhahiri kuyahusu majimbo yenye wabunge wanaokera baadhi ya wanasiasa, hususan wale wanaoguswa na tuhuma mbalimbali za ufisadi zilizoanikwa hadharani katika miaka ya karibuni.

  Source Raia mwema
   
 8. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #8
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mbowe kugombea ubunge nadhani ni hatua nzuri kwani pamoja na CCM kuboronga lakini bado naamini kabisa Rais J Kikwete atapewa ridhaa na wananchi kuongoza kwa muhula mwingine.Najua wapo watu wanao amini wapinzani wanaweza kuindosha CCM madarakani katika uchaguzi mkuu 2010,lakini tumeshuhudia wenyewe katika chaguzi ndogo za ubunge na udiwani namna wananchi wa Tanzania walivyo tayari kuwapa jukumu la kuendelea kuongoza nchi pamoja na matatizo yote waliyoifanyia taifa letu.Nawaomba viongozi wengine wa upinzani kujikita zaidi katika nafasi za ubunge na udiwani kwa maana ya kuvijenga vyama vyao kuanzia chini badala ya kukimbilia nafasi ya urais ambayo inaitaji mtandao mkubwa na imara.Mheshimiwa I Lipumba,A L Mrema,Dr S Mvungi na wengine jaribuni nafasi za ubunge ili kuongeza nguvu ya upinzani bungeni.
   
 9. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #9
  Feb 19, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
 10. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #10
  Feb 19, 2009
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,588
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Mbowe should have realised it yesterday, that he's not fit to run for president! Ubunge is a smart move for Mbowe, no regrets look ahead.
   
 11. Z

  Zanaki JF-Expert Member

  #11
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 1, 2006
  Messages: 544
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Urais wamwachie Mrema na Lipumba.Huku kushindwa-shindwa kila siku,kunapoteza hata imani kwa wananchi,kwamba hivi ni vyama ambavyo kamwe havitashinda.Na pia,vinaipa nguvu zaidi ile dhana kuwa upinzani wa kikweli utatoka CCM kwenyewe.

  Kila mtu anapenda kupenda au kufuata kitu chenye matokeo mazuri.Leo hii Tanzania,nina uhakika kuna mashabiki wengi wa Manchester United kuliko labda Yanga au Simba,nayo ni kwa sababu wanashinda mara nyingi

  Kama kweli Mbowe atagombea ubunge,huo utakuwa ni mwelekeo mzuri sana.Hivi vyama ni lazima vi focus kwenye generation zijazo.CCM had a head start,na wao ni lazima wajue wapi pa kuanzia na namna ya kufika huko kwenye ushindi.Ushindi ni lazima uwe ni kitu gradual,sio mkupuo wa kwanza tu.Vitu vyote vyenye mafanikio huwa vinaanza kidogo-kidogo.

  Kwa mtazamo wangu,wakati wa kuishinda CCM ulikuwa ni uchaguzi wa 1995,baada ya kuwakosa hapo,ndio basi tena...sasa inaelekea kuwa kama wamewafungulia kadirisha tena sasa hivi,ingawa sio kakubwa kama ka 1995
   
 12. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #12
  Feb 19, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Yote semeni lakini ni muhimu kwa CHADEMA kusimamisha mgombea wao wa URAIS. Swali gumu ambalo linaweza kuwa na jawabu rahisi ni nani wa kugombea nafasi hiyo kupitia chama hicho ambaye ana sifa ya kuaminiwa na watanzania walio wengi kuwa ataweza kuheshimu na kumudu majukumu ya urais wa nchi yetu na kuwa mbadala wa kweli wa marais watokao CCM.

  Ni muhimu CHADEMA kusimamisha mgombea urais kwa kuwa hilo linasaidia sana chama kukua na linawapa chama chao nafasi zaidi ya kunadi sera za chama chao kuliko wakati mwingine wowote ule kisiasa.

  Vilevile, kwa kutumia mfumo wa PRIMARIES kama ilivyokuwa katika uchaguzi uliopita, CHADEMA wanafaidika kama asasi katika kupanua wigo wa ushindani wa kidemokrasia ndani ya chama hivyo kuboresha utamaduni wa demokrasia miongoni mwa viongozi na wanachama wao.

