Mbowe kulifumua baraza la mawaziri kivuli; nani kuingia/kutoka?

Lilombe

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
242
39
Jana akiwa Arusha NMC, Mheshimiwa Mbowe alitoa kauli ifuatayo:-
"nakwenda kulifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri vivuli ili kuliandaa vizuri na kuwasilisha bajeti mbadala kwenye Bunge lijalo linalotarajiwa kukutana mwezi Juni".

Je ni nani ataendelea an nani atatishwa ili aendane na kasi ya mabadiliko ya JK?
 
Hivi ana mamlaka hayo au ni chama.Manake rais kikatiba anaweza bila kukishirikisha chama chake.Ila kwa mbowe sidhani.
 
Nimejaribu kusoma post zote za mkutano wa jana na bahati nzuri nilikuwepo. Sikuona aliyeleta hii habari nikashangaa maana ina umuhimu wake. Ni kweli alisema na ninaomba tujadili kwa mtazamo wa nani anafaa wizara gani na kwanini ili tupate baraza kivuli lililo bora. Nawasilisha.
 
Baraza lake jipyaa lijumuishe na wengine wa upinza aache ubinafsi.tuliona dr slaa alivyofanya kaz na hamad rashid mambo yalivyokua
 
Juzi nimeleta thread ya Chadema kufanya mabadiliko kwenye baraza la Mawaziri nimeshambuliwa sana nashukuru Mbowe kalifanyia kazi.
 
Baraza lake jipyaa lijumuishe na wengine wa upinza aache ubinafsi.tuliona dr slaa alivyofanya kaz na hamad rashid mambo yalivyokua

Mkuu labda ungetuambia nani anafaa wapi na kwanini. Hapo bado umeiacha hewani sana!
 
Feedback Mungi Mbowe kulifumua baraza la mawaziri kivuli.

Najua unataka kutuambia Mbowe naye atateua wabunge kivuli.
CHADEMA iko imara kuliko kipindi kingine chochote!
Mbowe atakachokifanya kwenye Baraza lake kivuli ni kuhakikisha kila waziri anaiwajibisha serikali kwa hoja, hasa katika kipindi hiki ambacho Mk.were amefanya mabadiliko ya kuwahadaa watanzania. Siku mbili kabla Jk hajabadilisha baraza lake ikulu ilitoa taarifa kwa umma kuwa baraza atakaloliteua litakuwa bora itakayokata kiu ya watanzania.
Wote tumeshuhudia alichokifanya Jk ni kuwabadilisha wezi wale wale wizara zingine.
Nyalandu, Mkuchika, Maghembe wote wezi wakubwa lakini cha ajabu Jk ameendelea kuwalinda!
 
STIDE.
TIMING.
KOMBAJR.
pendaela laizer.
FJM.
Manyanza.
Rev.Mzito K.

Chadema kulifumua Baraza la Mawaziri Kivuli baada ya kushindwa kazi.

Ritz acha kunywa Bangi bana. We sema ni waziri gani kivuli wa chadema aliyeshindwa?
Nakuhakikishia kuwa Mbowe atakachokifanya ni kuziba nafasi mbili ambazo zipo wazi za Regia Mtema (R.I.P.) na ya Kamanda Lema.
Mawaziri wengine watabaki na wizara zao. Labda anaweza kuwahamisha kutoka wizara moja kwenda wizara nyingine kulingana na changamoto za baraza jipya la Jk.
Mfano wizara ya Uchukuzi amepewa Mwakyembe, Nishati Prof. Muhongo sasa hawa wanatakiwa wakabiliane na mawaziri kivuli makini wa chadema.
 
Back
Top Bottom