Mbowe kuongea na waandishi wa habari

Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
21,271
47,271
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe anatarajia kuongea na waandishi wa habari leo saa tano asubuhi jijini Dar es salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya chama likiwemo tamko lake kuhusu kukamatwa kwa amri ya mahakama.
 
watahakikisha hafiki mkutanoni hao.. vitu kama hivyo wako makini kupita kiasi ila ukienda kwemye mambo ya msingi ni utumbo mtupu!

this country sucks big tyme! aaaaaargh
 
Nadhani Polisi watakuwa nje ya chumba cha mkutano wanamsubiri. Akimaliza tu kuongea, anakamatwa na kesho anakuwa headline kwenye magazeti ya ccm na serikali yake kama ilivyo leo!
 
naona ccm wameanzisha mkakati mwingine wa kuhakikisha kuwa viongozi wa serikali ijayo wanachafuliiwa kwa njia mbalimbali ili kupoteza taswira yao nzuri mbele ya jamiii. na mkakati wa sasa ni kutumia mahakama kuwachafua, na zaidi sana wanataka wasipate muda wa kushiriki shughuli za kukijenga chama. ccm watambue kuwa cdm sasa si mtu fulani, bali ni chama ndani ya mioyo ya watanazania. people's...........................!
 
Nadhani Polisi watakuwa nje ya chumba cha mkutano wanamsubiri. Akimaliza tu kuongea, anakamatwa na kesho anakuwa headline kwenye magazeti ya ccm na serikali yake kama ilivyo leo!

Hiyo kawaida,naona uhuru,jambo leo na habari leo kama kawaida,tena jambo leo kwa headline nyekundu kuonesha msisitizo
 
Tutamsikiliza kiongozi mkuu wa wa watanzania, chama kinachoongoza watanzania pasipo kumilki dola ila wanamiliki nguvu ya umma
 
Hivi hizi mahakama, polisi and other state apparatus hawaguswi kabisa na matatizo ya wananchi. Wao wako kundi gani, je kwao maisha magumu hawayaoni? I hate this government.
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema Freeman Mbowe anatarajia kuongea na waandishi wa habari leo saa tano asubuhi jijini Dar es salaam kuzungumzia masuala mbalimbali ya chama likiwemo tamko lake kuhusu kukamatwa kwa amri ya mahakama.

Wanashindwa kuwakamata mafisadi epa lichimondi kiwila kagoda nk watu wakichoka mabomu yataisha nawasiwatulize siombi tufike huko
 
mahakama ziko juu ya kila kitu aongee atakavyo kama hatafika atakamatwa , angeenda akaongee na hakimu yaishe ila suala zima ni uzembe wa mawakili wa cdm wanatakiwa kuwaelewesha wateja wao kanuni na taratibu za mahakama
 
Hivi hizi mahakama, polisi and other state apparatus hawaguswi kabisa na matatizo ya wananchi. Wao wako kundi gani, je kwao maisha magumu hawayaoni? I hate this government.

Mkuu!
Nadhani unafahamu kale ka msemo ketu ''kuwa kwenye system''.
 
Ningemsihi Kamanda Mbowe aachane na mkutano kama huu! Usibishane na Mjinga! Mahakama hawatumii Busara hata siku moja, wanatumia wanachokiita Sheria, tena kwa ujeuri wanadai SHERIA NI MSUMENO! Watamdhoofisha, wanaweza pia kumweka ndani na kumkolimba akiwa huko - kuna madhara mengi. Angetafuta njia nzuri ya kukabiliana na tatizo la kudaiwa kutotii mahakama, pengine kwa kujisalimisha kule mahakamni na vielelezo kadhaa, pamoja bila shaka kuegemea Nguvu ya Uma!

Mahakama hawajali gharama hata mara moja, hawajali shughuli za mtu yeyote, wanakuita unafika wanasema haya njoo tena siku zingine! Give me a gun and will surely set it on no other creature!
 
Tuziache taratibu za kisheria zichukue mkondo wake, kwani dharau yoyote dhidi ya sheria au mahakama ni kosa lisiloweza kuvumiliwa.
 
ile si kesi, ni mambo ya kisiasa na yeye lazima aichukulie kisiasa. hata wakimkamata kwani nani asiyejua ni kesi isiyo na miguu wala kichwa?, subirini aseme anachotaka kusema na hao wenye nchi yao wakitaka kumkamata watamkamata tu shinda ipo wapi? watanzania huu uwoga wenu kwenu mnaweza kufa kwa ajiri ya nchi yenu?

Mapinduzi ya kweli yana gharama zake, hakuna mtu alishapewa haki ya ki demokrasia akiwa amekaa kivulini nduguzangu - NEVER.
 
kama yeye anajidai kukemea wasiofuata utawala wa sheria iweje yeye alete dharau za kiajabu utadhNI HAJASOMA, HATA KAMA ALIFAIL ASOME VIFUNGU VYA SHERIA ZINAPATIKANA, ASIJIDANGANYE KUWA TUTAANDAMANA KWA UJINGA WAKE
 
Mwenyekiti anakua mjinga kiasi hiki ana bishana na mahakama? Shame on u CDM....

mimi nafikiri wewe ndiyo unamatatizo ya kufikiria - kwanza hujajua anakwenda kuongea nini na kwa nini then unakuja na upupu wako hapa.

Subiri aongee amalize then njoo na comments zako za kudhihirisha kuwa yeye ni mjinga au wewe ndiyo juha.
 
Back
Top Bottom