ipo siku utakufa
Senior Member
- Dec 8, 2016
- 146
- 530
Takriban miezi 2 au 3 imetimia sasa tangu tulivyotangaziwa kuwa Ben saa nane amepotea.Wiki 3,4 za mwanzo taharuki ilikuwa kubwa huku campaign ilianzishwa ya "Bring back Ben" na watu walibadilisha profile picture zao haswa za Facebook kuonyesha solidarity.
Imetimia sasa miezi 3 tangu Ben apotee na hali inavyoonyesha tukio la Ben kama limeshazikwa na kupotea pia.Kuna msemo unaosema usiwe kama bendera iki maanisha usipelekwe pelekwe hovyo hivi karibuni kumekuwa na matukio mengi ya kisiasa hivyo ishu ya Ben imepotea ghafla lakini mwerevu huwa hasahau,matukio yote anayaweka kwenye uzito sawa.
Chadema wameonekana kimya sana kwenye tukio la Ben na ukizingatia Ben alikuwa msaidizi wa kiongozi wa chadema.Mwanzoni Chadema walisema suala la Ben lipo polisi na watatoa ushirikiano lakini imeshapita miezi sasa mbona hawatupi feedback na mbona hawatoi tamko na kushinikiza ??
Nimeshangaa kuona Wema sepetu akithaminiwa sana na viongozi wa Chadema kuliko uhai wa Ben.Wakili msomi Tundu Lissu amejitoa kimaso maso kumtetea Wema sepetu na mh Mbowe amekuwa karibu sana na Wema huku Ben akisahaulika
Leo viongozi na wajumbe wa Chadema wakiongozwa na Mh.Mbowe,Lowassa nk walijumuika na Wema sepetu uwanja wa Taifa wakiwa na tabasamu zito huku Ben akiwa amesahaulika
Attention anayoipata Wema mbona Ben hajaipata?kwanini wakili msomi Lissu,Mbowe wasingekuwa wanapigania Ben apatikane,agenda ya Ben wangeipa kipaumbele
1. Je ina maana kubenea alikuwa sahihi kwamba Ben amejipoteza ili apate umaarufu wa kisiasa hivyo viongozi wa Chadema wameamua kumpotezea.
2.Na kama kweli kapotea basi uongozi wa Chadema ni bure kabisa yani Wema kapata attention kubwa huku suala la Ben likiwa kimya na haieleweki
http://www.jamiiforums.com/mobile-gallery/85435d16bce58fedaa4545536bcc6fa9.jpg[/IMG]