Mbowe kahusishwa na MKIRU, IGP Sirro ameamua kurudisha jeshi huko

Sirro hana uwezo wa kumshinda Mungu , ni mtu mdogo sana ambaye siku zake kwenye utumishi wa umma zinahesabika , Mbowe alimshinda Magufuli ndio aje kuwa huyu aliyepewa U IGP na Makonda ?
Mbowe alimshindaje Magufuli mkuu?

Wewe ni miongoni mwa watu wanaofanya CDM ionekana ni upuuzi kwa mambo unayoandika humu.
 
Mama amekubali kuingizwa kwenye siasa za kitoto, ndio maana anatumia fedha za umma kwenda kupambana na kesi ya kubambikizia, huku mambo ya msingi yakimshinda. Anashindwa kumkamata aliyekuwa anaitia serikali hasara kwa kijiunganishia bomba la mafuta, halafu anatumia hovyo pesa za serikali kwa kuendekeza siasa za kitoto, kisha unashanglia huo utoto kama zwazwa. Hapo wazungu wataacha kutuita manyani kweli?
Kweli kabisa.
Katiba mpya ilianzishwa na serikali ya CCM kwa kodi za wananchi. Tume ya Katiba ilikua na makada wa CCM walioaminiwa na wananchi na serikali ya CCM na wakashangiliwa kila walipokwenda na kupewa ushirikiano wa kutosha.

Katiba mpya haikuanzishwa na Magaidi bali ilianzishwa na Serikali halali kama ilivyo serikali ya Samia iliyojaza vijana Waroho wa Mali na madaraka Leo. Serikali ya Samia isipokubali Demokrasia italiangamiza Taifa hili mana amezidiwa na Mtangulizi wake kwa hayo anayotaka kumwiga kwa kuwa mwenda zake alikua na Elimu kubwa na alikaa madarakani akiwa Waziri aliyezunguka nchi nzima akisimamia Barabara ,mifugo na uvuvi kwa miaka 20 . Mwenda zake alikua na sifa za usimamizi na akiwajua watu mpaka wa mitaani kwa majina na alikua hasahau MTU kamwe. Alikua na uwezo mkubwa wa kukariri na kushika jambo kichwani na takwimu zake. Hata hivyo alishindwa kuunganisha Taifa kwa vitendo na kuweka Mbele siasa za vyama na makabila huku akipuuza mgawanyiko wa watu na watu kuumizwa.

Enzi za Mwendazake Gwajima na Polepole na Ndugai na Mwigulu wasingethubutu kutoa matamko yanayopingana na kauli zake akawavumilia hata sekunde moja.
Leo Mama Samia anakubali kuchezewa na Chama chake kinachokula bata na kuku katika nchi hii halafu anawaonea watu walioonewa kwa miaka yote ya mfumo wa vyama vingi.

Mwenda zake alijiamini kwa sababu kwanza alijitanabaisha kama mmoja wa watu wanaotoka katika kabila kubwa kabisa kwenye ukanda mkubwa wenye wasomi wangi , wachawi wengi,washirikina wengi, wafitini wengi, watananshati, walaghai, mitume feki na halisi, watu katili wengi, wabinafsi, waroho wa madaraka,wenye kupenda sifa na zaidi wengi wanafiki wasiosema ukweli unaoweza kuwaumiza kimaslahi.
Lakini zaidi Mwenda zake alijiweka chini ya mwavuli wa Rumi.
Kwa Mwenda zake ilikua ni jambo rahisi sana kutumia mabavu na watu wakakubali kishingo upande.

Kwa sasa Mama ni busara tu akaendesha nchi kwa Haki na Demokrsia vinginevyo anaweza akasababisha watu wakavuruga umoja wetu zaidi na watu wakamtupia lawama kuwa ameshidwa kuongoza nchi na kulinda amani ya nchi. Na inavyoonekana ndio hasa lengo la Genge la awamu iliyopita.


Katiba mpya ni Mwongozo mpya wa namna ya kuliongoza Taifa letu kwa Haki bila kujali vyama ,dini,kabila na urafiki. Haiwezi kuwa ni hisani ya mtu Bali ni Hitaji la watu kama ilivyo umeme na maji. Watu wana kiu ya Haki katika Taifa hili. Kiukweli kabisa Hakuna Haki kwa watu wa chini na wapinzani wa serikali iliyojibinafsia nchi hii na familia zao kama Mali ya CCM.
Katiba bora ni msingi wa sheria nyingine zote kuwa bora na msingi wa Jamii bora ya watu waliostarabika.

Waziri wa Mambo ya ndani alikua analalamika kuwa Jeshi la Polisi wanabambikia watu kesi. Akasema jeshi hilo inabidi liongeze mud Wa kutoa mafunzo mpkaa kufikia Mwaka mzima ili waive sana ili wasibambikie watu kesi .
Hata SimbaChawene aliona tatizo la watu kubambikiwa kesi.
Kwa hiyo Mama kukubaliana na Polisi kuwa Mbowe ni Gaidi ni kuendeleza roho mbaya ya kubambika watu kesi jambo litakalozidisha chuki kubwa kwa wananchi kwani wanona kuwa waliostahili hata kunyongwa wapo mitaani na watu wema wapo Gerezani.

Hata Manabii waliwaasa Polisi kutenda haki na kuepukana na Rushwa na kushitaki watu kwa uongo.(Kubambika watu kesi za ugaidin)

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Wakuu,

Tunaweza kuwa tunalaumu sana mashitaka aliyofunguliwa mwenyekiti wa CHADEMA bila kuwa na uelewa kwamba anajihusisha na mambo hayo au hajihusishi.

Kufuatia press meeting aliyoifanya IGP Sirro akiwataka wanachadema kutokuonekana Mahakamani kupinga tuhuma zinazomkabili mwenyekiti na kueleza umma kuwa Mbowe amehusika.

Kitendo cha Sirro kuzungumzia mambo yaliyotokea huko Mkuranga na Rufiji katika press ile ni wazi kwamba alijaribu kutaka kusema kwamba Mbowe amehusishwa na mambo yale ya Mkiru.

Kwanini atumie press ile kutoa taarifa ya Mbowe na ugaidi uliofanyika miaka michache huko Mkuranga na Rufiji.. pia kuriamuru jeshi la polisi kuongeza nguvu huko.

Hapa naona moja kwa moja Mbowe akihusishwa na Mkiru.
Hana lolote, mtupu kichwani kama Wewe tu!
 
Ndugu,
Waliomhusisha ni walewale mapolisi mabingwa wa kubambikiza kesi. Fuatilia pia matokeo ya rufaa yao itajibu zaidi maswali yako.
Hata Waziri wao Mh. Simbachawene alibainisha bila shaka kuwa Polisi wanabambikia watu kesi ndio maana alitoa tamko la kuongeza muda wa mafunzo mpaka kufikia mwaka mzima ili waive na waondokane na mazoea ya kubambikia watu kesi.


Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Mbowe alimshindaje Magufuli mkuu?

Wewe ni miongoni mwa watu wanaofanya CDM ionekana ni upuuzi kwa mambo unayoandika humu.

Hizi siasa za Chuki kwenye Wakati mgumu wa watu kufa kwa magonjwa kila kukicha bado tu mnaziendekeza.?
Kwa kweli CCM ni walevi wa madaraka.
Huu ulikua ni wakati wa watawala kuonyesha njia ya upendo na kuweka pembeni mambo ya vyama. Nashangaa CCM hawajui kuwa Dunia inapita kwenye uvuli wa mauti. Watasingizia mabeberu lakini Madhambi yamezidi duniani na watu wamekua wabaya kwa binadamu kuliko wanyama .
Sio madaraka wala Mali zitakazoiokoa dunia bali utu na upendo utawaokoa watu na kuwapa matumaini ya kufikia paradiso.

Sent from my TECNO L8 Lite using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom