MBOWE,KUPUNGUZA UBADHILIFU KWENYE HALMASHAURI Andaeni Wanachuo vyuo vikuu kugombea udiwani2015

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kuna haja ya kufanya hivyo sasa kwani

Madiwani wa vijijini wengi elimu ndogo hawapewi posho wanahongwa dili zinapitishwa.

ONGEZEKO LA VYUO HALILINGANI NA NAFASI ZA AJIRA ZINAZOTENGENEZWA HIVYO ITAAJIRI WAHITIMU KIBAO maslai watajiimarishia halmashauri zina hela

Watasaidia kupunguza uonevu unaofanywa na watendaji wa kata na vijiji. Wamejijengea jela jeshi(migambo) na vimahakama

Wanamvuto kwa vijana na wapigakura wengi ni vijana

Naamini kutakuwa na muhitimu wa chuokikuu kila kata kufikia 2015.

Kutaingiza harakati za ukombozi mpya mpaka vijijini.

ITAONGEZA UMAARUFU WA SIASA NCHINI
 
Ni wazo zuri hasa wasomi hao wakigombea maeneo wanayotoka wanaweza kuleta changamoto kubwa.
 
Mkuu hii thread ni nzuri sana lakini nasikitika itakosa wachangiaji kwasababu wengi wao sana sana magamba wanataka thread za udaku Kama za tumtemeke. Kama ingekuwa ya udaku mbona ingeshafikia page ya 8. Hapa ritz rejao au tume ya katiba hawaingizi mguu
 
Mkuu ngoja nikuumbue kwa kuchangia;
Kwanza namuunga mkono mtoa mada swala la kuondoa ubadhilifu kama report ya CAG inavyoonyesha,
ila tatizo hao vijana toka vyuoni kugombea udiwani! wengi wao hao vijana wana high expectation watakubali uwatoe majijini!
Swala la ubadhilifu sio la kisiasa kama wewe mtoa mada unavyotaka tuamini hilo ni swala la kukosekana kwa maadili na uzalendo katika taifa letu.
 
udiwani na ubunge ingewekwa sheria mgombea sharti awe na degree kama tunataka ufanisi na uwajibikaji. Huwezi kuamini karibu asilimia 40 ya madiwani ni mbumbumbu, na wengine ni wajinga hawajui kusoma, kuandika na kuhesabu, nenda kwenye halmashauri unaweza kulia. Ikifanyika FORENSIC ACCOUNTING & AUDITING mbali na usanii wa CAG, wizi utakaogundulika kwenye halmashauri zetu, hakuna halmashauri ambayo haitachomwa moto Tanganyika.
 
Nivizuri kugombea! wasomi wote fanye hivyo! ila mjiandae kupokea changamoto ya wazee wa ccm huku vijijini, kwamba huyu bado ni mtoto mdogo! Hajaowa/hajaolewa, huyu elimu yake ni kubwa mno hatakiwi kuja kufanya kazi hizi. baada ya frastration zote hizo watasema tumaacheni aje agom bee kipindi kijacho atakuwa amekwisha komaa! nimeandika haya nikiwa na nzoefu kwani mimi ni muathirika wa hilo,ambae nilipotoka cuo kikuu niligombea udiwani nikakabiliana na yote hayo.Hata halmashauri pia wanahofu sana na wasomi.
 
Sidhani kama ubadhilifu unatokana na ukosefu wa elimu wa viongozi.
Kuna phd holders wengi wao ndio vinara wa ufisadi.
Ila inasaidia kwa viongozi hasa madiwani na hata wenyeviti wa mitaa wakiwa na elimu angalau itapunguza ukiritimba na kufanya kazi kwa mazoea.
 
In one wauy itapunguza kama si kumaliza kabisa wizi na ubadhirifu katika halmashauri zetu kwakuwa watendaji watajua kwamba madiwani wako vizuri huwezi kuwapelekea ripoti nyepesi wakakuelewa ama unaweza kuwahadaa kirahisi.
Nakumbuka wilayani serengeti madiwani waligoma kujadili mkataba wa mwekezaji mmoja kwakuwa umeandikwa kiingereza na wao hawaielewi lugha hiyo!
 
Sidhani kama ubadhilifu unatokana na ukosefu wa elimu wa viongozi.
Kuna phd holders wengi wao ndio vinara wa ufisadi.
Ila inasaidia kwa viongozi hasa madiwani na hata wenyeviti wa mitaa wakiwa na elimu angalau itapunguza ukiritimba na kufanya kazi kwa mazoea.

Case study Prof. Mahalu
 
Dr Mahalu alikuwa diwani? Watu hawaelewi kazi za madiwani ndo maana hawaelewi mantiki ya mtoa hoja hapo juu. Diwani ndo wanasimamia pesa zote za serikali za mitaa ambazo ni zaidi ya nusu ya bajeti ya taifa na huko ndiko kuna tatizo kubwa la ufisadi. Ukiwa na madiwani wasomi hawatadanganywa na wakurugenzi na maafisa wengine wa halimashauri kupitisha mambo bila ufafanuzi wa kina.
 
DR. Mahalu ametajwa kwa sababu topic imetaja uhusiano kati ya elimu na ufisadi kwahiyo mfano wa mahalu ulikuwa perfect na pia tusiawasahau wakina chenge na dr.bilali pia wamo. na kingine cha msingi ni kuzipa mamlaka kamili hamashauri kuweza kufanya kazi yake bila kuingiliwa kwa mfano kuna mtu anaitwa mkurugenzi wa halmashauri mtu huyu ni hatari kwa sababu anafanya kazi kama mtumishi wa serikali kuendesha mijadala na kila kitu kwa maoni yangu ni watumishi waliochaguliwa moja kwa moja na watu ndio wangekuwa na mamlaka za mwisho na siyo un elected official ambao mara nyingi wanakuwa vikwazo vikubwa.
 
Dr Mahalu alikuwa diwani? Watu hawaelewi kazi za madiwani ndo maana hawaelewi mantiki ya mtoa hoja hapo juu. Diwani ndo wanasimamia pesa zote za serikali za mitaa ambazo ni zaidi ya nusu ya bajeti ya taifa na huko ndiko kuna tatizo kubwa la ufisadi. Ukiwa na madiwani wasomi hawatadanganywa na wakurugenzi na maafisa wengine wa halimashauri kupitisha mambo bila ufafanuzi wa kina.

DR. Mahalu ametajwa kwa sababu topic imetaja uhusiano kati ya elimu na ufisadi kwahiyo mfano wa mahalu ulikuwa perfect na pia tusiawasahau wakina chenge na dr.bilali pia wamo. na kingine cha msingi ni kuzipa mamlaka kamili hamashauri kuweza kufanya kazi yake bila kuingiliwa kwa mfano kuna mtu anaitwa mkurugenzi wa halmashauri mtu huyu ni hatari kwa sababu anafanya kazi kama mtumishi wa serikali kuendesha mijadala na kila kitu kwa maoni yangu ni watumishi waliokuwa moja kwa moja ndio wangekuwa na mamlaka za mwisho na siyo un elected official ambao mara nyingi wanakuwa vikwazo vikubwa.
 
Mkuu ngoja nikuumbue kwa kuchangia;
Kwanza namuunga mkono mtoa mada swala la kuondoa ubadhilifu kama report ya CAG inavyoonyesha,
ila tatizo hao vijana toka vyuoni kugombea udiwani! wengi wao hao vijana wana high expectation watakubali uwatoe majijini!
Swala la ubadhilifu sio la kisiasa kama wewe mtoa mada unavyotaka tuamini hilo ni swala la kukosekana kwa maadili na uzalendo katika taifa letu.

yap! Hao vijana waandaliwe kuwa waadilifu na wazalendo tangu vyuoni! Naamin INAWEZEKANA KABISA!
 
ni kweli tuwe na madiwani wenye vision na si madiwani wenye malengo ya kutatua matatizo ya maji, kujenga shule na zahanati. Madiwani walipwe laki 6 kwa mwezi ilikupunguza vishawishi vya hongo. Umezuka mtindo sasa hivi ambapo matajiri wanaungana kifedha kumsaidia diwani wanayemtaka ili ashinde nafasi ya uenyekiti ili wamtawale vizuri
 
Mkuu ngoja nikuumbue kwa kuchangia;
Kwanza namuunga mkono mtoa mada swala la kuondoa ubadhilifu kama report ya CAG inavyoonyesha,
ila tatizo hao vijana toka vyuoni kugombea udiwani! wengi wao hao vijana wana high expectation watakubali uwatoe majijini!
Swala la ubadhilifu sio la kisiasa kama wewe mtoa mada unavyotaka tuamini hilo ni swala la kukosekana kwa maadili na uzalendo katika taifa letu.

Huu ni wizi unaofanywa na CCM miaka na Miaka, kinachotokea sana ni kuwepo kwa wanaohoji huu uwizi kila Corner ya nchi..

Asanteni sana wananchi kwa mwamko wenu hawa wezi na majiizi ni kuyabana mbavu mpaka mwisho na Dawaya na Kiboko yao ni CDM hawatoki Bungeni wala kwenye Halimashauri...

Embu angalia wizi mwingi sana unafanyika sehemu ambazo haya majambazi CCM yapo yenyewe lakini sehemu amabazo kuna diwani hata mmoja wa CDM hakua huo uwizi tunausikia kwa majirani zetu ambao bado wapo usingizini..

Hawa CCM wataiba pesa mpaka basi na hawatosheki, mwisho watawaletea waizi wengine kutoka nje a.k.a Wawekezezaji ili waendelee kuiba kupitia mgongo wao Mfano ni ATCL tunaona ni nini kinaendela Nchi nzima haina Ndege hata moja? Hii ni aibu kwa nchi na aibu kwa waTZ.
 
Mkuu ninaunga hoja mkono kwa % zote

Mfano leo nimekutana na mzee m1 mkuu wa idara flani hapa Sikonge na maongezi yetu yalikuwa ni kwa nn Wilaya hii inaongoza kwa udhoofu wa kutupwa katika karibu kila idara na pesa zinaliwa zaidi ya kawaida,yule mzee alinijibu jibu moja tu na kusema kweli nilimwelewa,alisema hivi

DED na watendaji wengine wanatumia elimu ndogo ya madiwani na mbunge wao kuwapumbaza na kupitisha vi2 ambavyo mwisho wa siku ni hasara lakini wanajidefend kwa kusema vilipitishwa na madiwani kwenye vikao vyao huku wataalamu wakiendelea kunufaika na ujuha huu kwani kwenye madudu haya wao ndo wanakula

Sasa ndugu zetu tukubali kuchukua nafasi hizi na nina uhakika sehemu kama hizi endapo pana madiwani wasomi wa upinzani walau kutaweza kusaidia kuinua maisha ya watu hawa wa chini ambao ndo wengi na ndo maskin kapukwe,kwao hospitali,majosho,barabara,shule,masoko,mbegu,maji na mengine mengi ndo vitu vya msingi na ndo vya kuwainua hapa walipo,sasa kama madiwani ni mbumbumbu basi hamna ki2 kinaweza kupatikana kati ya haya na hatima yake ni umasikini.

Wanaopinga hoja hii ni haki yao kupinga lakini tuseme tu ukweli kwenye yale mambo yanaandikwa in technical terms/language yanaleta shida baina ya engineer kwenda kwa mwanasheria,daktari,mhasibu n.k kwamba kama si field yako ni vigumu kuelewa hata kama nyote ni graduates,fikiria inakuwaje hii lugha inapotumiwa pale Ikwiriri ama Kazoramimba ama Misenye kwa madiwani wa drs la 7 na fm4?je wataelewa kweli?,sasa kwanini tusiwe na professionals ili wakabaini matumizi ya kihuni ya lugha hizi huko chini?
 
Back
Top Bottom