MBOWE kuwafunga 'spidi gavana' wakorofi CHADEMA; Wamo Wabunge na madiwani | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MBOWE kuwafunga 'spidi gavana' wakorofi CHADEMA; Wamo Wabunge na madiwani

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Sep 27, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  *Hasa waropokaji na wapotoshaji wa sera za chama

  Rai | Alhamisi, Septemba 27, 2012

  IMEBAINIKA mambo si shwari kabisa ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Hayaendi sanjari na juhudi za viongozi wa juu na kada za kati, kuacha kuzingatia misingi na sera za kukiwezesha kujenga muonekano na mwelekeo mzuri. Hususani kuepuka kuwa chanzo cha vurugu, badala ya kuhimiza shughuli za maendeleo ambayo ndiyo misingi mikuu ya kukiwezesha kupata ushawishi katika umma. Kuaminika kuwa kinaweza kuwa mbadala wa CCM.

  Habari za kiuchunguzi zilizofanywa na gazeti la Rai, kwa kufanya mahojiano, tathmini na tafsiri za wataalamu wa masuala ya siasa, wengi wana maoni mchanganyiko juu ya CHADEMA. Wanakieleza kama chama cha siasa, ambacho kimekuwa katika harakati za kujijenga, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, kwa kupitia kaulimbiu za operesheni sangara, vua gamba vaa gwanda, na M4C-Movement for Chage.

  Miongoni mwa maoni ni ya kuutaka uongozi wa ngazi ya taifa hasa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, kwa kutumia busara zake, ndiye mtu pekee mwenye uwezo wa kuwafunga "Spidi Gavana" wanachama wa Chadema, wakiwemo wabunge, madiwani na viongozi wa ngazi mbalimabali. Ni kukifanya chama kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia taratibu, sheria na kanuni zilizopo za uendeshaji wa shughuli za vyama vya siasa nchini.

  Ni wazi kwamba Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, ni mwenye kauli ya mwisho katika uendeshaji wa vikao kwa mujibu wa sera, taratibu na sheria ambazo kila mwanachama anapaswa kuzizingatia na kuzifuata. Hivyo Mwenyekiti, sambamba na Katibu Mkuu Dk. Willbod Slaa, ni nguzo muhimu juu ya kutoa uamuzi sahihi wenye maslahi ya chama, alibainisha mchambuzi ambaye ni mwanachama hai na mkereketwa na mdau mkuu ndani ya CHADEMA.

  Katika kipindi chote tangu kuanza kwa zile zinazoitwa operesheni za kukijenga na kukiimarisha chama, kumekuwepo na matukio yasiyoonyesha mwelekeo mzuri katika mustakabali wa mfumo wa uendeshaji wa vyama vingi vya siasa nchini.

  Hali ilivyo sasa nchini siyo shwari, hali imekuwa ikishuhudiwa kuibuka kwa tabia ya kupenda kuendekeza zaidi kufanya ghasia, kupambana na mamlaka za dola. Baadhi ya wanasiasa akiwamo kiongozi wa operesheni sangara, Benson Kagaila, wamekuwa mstari wa mbele kuhamasisha vijana, na wadau. Mara nyingi wadau wamejazwa hasira na kupandishwa jazba, kiasi cha kudiriki kukaidi amri na sheria na kusababisha kuingia katika mitafaruku na mikanganyiko katika jamii yenye utulivu.

  Mwenendo huu unaweza kuchafua taswira, malengo na makusudio ya CHADEMA, chama ambacho kimekuwa kikivutia maelfu ya watu kushiriki katika kujiunga, na kukiimarisha kuanzia ngazi ya shina kwa kunadi sera zake katika jamii.

  Tangu kumalizika kipindi cha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, inaonekana wazi kuna watu wasioona mbele wakiwamo wabunge, madiwani na wadau mbalimbali kwa makusudi kuacha kuzingatia taratibu na sheria, hasa baada ya matokeo ya uchaguzi huo.

  Yako mambo mengi ambayo yanaelezwa na wachambuzi na kutafsiriwa kwa mtazamo kuwa baadhi ya watu kwenye jamii wamebadilika mienendo yao. Kila kukicha wanadai nchi imeharibika, eti hakuna jema bali mambo yote ni mabaya (hasi) tu.

  Yamkini wanasiasa na wadau wanapaswa kutuliza akili na mawazo yao. Waanze kupima mambo yote wanayofanya, watathmini na kuchambua kwa kina ni masuala gani yana mashiko na faida, katika taifa letu na jamii kwa ujumla.

  Hali katika baadhi ya mikoa haitabiriki, siyo shwari, tafsiri hii inatokana na duru za uchunguzi na mahojiano na watu mbalimbali katika mikoa hiyo. Matukio yasiyo ya kawaida ya uvunjifu wa amani yameongezeka kuanzia majiji ikiwamo Arusha, Mwanza, Mbeya, na miji ya Morogoro na Iringa.

  Uvumilivu na upendo umeanza kutoweka, imebainika zaidi ni miongoni mwa vijana, wadau na wakereketwa wa siasa. Wamekuwa watu wa jazba na hasira za kutisha. Wengi wao wanaonekana kupandisha mori kutokana na matamko ya wanasiasa, wakiwamo wabunge na madiwani.

  Taswira sahihi juu ya matokea ya operesheni zote kuanzia sangara, vua gamba vaa gwanda, na vuguvugu na harakati za mabadiliko (M4C), yamkini zimechangia kuwepo mikanganyiko. Ni mwendelezo wa matukio ambayo yanabainisha kuongeza kwa uhasama kuliko uhusiano mwema.

  Wataalamu, wanazuoni wa masuala ya siasa, wana mtazamo na tathmini endelevu, wanafafanua kuwa siasa ya vyama vya upinzani siyo ugomvi wala uhasama. Ni njia ya kupanua wigo wa demokrasia kwa kukosoa, kusahihisha na kurekebisha kasoro. Kutumia njia ya majadiliano kwa kujenga hoja zenye nguvu kwa ustaarabu. Kuvumiliana hata kama kuna kutofautiana kimawazo na kimtizamo juu ya masuala mbalimbali.

  Mwenyekiti wa CHADEMA, ambaye pia ni kiongozi wa upinzani kitaifa, ndiye mwenye uwezo wa kuwafunga "Spidi gavana" wale wakorofi na wavurugaji wa sera sahihi za chadema.

  Baba wa taifa Mwalimu Nyerere aliwahi kukisifu na kukiunga mkono chama cha CHADEMA kwamba kina sera nzuri. Mwalimu hakukosea hata kidogo, lakini baada ya miaka 13 tangu ametutoka, CHADEMA kimeweka kando zile sera nzuri alizozisifia Mwalimu, sasa kimeamua kukumbatia na kuendesha chama kwa sera za wanaharakati.

  Mwenyekiti na Katibu Mkuu CHADEMA, waongoze wadau kufanya kazi ya kunadi sera kwa njia ya amani na mshikamano wa kitaifa, badala ya kubomoa misingi ya utaifa tuliyoachiwa na Mwalimu Nyerere.

   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Sep 27, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Kutokuelewana kwa WANACHAMA wa CHAMA KIMOJA ni DEMOKRASIA, lakini ni bora kuwasiliza na kuangalia Uwezekano wa kubadilisha hizo hoja na sio KUFUKUZANA kutoka kwenye CHAMA...

  Kukiwa na Muungano ya watu zaid ya wawili ni Lazima HOJA zitatofautiana na lazima zisahihishwe na sio kufukuzana... USA - Sio All Democrats wanampenda OBAMA... kuna state inaitwa WEST VIRGINIA ni CONCERVATIVE

  DEMOCRATS... Hawampigii Kura OBAMA wanapigia kura Rais REPUBLICAN lakini Wabunge na Madiwani wengi ni DEMOCRATS... Siasa ndani ya CHAMA MATABAKA kuwa PAMOJA ni UHAI WA CHAMA...
   
 3. Mshindo

  Mshindo JF-Expert Member

  #3
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 479
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kumbe ni gazeti la RAI... (Rostam Aziz Incorporated).:blah:
   
 4. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #4
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  Hivi kumbe M4C imewashikia penyewe..........

  Sasa subirini na hii nyingine mje muuwe na watu wengine tena koz tutaanza pasipo kuchoka wala kulala, pia siasa za harakati ndizo sahihi kwenye nchi kama yetu yenye mfumo mbovu wa ukandamizaji, Pia sasa hivi hata msemeje sisi kamwe hatutarudi nyuma kamwe....

  The sruggles aluta continua.
   
 5. U

  UZEE MVI Senior Member

  #5
  Sep 27, 2012
  Joined: Feb 6, 2011
  Messages: 192
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Akili ni nywele..
   
 6. F

  FJM JF-Expert Member

  #6
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Sijui huyo mwandishi wa gazeti la RAI anaelewa nini kuhusu kazi za vyama vya siasa na majukumu ya serikali.

  Chama chenye dola kwa Tanzania bara ni kimoja tu - CCM. Na serikali ya CCM ndiyo inayokusanya kodi, inakodisha mashamba, inapokea misaada ya mbalimbali ikiwemo misaada kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Pia serikali ya CCM ndiyo inaandaa bajeti na kuipeleka bungeni kuomba ridhaa ya wananchi kupitia kwa wawakilishi wao (wabunge) waidhinishe mapato na matumizi ya fedha ya umma.

  Sasa haya mambo ya kulaumu CHADEMA yanatoka wapi? CHADEMA wawe afisa miradi? Na hao wanaopekea kodi wafanye nini na hela ya umma, kuweka Swiss?

