Mbowe kuhusu baraza la mawaziri

VoiceOfReason

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,194
1,355
Baraza ni kubwa sana kulingana na nchi yetu masikini

source BBC Swahili

My take
Thats what every honest taxpayer thinks
 
Sio kubwa tu ila limejaa watu wasio na lengo la kumkomboa mlalahoi hivi nani anategemea kitu kipya kwa ngeleja, magembe, lukuvi, kawambwa, sophia simba, kabaka,nchimbi,chami,hawa ghasia,husein mwinyi,nahodha,maige, mkullllllllo hawa ni bure tantalile labda juhudi binafsi, mark mwandoshya, magufuli, hawa wapya ngoja tuone but kwa mafisadi kuanzia juuuu tegemea maumivu zero zero
 
Mbona wananchi walio wengi wanalipongeza? Tuna safari ndefu kweli kweli
 
achangia nini na huku haitambui serekali ? au ndio anatambua kimtindo ?
 
Mbona wananchi walio wengi wanalipongeza? Tuna safari ndefu kweli kweli

Mbona kuna wananchi pia walimpongeza Mwenyekiti wa NEC kwa kumtangaza JK mshindi...so siwashangai wananchi wa tanzania
 
Sio kubwa tu ila limejaa watu wasio na lengo la kumkomboa mlalahoi hivi nani anategemea kitu kipya kwa ngeleja, magembe, lukuvi, kawambwa, sophia simba, kabaka,nchimbi,chami,hawa ghasia,husein mwinyi,nahodha,maige, mkullllllllo hawa ni bure tantalile labda juhudi binafsi, mark mwandoshya, magufuli, hawa wapya ngoja tuone but kwa mafisadi kuanzia juuuu tegemea maumivu zero zero
Denyo

Naomba ufafanuzi kwanini unadhani Mwandosya ni waziri mzuri na niambie hizo juhudi binafsi unazosema hapo kwenye post tafadhali
 
Uelewa wa watu wetu ni Tatizo na kikwazo kikubwa cha Maendeleo, Nidhamu ya Uoga na Lundo la ma-opportunist ni tatizo lingine linalozaa pongeza za kinafiki bila kuangalia gharama halisi ma madeni yanayotukabili watanzania.
Safari Bado ni ndefu sana ya maendeleo na Demokrasia ya Kweli
 
Kocha Kikwete amesajili wachezaji wengi na fikiri wengine watakuwa hawana kazi. Kodi zinatafunwa Watanzania ni mijimbumbu kazi kung'ang'ania AMANI. Haya kaeni na amni wenzio wala kodi . Sitegemei chochocte kutoka kwa mkuu Kikwete kwenye timu yake ya ufisadi.
 
Mbona wananchi walio wengi wanalipongeza? Tuna safari ndefu kweli kweli
Am sure hakuna mwananchi anayepongeza ukubwa wa baraza; bali watu wanapongeza baadhi ya uteuzi mfano magufuli, tibaijuka na kutokuwepo kwa kina lowassa ambao watu walizani watakuwepo. Ila idadi ya mawaziri sidhani kama kuna mtu anapongeza.
 
achangia nini na huku haitambui serekali ? au ndio anatambua kimtindo ?

Yeye ameulizwa kuhusu baraza la mawaziri anaonaje.... What could he have said kwamba baraza halipo? Diplomatically akajibu kuwa ni kubwa na anadhani itakuwa business as usual
 
Am sure hakuna mwananchi anayepongeza ukubwa wa baraza; bali watu wanapongeza baadhi ya uteuzi mfano magufuli, tibaijuka na kutokuwepo kwa kina lowassa ambao watu walizani watakuwepo. Ila idadi ya mawaziri sidhani kama kuna mtu anapongeza.

Mkuu soma magazeti ya leo, kisha subiri ya kesho
 
Nauliza hivi, safari hii mawaziri watapelekwa semina Ngurdoto kama 2005?

Nothing Surprises me anymore in this country. Tunavyofuja pesa utadhani we are the richest country in the world. Am sure hata tukipewa China, baada ya miaka miwili tutakuwa tumeifilisi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom