Mbowe: Kuwajengea wananchi miradi mikubwa siyo msingi wa amani

Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,039
2,000
Hivi karibuni Mh. Mbowe aliweka wazi kuwa baadhi ya watu wanaumia, wanaonewa hawana uhuru wananungunika! Hii ni kauli akiwa mbele ya Mh. Rais wetu tar 9.12.19 pale Mwanza. Na aliomba maridhiano ya Kitaifa. Ukipitia maoni ya wengi mitandaoni, wanashutumu kauli ya Mbowe.

Hata hivyo, kwa maoni yangu, bado ninasisitiza,alikuwa sahihi. Mfano rahisi ni Uchaguzi wa Serikai za mitaa. uliopita. Nina jirani yangu Mwenyekiti wa mtaa - ccm amenisimulia anavyoshindwa kuunganisha watu wake, kisa manunguniko . Wanasema hawajamchagua ! Waliyemtaka aliondolewa jina . Huu ni mfano mdogo tuu. Siku za mwisho za Gadaffi ( inajua siyo mfano mzuri). Alilaumu raia wake kwa kukosa fadhila za kupewa bara bara nzuri,elimu na afya bure, niliozesha vijana wenu bure nk.

Leo mmeamua kuungana na makafiri Wazungu kuniua, nilijua hamtaweza kumbe sikuwasikiliza!!!! Manunguniko katika jamii zetu hata kama yatatoka kwa wachache,hukua na kupata waungaji mkono ambao huwa tishio mbeleni. Sipendi nchi yangu ifike huko, muda ni huu kama ali vyoshauri Mh. Mbowe.
 
Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
10,171
2,000
Demokrasia ndio msingi.. kama hujui hata nyani kwenye vikao vyao husikilizana na kupiga kura.

Kama hakuna demokrasia, hakjna maendeleo.

Nchi kama sweden na norway mbona zipo vizuri na sina demokrasia.

Pepo gani tupo Tanzania.

Wanaoweza kusoma albadiri wafanye hima.. tanzania yetu inapotea.

Eti mnajitoa mahakama ya haki za binadamu?

Mnataka kutu ua watanzania wote?

Nini hasa sababu ya kuikimhia mahakama ya haki za hinadamu kama mpo vizuri?
Hivi karibuni Mh. Mbowe aliweka wazi kuwa baadhi ya watu wanaumia , wanaonewa hawana uhuru wananungunika! Hii ni kauli akiwa mbele ya Mh. Rais wetu tar 9.12.19 pale Mwanza. Na aliom ba maridhiano ya Kitaifa. Ukipitia maoni ya wengi mitandaoni, wanashutumu kauli ya Mbowe. Hata hivyo, kwa maoni yangu, bado ninasisitiza,alikuwa sahihi. Mfano rahisi ni Uchaguzi wa Serikai za mitaa. uliopita. Nina jirani yangu Mwenyekiti wa mtaa - ccm amenisimulia anavyoshindwa kuunganisha watu wake,kisa manunguniko . Wanasema hawajamchagua ! Waliyemtaka aliondolewa jina . Huu ni mfano mdogo tuu. Siku za mwisho za Gadaffi ( ninajua siyo mfano mzuri). alilaumu raia wake kwa kukosa fadhila za kupewa bara bara nzuri,elimu na afya bure, niliozesha vijana wenu bure nk. Leo mmeamua kuungana na makafiri Wazungu kuniua, nilijua hamtaweza kumbe sikuwasikiliza!!!! Manunguniko katika jamii zetu hata kama yatatoka kwa wachache,hukua na kupata waungaji mkono ambao huwa tishio mbeleni. Sipendi nchi yangu ifike huko, muda ni huu kama ali vyoshauri Mh. Mbowe.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fursa Pesa

JF-Expert Member
May 30, 2012
3,341
2,000
Kwa maana hiyo agenda ya upinzani kwa sasa ni amani?
Mbona amani tunayo siku zote.
Vipi kuhusu agenda zao za zamani nini tasmini yao?
Ningefikiri labda wangeliomba baadhi ya wizara wapewe wao 2020 ili tuwapime.
 
USSR

JF-Expert Member
Jul 15, 2015
3,627
2,000
Naona wajinga mmekutana mnapongezana tangu1992 ni mapambano ya siasa tu hakuna kilichofanyika hakuna lolote

Mwacheni afanye yake ,chadema wenyewe hawana demokrasia ya ndani

USSR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
30,402
2,000
Usichojua ni kwamba, waliomkataa Gaddafi walikuwa sio walibya ni hao hao amabo wewe na Mbowe mnawashangilia
Walibya walimchoka Gaddaf kama tulivyoichoka ccm hapa nchini, lakini kwakuwa alikuwa na maamuzi kwenye vyombo vya dola. Basi aliweza kuchezea box la kura kama afanyavyo Magufuli na ccm hapa nchini kwa kutumia vyombo vya dola kuendelea kukaa madarakani. Mataifa ya nje yaliingilia kati baada ya kujua fika Gaddafi alikuwa na nguvu ya dola hivyo wananchi wasingemudu bila msaada wao. Lakini wananchi kabisa wa Libya ndio waliomua Gaddaf. Hata hapa nchini wazungu pekee ndio wataweza kutuondolea huu ukandamizwaji kwani tayari ccm wanamaamuzi ya vyombo vya dola.
 
