Mbowe: Hatukubali matokeo EALA na tutakwenda mahakamani

Mimi ni ccm,lakini sikubaliani na bunge kuwapigia wagombea wa Chadema hapana,wenje na masha wanafaa kuwakilisha nchi eala,tuangalie taifa kwanza,tatizo wananchi wa Tanzania hatuna kitu maslahi ya Taifa kwanza,yaani tupo kisiasa zaid ambazo hazina maslahi kwa Taifa,


Kwa hiyo unawalazimisha watu wote wa one jinsi unavyoona wewe?
 
Issue ulikuwa ni ndogo tu kwa Chadema,wangeweka wagombea wanne(wawili wa kike na wawili wa kiume).
Hiyo ingetoa kabisa huu Ngonyani wote kwani in future kwa political party tunapata shaka kwa jinsi ambavyo wanabinya demokrasia hata kwa ndani ya Chana chao na wanachama wenyewe.
Nadhani ni fundisho pia kwa vyama vingine kwa hili lililotokea jana.
Bado hujaelewa hiki pambano mkuu,ccm walivyo na chuki hata ukiweka jiwe ligombee na masha ccm wange pigia hilo jiwe kwa ajili ya chuki.hivyo chadema waliliona hilo mapema ndo mana wakabana
 
Mbona Ccm wameleta wagombea 12?
Mbona Chadema hawakuleta pairs ili demokrasia ichukue mkondo wake lakini pia suala la jinsia.
Potelea mbali basi wangeleta wote wawili wa kike AU mmoja wa kike na mmoja wa kiume (very simple logic?
Why wategemee Ccm ndio ibalance gender equality?
It's shameful.
 
Kwa hiyo utaniambia hapakuwa na sababu ya kupeleka majina bungeni sababu viongozi wa chadema walishachagua?
chadema kazi yao ni kupeleka majina ya kupigiwa kura bungeni. mchakato wa bunge kupiga kura ni mchakato wa bunge, si ccm .
Kuna maana gani cdm kuwa na nafasi mbili?he ccm 6?toka lini can wamekuwa wabia wa cdm?hv mfano leo lisu angegombea unazani can wangempgia kula?ccm hapo wamechemka.
 
kwa hili siwaungi mkono kamwe. nini maana ya demokrasia? chadema jiangalieni zaidi mwazidi kuporomoka zaidi......
Demokrasia gani ya kukomoana makusudi? Africa wachawi wengi ni wazee ebu angalia wabunge wa CCM wengi ni wazee lakini wana mambo ya kihuni kuliko hata vijana ndiyo maana wengi ni rafiki zake Daud bashite.
 
Baada ya Wagombea waliopendekezwa na CHADEMA Wenje Na Masha kupigiwa kura nyingi sana za HAPANA kuwania kuiwakilisha Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki

Mbowe ameibuka na kuongea na wanahabari na kusema kuwa wanapinga matokeo hayo, na wanajiandaa kufungua kesi mahakamani kupinga matokeo hayo!
Nendeni kwq sabbu Tundu lisu ni Rais wa Chama cha wanasheria Mtashinda sabbu siasa zimehamia Mahakamani now days.
 
Sasa kwa taarifa ni kwamba hata wabunge wa CDM wengi wao walipinga uteuzi wa MASHA na WENJE tu...
Kwanini Masha?!aliyeoka CCM huko baada ya kukatwa ndio leo aingie Chadema na kusafishwa then aje achukue madaraka kirahisi?!kuna vijana wameipigania Chadema tangu inaanza lakini mpaka leo hata uwenyekiti wa tawi hawajawahi kupewa!!

Majina ya wagombea Mbowe aliyatoa mfukoni,hawakupigiwa kura hata ndani ya Chadema,wanachadema wameshangaa tu mwenyekiti analeta majina mawili tena bila ya kura!!

Sheria ilikuwa inataka kila chama kizingatie Gender,na mchakato uwe wa halali ndani ya chama.

CDM wamelinyima bunge haki ya kuchagua!!huko ni kulazimisha mamlaka..l
Kwakuwa nafasi 2 za Chadema bado ziko wazi,basi ni wakati sasa wa Mbowe kurudi Chamani na kufanya uteuzi kwa Democracy na sio kuja majina mfukoni!!
 
Ni muda muafaka kwa CHADEMA kubadili kifungu chake cha katiba ili iruhusu wasioridhika na maamuzi ya chama waende mahakamani.

Kwamba mwanachama asiporidhika na maamuzi ya chama ahame chama,sasa mbona wao hawahami nchi wasiporidhika na maamuzi kama hayo ya Jana?

Ni unafiki kwamba ndani ya chama marufuku mwanachama kwenda kupinga maamuzi ya chama mahakamani ilhali chama kiko mahakamani kila siku kupinga maamuzi mbalimbali.

Kama HAKI inapatikana mahakamani then kwa nini wawazuie wanachama wao kwenda huko wasiporidhika na maamuzi ya chama?

Chama chenye the so called wanasheria nguli kinakuwaje na vifungu vya kipumbavu hivyo kwenye katiba yake utadhani lile Ni shirikisho la mpira WA miguu mwanachama wa FIFA.
 
Mchakato wa kuleta wabunge Mfukoni umewagharimu.
Anzeni kuleta demokrasia ndani YA chama chenu kabla ya kumnyooshea kidole Magufuli.
Ona aibu YA mwaka hiyo, na bado
 
Chadomo=Chadema ,huko shule mlienda kusomea ujinga.
PhD ya ikulu mbona inamkumbatua bashite mwenye vyeti feki? Shule ya CCM ni kukomoana? Aliyekuambia kwenda shule ya ujinga ni kudai haki ni nani? Kufanya mambo ya ajabu kama ya CCM ndiyo kusomea Ujanja?
 
kwa hili siwaungi mkono kamwe. nini maana ya demokrasia? chadema jiangalieni zaidi mwazidi kuporomoka zaidi......
Wagombea wanaohitajika ni wawili. Na chadema imependekeza hao hao wawili. Sasa kuna haja gani ya kupiga kura?

Kuwapigia kura ya hapana ni sawa na kusema hatuwataki hao leteni wengine which means ccm watakuwa wanawachagulia chadema wagombea badala ya chadema kuchagua wenyewe.
 
Tumefurahi sana jana bunge letu limeonesha maana na umuhimu wa democrasia. Mtu apite kwa sifa sio kuchaguliwa na watu flani tu. CCM wanamchakato mzuri sana ktk kutafuta wagombea wao, acheni ubishi kwa hilo
Ni kweli Ndio maana mwenyekiti aliendana majina mfuko kamati kuu

Sent from my Lenovo A2010-a using JamiiForums mobile app
 
wapiga kura waliona wagombea hawafai, ndo sababu wakapiga kura ya hapana. Vp ulitaka wapigiwe kura tu hata kama hawana sifa mkuu?
Sifa ni zipi? Maana iwe isiwe lazima chadema ipeleke wabunge wawili.
 
Kilichofanywa na CHAEDMA hata kama siyo kosa kikanuni, ilitakiwa hekima zaidi. Sioni mantiki ya kupeleka majina mawali tu wakati wanaohitajika ni watu wawili. Ilikuwa hekima zaidi kupeleka angalao majina manne au matano ili katika hao wapatikane wawili.
 
Tusipangiane, cdm hawataki kupangiwa na ccm na ccm hawataki kupangiwa na cdm kwaio ni burudan! ila kwa maoni yangu cdm walistahili kupeleka wagombea 4 kutoa wigo mpana katika ugombeaji katika chama, Kupanua demokrasia katika chama, kukuza Iman kwa wanachama, Kuonyesha kuwa wanahadhina ya wagombeaji wenye sifa, kufuta dhana ya ' majina yalitoka mfukoni' kuruhusu kushindana nyinyi kwa nyinyi na kuaminiana.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom