Uchaguzi 2020 Mbowe itampa wakati mgumu sana kumnadi Lissu

Kumbe shida yako ni Mbowe kutomsifia Lissu kwenye mkutano huko Arusha, sasa kuna haja gani ya kumpigia debe Lissu wakati kila mtanzania anamjua na anayajua majaribu aliyopitia?

Mjomba kizuri chajiuza, kibaya chajitembeza.
 
Alipigwa yale marisasi kwa amri ya Mwenyekiti, mchana kweupe na kwenye makazi ya viongozi huku walinzi wa maeneo hayo wakiwa wameondolewa kupisha "baraka" za jiwe zitimizwe.

mpaka apo hauna ushahidi wowote unaongea ujinga tu, mm naweza nkasema pia ni chadema walifanya ivo na walitumia mbinu izo izo, unajua mnaonekana kama vichaa flan ilo kundi lenu la saccos
 
Wewe ndo kilaza ambaye hujaelewa hoja ya Lissu na hutaielewa. Lissu kasema Mwl Nyerere alijenga mabwawa yote tunayotumia sasa ila hakuna mahala Nyerere alinyanyasa watu at the expense ya miradi aliyoifanya. Sasa wewe sema humu wapi Nyerere alinyanyasa watu at the expense ya miradi aliyofanya????

Huyu anajenga bwawa moja tu ila anapiga watu risasi na kubambika watu makesi wanaomkosoa!!! Sasa ana uhalali gani wa kufanya ivo???!

Hujaelewa hoja ya Tundu Lissu juu ya corona!!! Kwanza nikuulize je watu hawakuwa wakizikwa usiku???? Kama sio kwa nini Gambo akiwa RC Arusha alizipiga marufuku mamlaka kuzika watu usiku????

Hoja ya Lissu kwenye Corona ni kuwa Raisi alionesha kutokujali afya za watu na maisha ya watu!!! Hapa Hata mie nakubaliana nae. Katika hili kama unamtetea magufuli nioneshe wapi alitoa pole kwa familia zilizopoteza watu wao kwenye janga la corona!!! Nipe uthibitisho hapa!!
Tatizo mnajitoa ufahamu kwenye janga la Korona, na huko kunyanyasa watu sijui unaongolea nini. Mshaurini ndugu yenu aache kutoa hizo boko kwenye korona
 
Ulitaka mwenyekiti aseme nini?? Kwani kampeni ishaanza???
Sasa wewe huoni ndugu yako alikwishaanza kampeni hata kabla ya muda wake kuanza? Si anajifanya much know, sasa ngoja uone atakavyokatwa, na angalieni msije mkasusa uchaguzi. We unaona vyama vingine vinafanya kampeni kabla ya muda wake?
 
Ndo maana utabaki hivo hivo. Kwenye research huwa kunakipengele cha kufanya literature review, unakijua? Basi kifanyie kazi
Mnateremeka nini nyie...kama ww unajua kufanya Literature review si ufanye kuhusu upimbi wa Chama chenu
 
..nadhani mnaziogopa hizi hoja na ndiyo maana mnatumia nguvu nyingi kuzi-crush.
Nikupe angalizo tu kuwa ubadilishe katiba usibadilishe kama utakuwa na viongozi kama akina Tundulisu, nikuiachia nchi kuwa mikononi ya mabeberu. Unayakumbuka Makinikia alivyokuwa anafanya?
 
Mnateremeka nini nyie...kama ww unajua kufanya Literature review si ufanye kuhusu upimbi wa Chama chenu
Lazima tuwe tunawapa angalizo, ili msiwe mnabugia kila kitu kutoka kwa viongozi wenu
 
Tatizo lako unatumia asilimia kidogo tu ya akili yako! Kama CHADEMA wanatengenezaga matukio, kama Chacha Wangwe, Lisu, kuchoma office zao wenyewe, nk. Kama Wewe na wenzako mnavyo tuaminisha, Kwanini serikali ikaye kimya? Kama waliweza kuwapa kesi ya Aquilina, ambayo muuaji anafahamika, wameshindwaje kutumia hayo matukio kukabiliana nao kwa urahisi tu?!
Unapotaka kusema uongo, peleka kwa chekechea wenzako huko Facebook, Hapa ni home of great thinkers!
Sasa mwangalie huyu?
 
