Uchaguzi 2020 Mbowe: Hatuendi kwenye uchaguzi kuomba kuwa Chama Kikuu cha Upinzani, tunatafuta dola

Fundi Mchundo

JF-Expert Member
Nov 9, 2007
5,077
2,000
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Mhe. Freeman Mbowe amesema, kuna baadhi ya vyama vya siasa na wanasiasa hasa wanaCCM wanasema tuachane na Urais tujiandae kwa Ubunge na Udiwani, Mbowe anasema stage ya kuwa chama kikuu cha Upinzani wameshaipita wanaingia kwenye uchaguzi mkuu kutafuta kushika dola.

"Hatuendi kwenye uchaguzi kuomba kuwa Chama kikuu cha upinzani, sisi ni Chama kikuu cha upinzani, tunakwenda kwenye Uchaguzi kutafuta dola. Hivyo vyama vingine vinakwenda kutafuta wabunge na madiwani" M/kiti wa @ChademaTz Mhe. @freemanmbowetz.
Anataka kusema ACT Wazalendo wanaenda kutafuta wawakilishi katika Baraza la Mapinduzi na si urais wa Zanzibar? Anatakiwa kukumbuka kuwa chama chake kinahitaji kushirikiana na vyama vingine ili kiweze kushika dola. Kwenye hili, Zitto amemzidi.

Amandla...
 

Nyanjomigire

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
6,006
2,000
Ila hii ni ngumu maanake unaenda kucheza na timu ambayo mchezaji wake moja ni refa na wengine wawili ni washika vibendera na kocha wao ndio Kamisaa halafu unatarajia mshinde, labda Yesu ndio awe striker wenu.
 

Jumbe Brown

JF-Expert Member
Jun 23, 2020
944
1,000
Watanzania mtatawaliwa kimabavu kwa miaka mingi ijayo.
Acha KUJITIA HOFU na kuwatia HAMANIKO la nafsi wenzako...mbona hayo hayapo Kaka.....
Km unataka CCM ipitishe katiba itakayokuwa Ina watetea mashoga na walawiti wa LGBT basi kweli nakuunga Mkono,hilo halitawezekana....
 

kantasundwa

JF-Expert Member
May 25, 2020
789
1,000
Hata rais wa malawi na chama chake hawakuamini Kama wangeondolewa madarakani..lkn kwa sasa ndo wanajutia kuwa nje...mwaka huu hamtaamini na masikio yenu cku hiyo mnatangaziwa kuwa mshndi ni mhe.Lissu
 

SPINE

JF-Expert Member
Dec 11, 2017
995
1,000
Hahahahah ......watu wana vituko sana ....wekeni hoja za kudhani mtapata dola
 

Kalamu1

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
6,587
2,000
Mkuu mazingira ya sasa yanajieleza wazi kabisa,upinzani kushika dola kwa sasa ni sawa na kupiga tiktaka ukiwa umevaa kanzu.haiwezrkani.
Na technology yote iliyopo sasa bado hutaki kuamini kwamba inawezekana sana ukapiga tiktak huku umevaa kanzu?

Mbona ni kama bado unaishi gizani mkuu!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom