Mbowe: Kamati ya Amani ilikaa kimya wakati watu wetu wanauawa na kuteswa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
49,191
103,715
Mh.Mbowe anaongea.....

Viongozi wa kiroho wanakataza watu wasilitumie neno MWENDAZAKE. Mimi ninapenda kuwaambia viongozi wangu ukifanyacho hapa duniani ndicho utakachovuna. Viongozi wetu hawa walikaa kimya watu wetu walipouawa, potezwa nk. Walikaa na kunywa mezani pa watesi weyu......

My Take
Anachomaanisha Mbowe ni kwamba ile kamati ni ya kinafiki.
 
Mbowe lipa kwanza mishahara, hata wewe ulikaa kimya huku ukijua Sabaya ana karakana ya kutesa watu.
20210527_213348.jpg
 
Napinga sana huu uana harakati anaofanya Mbowe.

Ukweli iwapo kila tendo tutataka kulijadili kiundani kama anavyotaka,hali inaweza kubadilika sana kwa kuamsha hisia kali za wanaoonekana kama wameonewa.Na bahati mbaya kisasi huwa kinafanywa kwa watu wasio husika kabisa.

Ninadhani Mbowe anataka kwenda mbali sana.Sijui anataka nini.Mashehe wameachiwa,kwa nini hilo pekee lisitoshe kumshukuru Mungu?

Kusema kweli natamani adhibitiwe,kwani hizi siasa zina lengo la uchochezi.
 
Mwendazake kwa hakika amekwisha enda zake, kwa kuwa hayupo tena nasi katika hali ya kimwili ambapo aliweza kuiongoza nchi hii. Ametuacha, ametutoka, ametangulia mbele za haki ama ameenda zake, hilo ni tukio la uhakika ambalo kwalo litamtokea kila mwanadamu aliyezaliwa na mwanamke hapa duniani.

Kuonja mauti ni jambo la hakika kwa mwanadamu awaye yeyote yule, wala sioni shida ama sababu yenye mantiki kwa viongozi wa kidini kuona ukakasi juu ya yule aliyekufa kuitwa mwendazake, kwani kwa sasa hayupo tena nasi katika ulimwengu huu wa kimwili. Neno hili limebamba mno kwa kuwa mwendazake alikufa akiwa kiongozi wa nchi yetu, na katika uongozi wake watu wengi waliathirika kwa aina ya utawala wake, kwa maana ya muelekeo athari hasi ama chanya, ingawaje wale wa upande wa athari hasi ndiyo hupenda hasa kutumia nomino hii ya utambulisho wake kwa sasa.
 
Mh.Mbowe anaongea.....

Viongozi wa kiroho wanakataza watu wasilitumie neno MWENDAZAKE. Mimi ninapenda kuwaambia viongozi wangu ukifanyacho hapa duniani ndicho utakachovuna. Viongozi wetu hawa walikaa kimya watu wetu walipouawa, potezwa nk. Walikaa na kunywa mezani pa watesi weyu...
Viongozi wa kiroho muwe kweli Manabii (wa kweli), Wafalme (wa kweli) na Makuhani wa kweli wakati wote na kwa kondoo wote wa BABA hata nyakati ngumu. Msielemee upande moja. HAKI ndicho kitu cha kwanza, AMANI itafuata palipo na haki. Mungu Baba ndiye aliyetuleta Tannzania (Tanganyika) sisi wote.

Hakuna binadamu mwenye jukumu hilo. Sisi sote tuna haki sawa ndani ya nchi hii. Hivi mnadhani vurugu ndani ya nchi zinaletwa na wananchi? La hasha, bali viongozi waliosahau kutekeleza wajibu wao, wakaanza kutekeleza matakwa ya Ibilisi Lusifa na vibaraka wake.

Kiongozi bila haya unafurahia aibu wanayotenda kina Sabaya kwa Watanzania wenye mtizamo tofauti nawe. Viongozi wa kiroho mmekaa kimya. Leo hii neno "Mwendazake" limewatoa karamuni mnakokula vinono na watesi tena kwa gharama zetu.

Mungu daima atabaki YULE Mwenye uwezo ulio MKUU unaodhibitiwa na Destruri yake iliyo bora (UPENDO, HURUMA, UPOLE, UVUMILIVU, UKARIMU hata kwa hao watesi wetu, WEMA, MKWELI, DAIMA MWAMINIFU). Mara zote tusimame kwenye kweli na haki, unafiki tuachane nao. Amin
 
Back
Top Bottom