Kididimo

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
3,039
2,000
Kwa maana hiyo agenda ya upinzani kwa sasa ni amani?
Mbona amani tunayo siku zote.
Vipi kuhusu agenda zao za zamani nini tasmini yao?
Ningefikiri labda wangeliomba baadhi ya wizara wapewe wao 2020 ili tuwapime.
Kenya jirani hapa wameridhia kujenga umoja wa Kitaifa. Wanaenda vzr sana,nadhani wazo la Mbowe bado ni jema.
 
LESIRIAMU

JF-Expert Member
Feb 12, 2008
5,567
2,000
Hata kama walio mchukia Gadafi ni wazungu, lakini hata baada ya kumkuta Gadafi kwrnye mtaro wazungu hawaku muua waliwaacha Walibya wamuue. Kama Walibya walikuwa wanampenda wange mbeba wakimbie nae. Acha comment zisizo na rejea
Usichojua ni kwamba, waliomkataa Gaddafi walikuwa sio walibya ni hao hao amabo wewe na Mbowe mnawashangilia
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
34,885
2,000
Usichojua ni kwamba, waliomkataa Gaddafi walikuwa sio walibya ni hao hao amabo wewe na Mbowe mnawashangilia
Usipotoshe kabisa. Walio mkataa Gaddafi ni walibya kwa matendo yake ya kuminya Uhuru na hao mnaoita mabeberu wakapata mwanya wa kuchochea na kusaidia kumuondoa.
Hakuna kitu kibaya kunyanyasa binadamu, hata mwanao ukimfanyia mambo yote mazuri lakini ukamnyanyasia Uhuru wake utashangaa atakacho kifanya akipata nafasi.
Hao mnao ona wamevaa kijani Leo na kuwashangilia mtashangaa ndio watawacharaza bakora (kama sio vijiti vya Gaddafi) siku moja, muulizeni Mugabe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
warthog gun

JF-Expert Member
Aug 9, 2018
1,471
2,000
Demokrasia ndio msingi.. kama hujui hata nyani kwenye vikao vyao husikilizana na kupiga kura.

Kama hakuna demokrasia, hakjna maendeleo.

Nchi kama sweden na norway mbona zipo vizuri na sina demokrasia.

Pepo gani tupo Tanzania.

Wanaoweza kusoma albadiri wafanye hima.. tanzania yetu inapotea.

Eti mnajitoa mahakama ya haki za binadamu?

Mnataka kutu ua watanzania wote?

Nini hasa sababu ya kuikimhia mahakama ya haki za hinadamu kama mpo vizuri?

Sent using Jamii Forums mobile app
Trump hakukosea kutuita shimo la choo, watawala wetu mambo wayafanyayo ni shithole hovyo kabisa.
 
Patriot

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
4,741
2,000
Hivi karibuni Mh. Mbowe aliweka wazi kuwa baadhi ya watu wanaumia, wanaonewa hawana uhuru wananungunika! Hii ni kauli akiwa mbele ya Mh. Rais wetu tar 9.12.19 pale Mwanza. Na aliomba maridhiano ya Kitaifa. Ukipitia maoni ya wengi mitandaoni, wanashutumu kauli ya Mbowe.

Hata hivyo, kwa maoni yangu, bado ninasisitiza,alikuwa sahihi. Mfano rahisi ni Uchaguzi wa Serikai za mitaa. uliopita. Nina jirani yangu Mwenyekiti wa mtaa - ccm amenisimulia anavyoshindwa kuunganisha watu wake, kisa manunguniko . Wanasema hawajamchagua ! Waliyemtaka aliondolewa jina . Huu ni mfano mdogo tuu. Siku za mwisho za Gadaffi ( inajua siyo mfano mzuri). Alilaumu raia wake kwa kukosa fadhila za kupewa bara bara nzuri,elimu na afya bure, niliozesha vijana wenu bure nk.

Leo mmeamua kuungana na makafiri Wazungu kuniua, nilijua hamtaweza kumbe sikuwasikiliza!!!! Manunguniko katika jamii zetu hata kama yatatoka kwa wachache,hukua na kupata waungaji mkono ambao huwa tishio mbeleni. Sipendi nchi yangu ifike huko, muda ni huu kama ali vyoshauri Mh. Mbowe.
Wewe jamaa unachanganya mambo sana! Sasa anachofanya Magufuli, huku akina Mbowe wakilaani kina tofauti gani na walibya waliomkataa Qaddafi? Mbowe amezidi na nadhani munampa ushabiki unaozidi uwezo wake.

Miaka yote tatizo kubwa la serikali ilikuwa kushindwa kufanya miradi ya maendeleo. Kila senti ilikuwa ni kusafiri na kula bata. Bajeti ikawa na sehemu kubwa inayoitwa ni ya 'chai'. Wakati huo akina mbowe hawakuona ni tatizo sana kama sasa hivi maana na wao walikuwa sehemu ya walaji bata. Sasa miradi inaonekana halafu kelele zinazidi eti sasa wanahitaji sana uhuru wa kutoa hotuba. Hotuba zipi toka kwa Dj?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom