Mbowe hamasisha wafuasi wa CHADEMA wafanye shughuii za kiuchumi badala ya harakati zisizo na tija

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,997
Ndugu zangu,

Kuanzia mwaka 2005 kulizuka wimbi la vijana kuingia kwenye harakati za kisiasa hususani waliomaliza vyuo ambao walikuwa wameajiriwa serikalini na sekta binafsi.Baadhi yao walikuwa wameshindwa kumaliza vyuo kwa sababu mbalimbali kwa mfano John Mnyika.

Vijana wengi waliacha kazi ya ualimu na kujikita kwenye siasa wakilenga kupata udiwani,ubunge nk.baadhi yao walifanikiwa kama akina Boniface Jacob,Silinde nk.lakini kundi kubwa halijafanikiwa hili linaongozwa na akina Mkisi,Pamba nk.

Mbowe,fahamu ya kuwa wengi wa walioacha ajira serikalini na kutofanikiwa kwenye siasa wana hali ngumu kiuchumi.Wamejawa na hasira usipokuwa mkweli kwa kuwashauri watafute cha kufanya mkono uende kinywani uenyekiti wako haupo salama.Watakuuza ukiwa hapo juu kumbuka "njaa haina baunsa" na wala "hakuna mkate mgumu mbele ya chai"

Matusi mitandaoni au kuitakia nchi mabaya havitawakwamua kiuchumi na badala yake wachape kazi.

Nawasilisha
 
Yaani tatizo la ukosefu wa ajira lililochangiwa na serikali kukosa ubunifu naona sasa lumumba mnaomba msaada kwa Mbowe.

Unataka Mbowe awape kazi gani hao vijana? na una hakika nyie mnaosifia CCM mna ajira au mmeridhika tu na vibarua vya buku saba kwa siku?
 
Tuendelee kuwakopesha fedha wanaCCM wanaotulilia shida huku mtaani?
Naona Bata anamfundisha kuku kunya. This is shame. Yaani CCM wanajiona wajuaji huku wakipewa msaada wa 150k na waziri kutoka China na wanaruka live TV zote nchini. Hii nchi hii!!! Na kwataarifa yake hakuna wapambanaji kama vijana wa upinzani. Hawaishi kwa mategemeo ya kusubiri teuzi wala kupewa mb na wabunge.
 
Itakuwa mkeo amekutoroka sasa unaandika vitu visivyoingia kichwani, wewe unauwezo wa kumtambua mwenye njaa ni mfuasi wa Chadema! Huu ni ujinga.
 
Huu utafiti umefanyia ofisini? viti maalum huna jimbo huna ofisi sijui uko barabarani? Nenda popote vijana wapinzani halisi siyo ombaomba, wote ni wajanja na wapiganaji. Waambie vijana wa Lumumba watafute kazi za kufanya maana wenzao walijitambua siku nyingi.
 
Kamanda tafuta shughuli ya kupatia kipato
Huu utafiti umefanyia ofisini? viti maalum huna jimbo huna ofisi sijui uko barabarani? Nenda popote vijana wapinzani halisi siyo ombaomba, wote ni wajanja na wapiganaji. Waambie vijana wa Lumumba watafute kazi za kufanya maana wenzao walijitambua siku nyingi.
 
Bwana mkubwa miaka zaidi ya 15 wanakula nini? Halafu vijana hawa si kama wenzao wa ccm tu nao wanakesha kutukana mitandaoni au wenu mnawalipa?
 
IMG_20210108_090651_7.jpeg
 
Nawewe hamasisha kukamua kodi na vyanzo vingine vya mapato kutoka shughuli hizo za kiuchumi watakazo anzisha.
 
Back
Top Bottom