  Suala la kuunga mkono wagombea wa vyama vingine ambavyo tofauti na CHADEMA vingi vyao vimeshindwa kuonyesha kukua kimikakati, kiasasi na pengine hata kupoteza mvuto kwa watanzania, lije pale tu vyama vingine binafsi ama kwa pamoja wakaja na wagombea wapya tofouti na wale tuliowazoe ambao wataendana na mahitaji na taswira ya wakati wa sasa na ujao, kisiasa, kiuchumi na hata kijamii.....

  Kama kweli MBOWE ameamua na atakuwa tayari kusimamia uamuzi wake wa kugombea UBUNGE badala ya Urais basi nampa pongezi za dhati kwa kushinda kutambua alama za nyakati na kushinda matamanio ya UHESHIMIWA SANA na hivyo kutoa nafasi nyingine zaidi ya CHADEMA kukua kiasasi....

  Naamini vyama vingine haswa chama cha CUF nao watachukulia hili kama changamoto ya wao pia kuchukua maamuzi mazito kwa maslahi ya maendeleo ya demokrasia nchini mwetu(TANZANIA).

  Omarilyas
   
  Last edited: Feb 19, 2009
 13. Nono

  Nono JF-Expert Member

  #13
  Feb 19, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 1,305
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Mimi nitoe sifa kemkem kwa CHADEMA kwa mikakati yake.
  Naamini kama watu ni wafiatialiji wazuri wa siasa za Tanzania mtafahamu vyema hatua ambazo chama kama CHADEMA walipitia hadi kufikia hapa walipo. Mwaka 2000 Mbowe alipochaguliwa HAI alikuwa mbunge machachari sana na aliyependwa pia na wanajimbo wake. Alikuwa na nafasi kubwa sana ya kushinda tena katika jimbo la Hai. Ila waliona mbali zaidi ni ndipo walipoamua kujitoa muhanga kumsimamisha kuwa mgombea urais ili waweze kuweka ramani ya CHADEMA Tanzania. Walifahamu wazi kabisa kuwa wasingeshinda, lakini wangeweka misingi ambayo leo hii hakuna ubishi wowote pale Tanzania hii. Naamini ilikuwa ni vigumu kukubali kujitolea kuutupa Ubunge kama ninavyoamini kuwa alifanya Mbowe kwa nia ya kusambaza mizizi ya CHADEMA Tz.

  Katiba yetu inawaminya hawa watu wenye ushawishi mkubwa kama, kina Lipumba, Mrema wakati huo na Mbowe ambao pamoja na kwa vipindi mbali mbali kujipatia kura asilimia kubwa za urais ambazo hazikuwezesha kuongoza, lakini hawakupata japo ubunge ili waweze kuyasema yale wanayoyaamini kwa msalahi ya Watanzania. Mimi nadhani ni busara katiba yetu ikaruhusu kuwa anayepata angalao 5% ya kura za urais awe mbunge moja kwa moja, au wapewe nafasi za kugombea ubunge na urais wakati huo huo, na anaeshinda urais basi anapoteze ubunge kama ilivyo marekani. Nasema hivi kwa sababu ya demokrasia yetu changa ambayo imetawaliwa zaidi na dola ambapo ni vigumu kuwapata watu wengi waliotayari kutoa sauti zao. Kitendo cha kuwatega watu, mfano Dr. Slaa akagomee urais halafu akishindwa ni bao moja wapo la kuumaliza upinzani ambapo hauleti afya kwa ustawi wa taifa letu.

  Lakini kwa vyovyote vile, piga uwa CHADEMA lazima msimamishe mgombea urais
   
 14. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #14
  Feb 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,548
  Likes Received: 18,218
  Trophy Points: 280
  Naunga mkono uamuzi wa Mbowe kugombea ubunge. Kwa utafiti usio rasmi, mikoa ya watu walioenda shule, CCM haipendwi sana ila hujikuta CCM ikichaguliwa kwa sababu hakuna mgombea serious toka upinzani.
  Mbatia pia hauwezi urais, arejee Moshi Vijijini ataipiga CCM kumbo kwa mbali. Katika uchaguzi wa 1995, Mbatia alikuwa mmoja wa wabunge vijana waliochaguliwa kwa kura nyingi kabisa. Mbatia aliingia bungeni kwa ushindi wa kura zaidi ya 69,000. Hata baada ya CCM kuligawa, jumla ya kura zote, haijafikia zile za Mbatia za 1995. Kwa maneno mengine wengi walisusa kupiga kura.
  Kama kweli upinzani unataka kuwa serious, waungane wasimamishe mgombea mmoja anaekubalika kila jimbo ili kuleta upinzani wa dhati dhidi ya CCM. Urais Dr. Slaa hauziki, huyu aendelee kulitetea jimbo lake la Karatu ambapo Chadema ina nguvu kubwa ya madiwani. Lipumba nae aende jimboni Tabora. mrema ajaribu bahati yake Moshi maana 'he is almost a gone case'.
  John Cheyo akisimama na JK, wao pekee, JK atakuwa na hali mbaya. Ikipigwa kampeni kubwa ya ukweli kwa kuutumia udhaifu wa JK, CCM Chini!. Tatizo ni wapinzani hawana line-up ya kushiba kuendesha nchi. Hiyo kuliko kushinda na kuboronga, bora upinzani ujinyakulie majimbo mengi bara na kujipanga kuchukua nchi 2015 by that time, Zito atakuwwa ameiva.
  Kwa upande wa Zanzibar, Cuf itashinda kwa kishindo kama watamsimamisha Juma Duni ama Hamad Rashid
  Hata baadhi ya wana CCM watamchagua. Ukweli ni kuwa Juma Duni ama Hamad Rashid wana siasa za staha na hawana visasi. Sheif Sharif anaonyesha amekamia sana, anasiasa za jazba, na ukimuona macho yake, anaonyesha ana hasira na uwezekano wa kulipiza kisasi, vitu vinavyofanya japo huwa anashinda lakini hawezi kupewa nchi. Pia ile asili ya Uarabu ya Sharif inafanya aonekane kama mwana Sultani, hivyo kumkabidhi nchi pia kutahatarisha -muungano na hata Mapinduzi Matukufu (ya umwagaji damu) ya Zanzibar.
   
 15. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #15
  Feb 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Mbowe pamoja na kuwahi kuwa Mbunge, lakini hakuweza kufanya chochote kwani ngazi hiyo ilikuwa kubwa sana kwake.

  Nina heshima kubwa kumshauri yeye binafsi na chama cha chadema kuwa inafaa Mbowe agombee Udiwani katika wadi yoyote pale Dar, ili aje kugombea Umeya wa Jiji. Ustahiki Meya ndio kazi inayomfaa hasa!
   
 16. Nyumbu

  Nyumbu Senior Member

  #16
  Feb 20, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 141
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very good idea Kibunango. Kwa mtazamo huo 99% ya wabunge bubu wa ccm itabidi wagombee udiwani.
   
 17. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  CCM kuwa na wagombea wanaovutana sio jambo kubwa au la kukupa tamaa kuwa utaweza kunyakuwa ushindi kirahisi, alikuwepo Hilary na Onyango waote kutoka chama kimoja kampeni zao tuliziona na kuzifuatilia kwa karibu lakini mwisho wake Onyango alishinda na kupewa dhamana ya kuwakilisha Chama chake huku Hilary akiwapa changamoto wafuasi wake kuhamishia majeshi na kumuunga mkono Onyango.
  Tatizo lilipo kwa hapa Tanzania ni wananchi kuwa na uzoefu wa kupokea mataputapu,kanga na kofia na wakishapokea hayo inakuwa hawasikii wala hawaoni isipokuwa wao ni kuipa kura CCM ,bado wananchi wa Tanganyika hawajaamua kuiondoa CCM ndipo Chiligati aliposema Nchi imetulia kutulia wenyewe ni kushinda kiulaini bila ya purukushani kama zitokeazo Zanzibar ,waTanganyika bado ni woga katika kulinda kura zao ,bado wanapokea rushwa kuuza kura zao ,bado wanadanganyika kwa takirima ndogondogo hivyo kinachotakiwa ni kuwaamsha hawa wapiga kura wale kila kitu watakachopewa na CCM lakini kura yao tu wasikubali kuipeleka CCM.
   
 18. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Kaka uko kaskazini zaidi ya dunia huko unajuaje ya Tanzania na zaidi ya Hai? Salamu wazee wa huko....

  Omarilyas
   
Loading...