Mbowe kugombea ubunge Hai 2010 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe kugombea ubunge Hai 2010

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkulima, Oct 26, 2009.

 1. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Je Dr. Slaa kugombea urais TZ mwakani?

  Kuna kila dalili kwamba CHADEMA wanamuandaa Dr. Slaa kugombea urais 2010. Mpambano huo utakuwa mzuri sana, huenda tukamkosa sana Dr. Slaa kwenye bunge la kuanzia 2010.

  Jana CHADEMA walipokuwa Karatu waligusia kitu kama hicho kwamba wanatafuta mtu mwingine kugombea ubunge Karatu. Na sasa Mbowe kaamua kurudi Hai, basi mpambano mwakani nadhani utakuwa JK vs Dr. Slaa.

  Naye Mbowe si angesema tu kwamba ameamua kugombea? Hii ya kwamba wananchi wamemuomba na propaganda tu za kisiasa.

  Mbowe kugombea ubunge Hai 2010

  na Grace Macha, Hai

  WANANCHI wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, wamemuomba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kugombea ubunge kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka 2010; naye amekubali.

  Kutokana na Mbowe kukubali ombi hilo, ni wazi sasa atapambana na mbunge wa jimbo hilo hivi sasa, Fuya Kimbita (CCM), katika uchaguzi mkuu ujao.

  Alisema amefikia hatua hiyo, baada ya kuombwa na wananchi wake ambao walisema wamekosa mwakilishi makini tangu alipoachia ubunge kwenye jimbo hilo mwaka 2005.

  Wananchi hao ambao walikuwa wakipaza sauti wakati wote, hali iliyosababisha Mbowe akatishe hotuba zake mara kwa mara kwa ajili ya kuwasikiliza, walisema wakati akiwa mbunge alianzisha miradi mingi ikiwemo ya elimu , kijamii na kiuchumi ambayo kwa sasa imekufa.

  Hata hivyo, Mbowe aliwasisitizia wananchi hao kuwa lazima wampe watu wa kufanya naye kazi ambao ni wenye viti wa vitongoji na vijiji kwani kinyume cha hapo atafanya kazi katika mazingira magumu.

  Alisema katika kipindi cha miaka mitano alichowaongoza kuanzia 2000-2005, jambo kubwa lililokuwa likimsumbua ni vikwazo alivyokuwa anawekewa na viongozi wa vitongoji na vijiji ambao kwa wakati huo walikuwa wanatoka Chama Cha Mmapinduzi (CCM), ambao alikuwa akipanga nao shughuli lakini walikuwa wagumu kutekeleza.

  Mbowe ambaye kabla ya kuwanadi wagombea wa Chadema, aliwauliza wananchi hao iwapo wagombea wake walikuwa na sifa na wananchi walisisitiza kuwa wote walikuwa wanafaa. Kwa upande wake, Mbowe aliwataka wananchi hao kuwapuuza wanaodai kuwa mahindi ya chakula cha msaada yanayotolewa ni mali ya CCM. Mbowe alifanya mikutano kwenye vijiji vya Kilanya , Narumu , Machame - Uroki , Kyuu - Masama Magharibi na Mbweera Mula - Masama Mashariki eneo analotokea mbunge wa jimbo hilo Fuya Kimbita (CCM).
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkulima,
  Kwani ulimwomba wewe?..tulio mwomba tumekaa kimya iweje wewe uwe msemaji mkuu wa kujua kila kinachofanyika Chadema!.. si ndio unafiki huu mkuu wangu.
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Hawa Chadema nao wanapupa...walianza vizuri hawakuwa na haraka wala pupa ya mambo...kama watampeleka Slaa kwa wananchi ambao wanamjuwa Slaa lakini chama chake bado si maarufu katika maeneo ya wapiga kura wengi,Dr.Slaa anahitajika bungeni wakati utafika wananchi wenyewe...watamuhitaji awe kiongozi wao wa nchi...kama walivyofanya wanachi wa Karatu wakati ule alipopokwa tiketi yake na wananchi wakamtaka agombee kupitia chadema...si walimpa, chadema wasifanye papara...we need the guy in parliament.
   
 4. M

  Mkulima JF-Expert Member

  #4
  Oct 26, 2009
  Joined: Feb 4, 2007
  Messages: 698
  Likes Received: 113
  Trophy Points: 60
  Mkandara,

  Mimi siamini hizi blah! blah! za kwamba wananchi wameniomba nigombee. Kugombea ubunge ni jambo kubwa na mtu anaamua mwenyewe kwanza na wananchi wanamuunga mkono.

  Lakini kwa TZ kila mtu anajifanya kaombwa kugombea. Hawa wanasiasa wetu hata tuwaombe namna gani, huwa hawafanyi, isipokuwa kwa mambo ambayo wameamua wenyewe.

  wameombwa mara ngapi ili waungane? Hawataungana wakati wanaona ulaji mbele.
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Oct 26, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Junius,
  Mkuu hapa ume raise kitu kingine ambacho kusema kweli mimi sielewi nini malengo ya mfumo wetu..Wakuu zangu naomba somo ktk hili.
  Kwa mfano hapa Canada mgombea yeyote wa chama ktk ngazi ya Waziri mkuu ni lazima agombee pia ubunge sehemu yake na kama sikosei wote waliogombea Uwaziri mkuu hapa wapo bungeni inakuwaje sisi mtu akigombea Urais akishindwa ndio imetoka!. Nikitazama Marekani McCain bado yupo ktk senate, mama clinton pia angeendelea kuwa wa New York kama asingechukua kazi ktk serikali ya Obama... lakini sii Bongo, Hivi nini kazi ya Mbowe, Lipumba, Mrema na viongozi wengine baada ya kushindwa uchaguzi uliopita.
   
