Mbowe- Kurudisha gari uamuzi wa busara kwa usalama pia | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe- Kurudisha gari uamuzi wa busara kwa usalama pia

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Jun 25, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
  Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe

  Alipotakiwa na NIPASHE kueleza utaratibu alioutumia kulirejesha gari hilo, Mbowe alisema alifanya kama alivyokabidhiwa awali.Alisema baada ya kuchaguliwa kuwa Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hakupewa barua wala kusainishwa mahali popote nilipokabidhiwa gari hilo.

  Alisema badala yake, alionyeshwa gari hilo pamoja na dereva wa kuliendesha.

  “Nilipokuwa nikihitaji kulitumia, naenda tu pale, dereva anakuja. Sijui anatoka wapi, wala sijui yanatoka wapi,” alisema Mbowe.
  Swali hilo la NIPASHE kwa Mbowe, linafuatia kauli iliyotolewa na Kaimu Katibu wa Bunge, John Joel, ambaye Jumatano wiki hii, alisema ofisi yake haijapata barua yoyote kutoka kwa Mbowe inayoeleza uamuzi wake wa kurejesha gari hilo kwa Ofisi ya Bunge.

  Nipashe
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Jun 25, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa mtazamo wangu mtu unaonyeshwa tu gari lile na ukishafika kwenye gari dereva anakuja na kukupeleka unakotaka, hujui dereva anaishi wapi, ni nani na wapi gari huhifadhiwa, wakati huo huo ukiwa mpinzani mkuu wa serikali ni jambo la kuwa makini. Dereva unamtaka au humtaki huna jinsi lazima uwe tayari kwa ye yote watakayekuletea.
   
Loading...