Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe anatarajiwa kuanza ziara rasmi ya kichama katika mkoa wa Mwanza kuanzia tarehe 14 Desemba.
Taarifa kutoka Makao Makuu ya Chama Dar es Salaam na ofisi za chama Mkoani Mwanza zinasema kwamba ziara hiyo itakuwa na nia ya kuimarisha chama.
Kiongozi huyo anatarajiwa kuhutubia wanafunzi wa vyuo vikuu mkoani Mwanza ambao ni wanachama wa CHADEMA katika siku ya kwanza ya ziara yake.
Mkoa wa Mwanza ni kati ya ngome kuu za CHADEMA kanda ya ziwa na Mwenyekiti huyo amekuwa akiheshimika sana katika mkoa huo.
Source:Chademablog.