 6. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #6
  Oct 26, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Kaka na wewe ni Chadema? una agenda mama ya Chadema?
   
 7. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #7
  Oct 26, 2009
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  we dont care umemwooomba wewe au wengine what I know we need the man mbona unaleta mambo ya kizamani hapa, Tunamhitaji Slaaa only that we dont care nani kamuomba.
   
 8. Mchaga

  Mchaga JF-Expert Member

  #8
  Oct 26, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,371
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  wakati gani tena mkuu? wakati ndio sasa...
   
 9. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #9
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Wawaache viongozi wao wagombee ubunge kwani angalau huko wanaleta challenge lakini suwala la Urais bado 2010 Kikwete atapeta. Ni kupoteza fedha na wakati kwa mbowe kugombea Urais kwani hata Lipumba atapata kura nyingi kuliko Mbowe!
   
 10. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #10
  Oct 26, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa Tanzania hilo litakuwa ndio chanzo kikubwa cha mtafaruku kwani kuna utitiri wa vyama na wagombea wengine wa Urais wa vyama hivyo we acha tu!
   
 11. K

  Kwayu JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2009
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 487
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi kama mwananchi wa hai ni kweli kabisa wananchi wa hai wana hamu kubwa sana mbowe arudi bungeni kwa kuwa mbunge wa sasa fuya kimbita hakubaliki kabisa. Na dalili zinaonesha kuwa chadema watashinda kwa kishindo kwa sababu ngome kubwa ya ccm katika kitongoji cha nnyama ambako mwenyekiti wa ccm wilaya ya hai ndugu amin athman uronu iemevunjwa kwa chadema kuibuka kidedea kwa kura nyingi sana.
   
 12. W

  WildCard JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2009
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Kama ni kwa suala la kuboresha RUZUKU kwa ajili ya maandalizi mazuri ya 2015 ni sawa kumteua Dr Slaa kwa ajili ya 2010. Hii pia itampa uzoefu wa kutosha kwa ajili ya mpambano wa KWELI 2015 ambako CCM watakuwa na wakati mgumu sana kuteuana kwa jinsi walivyojichafua na kuchafuana.
   
 13. h

  hsagachuma Member

  #13
  Oct 27, 2009
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 22
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kweli sasa anataka kuvaa viatu vyake. Ubunge ndiyo saizi yake. Uraisi hata ajaribu mara mia hatapata. Itaishia kuchoka kama Mrema Lyatonga mwana wa kiraracha.
   
 14. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2009
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Mbowe ni mtu makini kama ilivyo CHADEMA yenyewe,Nina uhakika kabisa kuwa akiingia ulingoni na huyo Kilaza wa CCM atampiga mwereka kamili.Bwana Mdogo Fuya Kimbita alipewa kwa kuwa kulikuwa hakuna mtu wa kupingana naye.Nawahakikishia kuwa Mbowe yuko imara tena ana kila sababu ya kuchukua kiti cha Wilaya ya Hai.
  Sina shaka na Dr.Slaa japo wizi wa kura hautampa nafasi lakini CCM itapata joto ya jiwe,Kwani Kinara wake ameonyesha uchovu wa hali ya juu kabisa kumalizia ngwe iliyosalia.Najua kuwa atapata kuendelea lakini kwa pata shika ya hali ya juu mno,Hata ikilazimu nchi kugawanyika na iwe hivyo kutokana na kundi kubwa la wananchi kuishia kuchagua tu alimradi wamepewa kanga,plau na kofia!!!!
   
 15. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2009
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Dr Slaa baki bungeni, michango yako inahitajika sana. Kugombea urais wa Jamhuri kwa wakati huu ni sawa na mbio za mita 100 ushindanishwe na Usain Bolt. Utapoteza nafasi ya kuwakilisha wananchi wa jimbo lako Bungeni.
   
 16. M

  Mvutakamba Member

  #16
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nawapa hongeara Chadema maana watu walisema Chadema hawasikiii na kwa mara nyingine Chadema wanaweka rekodi ambayo iliwekwa na wenzao wa NCCR kwamba si lazima Mwenyekiti wa Chama agombee Urais . Ushauri wangu pia kwamba Slaa gombea mwaka 2015 na si sasa . Weka uwanja sawa kwanza watu waumie mwaka 2015 tia timu msee wangu .
   
 17. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2009
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hawa waache ujinga kwanini wagombee urais ambao hawawezi kushinda!!?
   
 18. H

  HM Hafif JF-Expert Member

  #18
  Oct 27, 2009
  Joined: Aug 16, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Yaani Slaa tena awe raisi. Si Itakuwa balaa. UKATOLIKI MTUPU HAPO na nchi itakuwa ya Kikatoliki kama ilivyokuwa wakati wa JKN. kwani yeye alikuwa katibu wa TEC.

  Watanzania tumwangalie sana Slaa huyu.
   
 19. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Dah,noma kweli yaani,ina maana Mkatoliki si Mtanzania?????,kwamba nchi isiongozwe na Mkatoliki!!!,duh.Hii hali imekuwa mbaya kwa kweli,yaani tumefika huku!!!!.Tanzania ni secular state mkuu so mtu wa Dini yoyote ana uhuru wa kushiriki uchaguzi(kwa kugombea) na kuongoza nchi..Haya mambo ya Udini yanatupeleka kubaya kwa kweli.Tubadilike jamani(hasa humu ndani ya JF maana haya mambo ya Udini yanakera sasa)
   
 20. l

  lukule2009 Senior Member

  #20
  Oct 27, 2009
  Joined: Sep 23, 2009
  Messages: 132
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0

  No we need him to be President ... His excellence President Dr Slaa. yes it is possible. He has done a good job he deserve promotion
   
Loading...