Mnachokitaka nyie msifikiri ndio kizuri sana WALA wale wanachokitaka usifikiri ndio kibaya sana acha kila mtu afurahie kile anachokitaka hata kama sio kile usichokitaka na dunia yenyewe ndio iko hivyo.
 
Na wewe hapa unaona umecjambuaaaaa! CCM hawana watu wa kuwafanyia propaganda kulingana na kizazi hiki. Wana wapigaji tu wanaopewa Hela kuja kutalii kwenye mitandao.

Lowassa si TL. Lowassa alikuwa mwana CCM aliyejeruhiwa. Hakuna na DNA ya mabadiliko. Hakuna na makovu ya mateso toka CCM na magenge yake ya uhalifu. Hakuwa na hasira ya kweli ya kuonewa. Mbowe alimkatibisha kama mwananchama mwingine tu katika mazingira ya mpito. Hakuwa na sababu ya kumzuwia.

Mbowe bado anaaminika sana. Wengi wanajua alimwamini Lowassa toka CCM kama ambavyo Magufuli amewaamini mamia ya Wana Chadema wanaohamia CCM.

Kumnadi TL? Kwani TL anahitaji kunadiwa na mtu? Ni Wana CCM tubwwnaojifanya hamnazo. Wauaji wa CCM na Magufuli ndiyo wamemtangaza TL. Si ndani ya Tanzania tu, bali Kimataifa.

TL hahitaji hata mabango. Kivuli chake tu kinatosha kumfanya Jiwe aamrishe jeshi la polisi likafanye fujo. Sauti yake tu inamdanya Magufuli apimwe presha mara 3 kwa siku.

Halafu eti unakuja hapa na uchambuzi huu wa elimu ya msingi?

Jipangeni sawa sawa. The end has come.
Nyie nyumbu bana watu waajabu sana kwa kubadilika, kwenye list of shame, Tl et al., hakumuita fisaidi EL afu mkaanza kumsafisha tena? CCM itabaki madarakani mpaka huu upinzani njaa uuangane na kuwa chama kimoja.
Nyerere aliwapa ushauli ila vile vichwa vyenu ni maji bado vileviele.
 
Tuna utawala wa kipumbavu sana, enzi za Nyerere watawala wa namna hii aliwaita WASHENZI NA WENDAWAZIMU. Kushindwa kuwajibika kwa serikali hii katika matukio ya kifedhuli yanayoendelea nchini, inamaana TANZANIA HATUNA SERIKALI. Bali kuna GENGE TU linalotawala kihuni na kihalifu, utawala wa namna hii SASA BASI.
NA TUNAWAPINZANI WENDAWAZIMU HAIJAWAHI TOKEA, YAMESHINDWA KUUNGANA NAKUWA CHAMA KIMOJA ILI KIWEZE KULETA UPINZANI MADHUBUTI ANGALAU KAMA ULE WA 2015. TATIZO LA KUVIFANYA VYAMA VYA SIASA MALI YA MTU BALI YA KUWA CHAMA CHA WATU WOTE, NDO MAANA MKO HIVO MPAKA LEO.
 
Ndugu zangu,

Napenda kumshukuru Mungu kwa kunipa siku ya leo.

Katika uchaguzi ambao niliufuatilia kwa karibu kubwa sana tangia nianze kufuatilia siasa na wanasiasa, basi ulikuwa ule wa 2015. Ulikuwa uchaguzi wa kipekee sana kuwahi kutokea hapa nchini, na ulikuwa uchaguzi mgumu sana kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), ila CCM walicheza karata kubwa sana ya kumweka Mh. Magufuli. Kwa kutumia rekodi za nyuma za umahili wake wa uchapazi kazi katika kila wizara aliyoteuliwa, ilinifanya kura yangu nimpe huyu ndugu. Na kama CCM wangempitisha Membe, basi kura yangu ingeenda kwa Mh. Lowasa. Na itachukua miaka mingi sana kuwa na uchaguzi kama ule.

