Salary Slip
Platinum Member
- Apr 3, 2012
- 49,033
- 151,255
Mbowe amekaa kwenye hiyo nafasi kwa muda mrefu na amefanya mengi mazuri na bila shaka kuna mambo hakuyafanya vizuri kama binadamu.
Hata hivyo; ni hulka ya wanadamu kutaka mabadiliko hata kama utakuwa kiongozi mzuri kiasi gani. Kuna wakati utafika watu watatakka ukae pembeni upishe wengine.
Sio hivyo, katika kuonyesha demokrasia ya kweli na kuonyesha kutokuwa na uroho ws madaraka pamoja na kuonyesha utofauti na vyama vingine, Mbowe alipaswa kuyaona yote haya mapema na kutangaza l kutogombea tena hiyo nafasi ili atoe fursa kwa wengine.
Hii ingemjengea heshima, ingeimarisha umoja katika chama na kuondoa hatari ya kuwagawa wanachama na hata kukivuruga chama kwa ujumla. Tukumbuke maadui zetu hasa CCM wanatamani tuvurugane kwahiyo tusiwape hiyo nafasi.
Kwa sasa nafasi bado anayo, ila uamuzi wowote ataoufanya sasa baada ya Lissu kutangaza kugombea uenyekiti, utapokelewa kwa hisia tofaut.i Mojawapo ni hofu ya kushindwa na Lissu jambo ambalo lisingetokea kama angerangaza kutogombea kabla ya Lissu kujitokeza kugombea hivyo nafasi.
All in all, Mbowe ni wakati wa wewe kustaafu kwa heshima kuliko kung''ang'a hiyo nafasi. Ni wakati wa kuonyesha kwa vitendo tofauti ya CHADEMA na vyama vingine hasa CCM wanaotoa form moja ya kugombea uenyekiti wa chama Taifa na hata kwa mgombea uraisi.
Mwisho, naahauri wajitokeze na wengine ili Lissu asigombee pekee yake ingawa Lissu kwa sasa huu ni wakati wake.