Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 117,601
- 217,993
Kuna msemo wa Kiswahili unasema hivi, nanukuu, "Usishindane na aliyejaaliwa," mwisho wa kunukuu.
Freeman Mbowe ni mtu aliyejaaliwa karama ya kupendwa, hili wahafidhina mnatakiwa mlijue, mtake msitake! Watu wa namna hii hawatokei mara nyingi sana kwenye jamii, ni wachache sana, hata hivyo kupendwa kwa watu hawa hakuji kwa bahati mbaya, mara zote kunakuwa na mpango fulani wa Mungu juu ya maisha yao.
Uchunguzi wangu wa muda mrefu juu ya maisha ya Freeman umebaini kwamba, mtu huyu hajawahi kumchukia mtu yeyote yule (personally), anaweza kuichukia mifumo fulani au mambo fulani yanayotendwa na watu fulani lakini hakuwahi kuwachukia watu kama watu binafsi, ni nadra sana kupata mtu aliyejaa upendo wa kiasi hiki kwenye Taifa, na ikitokea inakuwa Baraka kubwa sana kwa Nchi.
Ndio maana popote anapokuwepo huyu jamaa watu hujaa, wa kumshangilia wanakuwa wengi kuliko wanaomzomea, iwe Mahakamani, Kanisani, kwenye Majukwaa ama kwingineko.
Mungu aendelee kumbariki tu, Amina.