  Sijui nani ameandika huo upuuzi, maana kajichanganya kuliko mwanafunzi wa darasa la sita! Anasema CHADEMA hakujatulia kwa sababu hawahamasishi miradi ya maaendeleo, wakati huo huo anasema kama wanataka kuimarika (CHADEMA) Mwenyekiti - Freeman Mbowe awafunge wabunge wake 'speed governor'. Ghafla anarukia kwenye zilipendwa za 'amani na utulivu'. Nahisi Tendwa kwa kushirikiana na Benson Bana ndio wameandika huu waraka.
   
 7. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #7
  Sep 27, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Well said
   
 8. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #8
  Sep 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,273
  Trophy Points: 280
  Haya ni mawazo ya muandishi, ili mradi mkono wake uende kinywani, hana tofauti na fisi anayemfata binadamu nyuma akidhani mkono utadondoka ili apate kitoweo. uandishi wa namna hii ndio unaonifanya nione kwamba nchi hii hakuna haja ya kusomea taaluma ya habari, maana ni vigumu kumtambuwa aliyesoma na kanjanja.
   
 9. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #9
  Sep 27, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,744
  Likes Received: 1,454
  Trophy Points: 280
  Pamoja na kuwa sijaona chili sosi ya hii habari, ni rahisi kujua tu inatokea upande gani. Nchi ya unknown flying objects hii bana!
   
 10. M

  Molemo JF-Expert Member

  #10
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Mhariri mkuu RAI ni Prince Bagenda.
   
 11. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #11
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Chama kina hali mbaya mwanza hadi mbunge anajificha kwenye uvungu wa meza
   
 12. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #12
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Uchambuzi yakinifu.
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Elimu ya Uraia! watu wengi hawana na wala hawataki..M4C wamejitolea kuitoa bureee lakini bado kuna mijitu inaona shida hata kusikiliza tu.. shule haikupanda basi hata hotuba wanaona wanapoteza muda wao..
   
 14. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #14
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Haikuwa sahihi kuwavua uanavhama adam chagulani na matata,mgogoro uliokikumba chama arusha ungepaswa kuwa funzo tosha kabisa
   
 15. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #15
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  tatizo m4c inahamasisha vurugu,watu wameshtuka,saivi inaitwa m4v yaani movement for vurugu
   
 16. M

  Mkandara Verified User

  #16
  Sep 27, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Safi kabisa kama inaitwa M4V ikiwa lengo lao ni kukuelimisha wewe lakini Polisi hawataki uelemike. Kama vurugu zao zingekuwa na raia wa kawaida na sio Polisi hapo ungenimaliza lakini Vurugu zao zina malengo ya kumwelimisha raia na serikali inataka wananchi waendelee kuwa wajinga..Kwa hiyo V inaweza kusimamia Values
   
 17. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #17
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  tena wale ambao we unawaamini ndio huandika uchafu afadhali hata huyu amekaribiana na kweli tupu
   
 18. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #18
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Another **** from Rai. Masterminder wa hii kitu ya Rai anajulikana. Kazifanya huko kwenye magazeti yao ya ajabu ajabu, ameshindwa wakamrudisha 'nyumbani'. Tunaojua industry tunawaheshimu na kuwakubali baadhi ya waandishi wa NHC. Bahati mbaya sana Rai inaendelea kuathirika.

  Badala ya watu kuhangaika irudi kwenye chati ya awali, wanahangaika kuididimiza. Kwa stori hizi za kutunga, Mhariri mzima anaweka headline kubwa isiyokuwa na uhusiano na stori, ni wazi wanazidi kulichimbia kaburi kabisa.

  Lakini lazima tuwasikitikie waandishi wanaoumia kwa mambo wanayofanyiwa kwa misingi ya taaluma yao kuvunjwa vunjwa kwa misingi ya taaluma yao, lakini wanalazimika kuumia kimoyo moyo.

  Yaani stori haisemi ukweli kuanzia headline mpaka mstari wa mwisho, isipokuwa nukta ya mwisho. Ni aibu kubwa.
   
 19. T2015CCM

  T2015CCM JF-Expert Member

  #19
  Sep 27, 2012
  Joined: Sep 13, 2012
  Messages: 7,924
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  siasa tu hiyo hamna lolote,polisi wapo tangu uhuru hawajawafanyia wananchi vurugu,kwann leo?lazima uwe makini kidogo kutambua hili. Wenye uchungu zaidi na kujua madhara halisi ya hizi vurugu za m4v ni wale waliofiwa na ndugu zao na waliojeruhiwa
   
 20. AdvocateFi

  AdvocateFi JF-Expert Member

  #20
  Sep 27, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 10,705
  Likes Received: 592
  Trophy Points: 280
  wewe si huwa mwaa CUF tena mshabiki mkubwa wa Jussa na Lipumba.

  Sasa mambo ya CDM ya nn?
   
Loading...