Kamari ambayo waliicheza Ukawa, hasa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kwa kumkaribisa Mh. Lowasa (), Mh. Mbowe alikuwa na furaha mno na confidence kubwa sana huku alikuwa anajua kabisa Lowasa anaenda kuingia Ikulu, kulingana na nyota ya siasa amabayo Lowasa alikuwa nayo ambayo ilisababishwa na kuwa na maandalizi ya muda mrefu kwa nafasi hii kubwa kabisa katika kulitumikia taifa. Kama ukisikia mafuriko ya watu kipindi cha Mh. Lowasa, basi yalikuwa mafuriko kwelikweli, Tundulisu hawezi hata kumfikia nusu yake ()

().

Kipindi hiki naona kama Mh. Mbowe hana ile confidence kabisa ambayo aliyokuwa nayo 2015 kipindi cha Mh. Lowasa (). Kwa kutumia uwezo wangu, ambao amenipa mwenyezi Mungu wa kusoma saikolojia ya mtu, yafuatayo yanaweza kuwa ndio sababu ya Mh. Mbowe kuloose confidence kabisa kuelekea uchaguzi mkuu, yaani hajui kinachoenda kutokea. TL alipokuwa Arusha kusaka wadhamini, wananchi walimtaka Mbowe aongee, Mbowe akaja na hakusema chapuo lolote kwa TL, badala yake alitaja kauli mbiu tu (). Kwa jambo hili kwangu linaweza kubeba hoja zifuatazo:

  • Mbowe alikuwa anajua kabisa kuwa watu walikuwa wanamtaka Tundulisu ili aweze kupeperusha bendera ya uraisi Chadema kwa sababu ya lile tukio la mashambulizi dhidi yake ili kulenga kura za huruma ya wananchi, ila bado najiuliza kwa nini aliamua naye kutangaza nia, baadae akaacha?
  • Au Mbowe aliogopa aibu ya kushindwa na Lisu, maana asilimia kubwa ya wajumbe walikuwa wanataka Lisu apeperushe bendera?
  • Kuna uwezekano Mh. Mbowe alikuwa anajua kabisa, Tundulisu hana uwezo wa kupambana na Magufuli, ila kura atakazopata zitakuwa za huruma ya wananchi, ila kwakuwa mkutano mkuu ulikuwa unamtaka TL, basi hakuwa na namna yoyote zaida ya kuunga mkono
Namalizia nakusema, Mh. Mbowe hana confidence kabisa kwenye uchaguzi huu, japokuwa wengine wanaonekana wanayo, ila ni tofauti sana na huyu ndugu, anajua kabisa Lisu hawezi kuifikia level ya Lowasa, hata nusu yake hawezi, ila ataleta upinzani angalau kidogo tu.

Asante,
Nawasilisha
Kejuu

Delete ccm Oct 28
 
Hamna kitu kama hicho Lissu kama Lisu anajinadi mwenyewe haihitaji mbwembwe kumwelewa
 
Sasa wewe huoni ndugu yako alikwishaanza kampeni hata kabla ya muda wake kuanza? Si anajifanya much know, sasa ngoja uone atakavyokatwa, na angalieni msije mkasusa uchaguzi. We unaona vyama vingine vinafanya kampeni kabla ya muda wake?
Kutafuta wadhanmini ni kampeni??? Miaka yote chaguzi zimekuwa hivi, wagombea hutafuta wadhamini mikoani, 2020 sheria imebadilika lini??
 
Kwamba hujui kila rais anapomalza muda wake hasa miaka 10 uchaguz unakuwa moto sana? Je hujui kampen hazijaanza? Je hujui watu wametishwa sana mpaka vyombo vya habari havipo huru tena? Je umesahau demokrasia iliyokuwepo wakat wa kikwete?
 
Nikupe angalizo tu kuwa ubadilishe katiba usibadilishe kama utakuwa na viongozi kama akina Tundulisu, nikuiachia nchi kuwa mikononi ya mabeberu. Unayakumbuka Makinikia alivyokuwa anafanya?

..nasikitika kuwa umepotoshwa kuhusu makinikia.

..bado yanasafirishwa kwenda nje, na wananchi hatujaambiwa yanapelekwa wapi.

..Jpm alikuwa anatafuta popularity tu, lakini suala la utetezi wa rasilimali TL alitetea tangu miaka ya 90.
 
22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom