Mbowe, Dr Slaa na Mnyika ni viongozi hovyo hovyo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe, Dr Slaa na Mnyika ni viongozi hovyo hovyo

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Dec 15, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Dec 15, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Na Mwandishi Maalum

  NIMEFUATILIA kwa siku nyingi sana kelele zinazopigwa na viongozi waandamizi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuhusu kile kinachoitwa kuwa ni "kashfa" ya Richmond na ile ya kuchotwa kwa shilingi bilioni 133 kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kinyume cha taratibu.

  Sina sababu ya kuhadithia upya kuhusu kashfa hizo, bali ninataka kuzungumzia hatua ya viongozi wa CHADEMA ya "kuzishikia bango" na kutumia kivuli hicho kuficha ubadhirifu wa mamilioni ya fedha wanaofanya katika chama chao.

  Wanachama waliojazwa imani kuwa chama chao kinaongozwa na viongozi waadilifu katika matumizi ya mamilioni ya fedha za ruzuku na zile zinazotoka kwa wahisani na wafadhili wamekuwa mstari wa mbele kushangilia kila tamko linalotolewa kwa namna moja ama nyingine na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe; Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Peter Slaa; Naibu Katibu Mkuu (Tanzania Bara), Zitto Zuberi Kabwe na Mkurugenzi wa Taifa wa Vijana, John John Mnyika.

  Tathmini ya uhakika inaonyesha kuwa viongozi hao wanne ndio wamekuwa vinara wa kutengeneza na kuhubiri kila aina ya uzushi na uongo dhidi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na serikali yake, na pia wanataka wanaonekane wajuzi na wataalamu mabingwa wa kutetea raslimali za taifa na Watanzania.

  Pamoja na kufanya hivyo mara kwa mara kwa kutumia majukwaa ya siasa mikutanoni, vyombo vya habari na intaneti, ukweli kuwa lengo lao hasa ni kutaka sifa kwa faida zao wenyewe unaweza kuthibitishwa kwa namna nyingi, moja kati ya njia hizo ukiwa "udandiaji" wa kila "ishu" inayofanywa na serikali na kuipotosha kwa kadri wawezavyo.

  Ndivyo alivyofanya Mbowe alipowahutubia akina mama wa CHADEMA kwenye ukumbi wa Urafiki, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakati akiwahutubia katika Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani hivi karibuni.

  Si lengo langu kuwasemea wanachama wa CHADEMA kuhusu vilio vyao vya chini chini kutokana na woga wanaojazwa, lakini ukweli kuwa chama hicho hakina nidhamu ya matumizi ya fedha za ruzuku na wahisani yamewahi kulalamikiwa hadharani na Mwenyekiti wa Chama hicho wa mkoa wa Mara, Chacha Zakayo Wangwe mwishoni mwa mwaka uliopita.

  Pamoja na mambo mengine, Wangwe alikuwa akipigania ruzuku iende kwa wanachama katika matawi, kata, wilaya na mikoani zikaijenge CHADEMA kuliko hali iliyopo hivi sasa ambapo fedha hizo za walipa kodi zimekuwa "zikitafunwa" na viongozi waandamizi utadhani zinaliwa na mchwa katika makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam.

  Nakubaliana kwa asilimia 100 na hoja hiyo ya Wangwe ambaye hata hivyo inasikitisha kuona alipochaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti kelele zake hizo zimekwisha, badala yake ameungana na kundi hilo ambalo wakati akiwania nafasi hiyo alikaribia kulisambaratisha kama kishada kilichokwenda harijojo.

  Je, yuko wapi Wangwe aliyekuwa mpinzani mkubwa wa matumizi ya helikopta inayoonekana kuwa ya Mbowe zaidi badala ya CHADEMA ingawa inakodiwa kwa shilingi milioni tatu kwa siku zinazolipwa na chama, lakini ambayo kama Mbowe hayupo nchini haikodiwi hata kuruka kwa dakika tano tu?

  Yuko wapi Wangwe aliyekuwa kinara wa mapambano dhidi ya matumizi mabaya ya ruzuku inayofujwa kwa idhini ya Ofisi ya Katibu Mkuu, yule ambaye anapokwenda Karatu ama bungeni anajifanya ana uchungu mkubwa na fedha za walipa kodi, lakini anapokuwa Makao Makuu ya CHADEMA anasimamia ubadhirifu anaodai kuupinga mikutanoni?

  Yuko wapi Wangwe aliyekaribia kusababisha Zitto na Dk. Slaa wajiuzulu nyadhifa zao wakidai wamedhalilishwa, yule ambaye alipokuwa akitafuta achaguliwe kuwa Makamu Mwenyekiti alikuwa na ujasiri mkubwa wa "kupasua" ukweli na kuanika maovu yote yanayofanywa katika chama chake?

  Je, inawezekana kwamba amenyamaza baada ya jina lake kuingia katika orodha ya "vigogo" wanaolipwa fedha nyingi za mishahara katika Makao Makuu ya CHADEMA huku wakidai ni posho ili kuwazubaisha wasiolipwa hata senti tano waliopo kwenye matawini, kata, wilaya na mikoani?

  Mbali na kaka yangu Wangwe, nashindwa pia kujua kinachosababisha Mkurugenzi wa Taifa wa Vijana, John John Mnyika asipinge wala kusema chochote kuhusu matumizi ya ovyo ya fedha za ruzuku, lakini kama Wangwe inawezekana pia anafanya hivyo kwa sababu naye ni mmoja wa wakurugenzi wanaolipwa malaki katika mishahara yao huku wakicheza "danganya toto" kwa kudai eti kwamba wanajitolea!

  Wanaodhani Mnyika ni kiongozi mwenye uchungu wa kweli na fedha za walipa kodi anapopiga kelele za EPA, Richmond ama mkataba wa Buzwagi na kuanza kumshangilia kwa nderemo na hoihoi hawajui kwamba ni mjumbe wa vikao vyote vya Sekretarieti, Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano Mkuu wa Taifa huku pia mara kwa mara akikaimu Ukatibu Mkuu wa Chama; lakini hata siku moja tu hajawahi kupendekeza kuwa mamilioni ya fedha hizo za ruzuku "yanayotafunwa" kwa fujo yatengenezewe mfumo wa kutumika mpaka matawini.

  Simwelewi Mnyika anapopiga kelele nyingi magazetini akitangaza "utakatifu" wa kisiasa huku akishindwa kuzuia ubadhirifu uliokithiri katika chama chake, akashiriki kudhulumu wanachama na viongozi wanaosota matawini, kata, wilaya pamoja na mikoa ingawa ni wao waliofanya kazi kubwa zaidi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005 na hatimaye kukiwezesha kupata ruzuku inayokaribia shilingi milioni 100 kila mwezi.

  Wakati akiwa sehemu ya wateule wachache kabisa wanaofaidika na fedha hizo, Mnyika mwenyewe ni shahidi kwamba hakuna cha maana anachowafanyia vijana wa CHADEMA iwe Dar es Salaam, Kigoma, Arusha, Ruvuma, Tanga, Pemba na kadhalika.

  Kama anabisha atuambie mwaka jana alifanya ziara ngapi za kikazi katika na mikoa ipi ili tuone iwapo kweli ni Mkurugenzi wa Taifa wa Vijana wa CHADEMA na siyo Mkurugenzi wa Taifa wa Mafaili Ofisini, kisha aseme katika ziara hizo alibeba agenda zipi za kukijenga chama hicho ili tujue kama anapokea mshahara kwa haki hata bila kuhoji posho nyingine.

  Aseme amekwenda wilaya zipi nchini katika kipindi angalau cha miezi sita tu iliyopita ili kuwahamasisha vijana wa CHADEMA wazidi kushikamana, vinginevyo atueleze amehutubia mikutano mingapi ya hadhara katika kipindi hicho kama hashindi tu ofisini "akicheza" na intaneti akidhani atamwezesha rafiki yake Mbowe kushinda urais mwaka 2010.

  Hata kwa siasa dhaifu kiasi gani haiwezekani kwa kiongozi mwandamizi kama yeye ategemee kujenga chama ili baadaye kije kushinda uchaguzi mkuu kwa makala za intaneti huku takribani zote zikisheheni uongo na uzushi dhidi ya CCM na serikali yake.

  Ni Watanzania wangapi wanaoishi mijini wanatumia intaneti iwe kwa shughuli zao wenyewe ama za kikazi ili awe na imani ya wapiga kura kuzisoma makala zake anazoandika huko na kutarajia ushindi mwaka 2010? Au, ni kijiji gani nchini ambako wananchi wamewahi angalau tu kusikia neno linaloitwa intaneti achilia mbali kujua maana au hata shughuli zake?

  Wanaodhani Mnyika ana mchango mkubwa kwa CHADEMA hawapembui mambo kwa upana, na pia inawezekana ni wavivu wa kufikiri na hivyo wao wenyewe ni kama usiku wa giza.

  Inawezekana wanachama na viongozi wa CHADEMA waliopo kwenye matawi, kata, wilaya pamoja na mikoa hawajui kama chama chao kinapata mamilioni ya fedha za ruzuku, yale ambayo badala ya kukijenga "yanatafunwa" na viongozi na maofisa wa makao makuu huku wakidanganywa na kuaminishwa kuwa chama kinaendeshwa kwa kufadhiliwa na Mbowe, Edwin Mtei, Philemon Ndesamburo na matajiri wengine rafiki.

  Kama Mbowe na Dk. Slaa ni viongozi waadilifu na waaminifu katika pesa waonyeshe mgao wa ruzuku ya karibu shilingi milioni 100 inavyotumika katika chama chao, waseme makao makuu inatumia kiasi gani kila mwezi na mikoani zinakwenda kiasi gani ili kulipia kodi za ofisi na mahitaji mengine, vinginevyo wamsute uso kwa uso Chacha Wangwe kuwa ni muongo aliposema hakuna chochote kinachopelekwa.

  Nasema kifua mbele na bila mashaka yoyote kwamba kitu pekee kinachosaidia kuficha ufisadi uliopo CHADEMA ni ukweli kuwa chama hicho "kipo kama hakipo", kwamba ukiondoa pale panapoitwa makao mkuu kulikobaki kote ni sawa na sufuri.

  Endapo kingekuwa kikubwa kama CCM, ukweli kuwa mamilioni ya fedha za ruzuku "yanayotafunwa" na viongozi wa makao makuu utadhani zaka ungekuwa umeshafichuka.

  Ndiyo maana ukifika hapo hakuna agenda yoyote ya kukijenga chama ili kiwe na nguvu isipokuwa watu wako "bize" kuandika makala za uzushi katika intaneti, na pia hakuna mkakati wowote wa muda mrefu wala mfupi unaolenga kukiinua kiuchumi ili kisiwe ombaomba kupita kiasi. Kubwa linalofanywa na viongozi waliopewa madaraka ya kitaifa ni kujijenga wenyewe ikiwemo kujilipa mamilioni ya fedha za ruzuku pamoja na kutoka kwa wahisani na wafadhili.

  Wanaobisha kuhusu ukweli huu wamuulize Wangwe imekuwaje ageuke bubu muda mfupi tu baada ya kuchaguliwa kwake kuwa Makamu Mwenyekiti miezi mitatu iliyopita. Aseme kwa nini ameachana kabisa na mapambano ya kupinga kwa nguvu zake zote ubadhirifu mkubwa wa ruzuku unaozidi kushika kasi katika makao makuu ya CHADEMA.

  Wahoji inakuwaje chama kinakodi helikopta kwa shilingi milioni tatu kwa kila dakika 60 inazoruka angani huku wakati huohuo kikishindwa kupeleka angalau tu shilingi elfu tatu kwa mwezi katika kila mkoa hata kama ni mara mbili kwa mwaka.

  Waulize ni nani ameidhinisha maofisa wa makao makuu ya chama hicho wanaotaka kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 wajigawie kabisa majimbo watakayokwenda kuwania nafasi hiyo utadhani wanachama wote waliopo huko hawana mbele wala nyuma.

  Waulize kikao gani kiliketi na kuidhinisha wawe wanalipwa shilingi milioni moja kila mmoja kwa kufanyiana zamu utadhani wake wenza kwa mume wao huku wanachama waliopo kwenye matawi, kata, wilaya mpaka mikoa wakitengwa katika mgao huo wa ruzuku ambayo mwaka 2005 walishiriki kwa nguvu zao zote kuihangaikia.

  Waombe kuonyeshwa sheria ya ruzuku inayoruhusu fedha hizo zitumiwe na viongozi wa makao makuu kwenda katika majimbo wanayotoka na kufanyia maandalizi ya kuwania ubunge mwaka 2010.

  Wakati hayo yakifanyika kwa siri na tahadhari, "vigogo" wa CHADEMA wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa, Freeman Aikaeli Mbowe; Katibu Mkuu, Dk. Wilbroad Peter Slaa pamoja na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Zuberi Kabwe wamekuwa wakiwadanganya Watanzania eti kwamba hawana mawaa.

  Mpaka hapo uko wapi uaminifu na uadilifu wao katika chama chao kwanza ili tuweze kuziamini kauli zao wanapozungumza kwa ukali kuhusu Richmond au EPA?

  SOURCE: GAZETI LA TAZAMA
   
 2. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #2
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Naam, kweli habari ndiyo hiyo! Whistling...

  Tanzania zaidi ya ninavyoijua
   
 3. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #3
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hapana mkuu Jasusi,

  Mleta ujumbe mi nimempenda tena SANA maana ujumbe kama huu kufika hapa ni ngumu sana, tena tungejidanganya kuwa hakuna vitu kama hivi, heri kujua kuwa kuna vipo, then you better get equipped when you wanna face such people!

  Mkuu Habarindiyohiyo, ahsante sana kwa ujumbe, TAZAMA wana habari za mwelekeo huu, huwa sipati soft copy yao, huwa sipati hata gazeti lao, sipendi kusoma magazeti ya kuwa na mwelekeo mmoja tu, bora kusoma magazeti ya pande zote nichambue pumba na mchele mwenyewe!

  Kuelekea uchaguzi tutawajua makanjanja na waandishi wa ukweli tu
   
 4. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #4
  Dec 15, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Duh, kweli habari ndiyo hiyo - trust me, only in Bongo...anything's possible.
   
 5. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #5
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hapo tukiamua kufuatilia within 4 days tunaweza kupata list ya kikundi kilichoandika hiyo habari nzima, unakuta hakuna hata mwandishi wa habari mmoja, wote wako kwenye mission moja tu...

  Sielewi taaluma ya habari inaelekea wapi!
   
 6. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #6
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Hili Tazama ni gazeti la nani? mbona halizingatii maadili ya uandishi? huwezi kuleta tuhuma kama hizo kama huna proof.Mambo ya kusema sijui huyu hajaenda mkoani, sijui fedha zinatafunwa! umefatilia hesabu na kufanya ukaguzi wa chama ili kutambua ni kweli kuna ubadhirifu.Waandishi kama hawa ni wale wanaochukua habari za vijiweni na kuzishadadia zionekane kuwa ni halisi.
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  They have some docs (but wrong docs) najua, a few I can mention, kina Mnyika, Mbowe na Slaa kabla hawajairukia hii hoja bora waulize... They have something they're looking for, I know what am writing, trust me guys. It's a mission!
   
 8. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #8
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli hayo unayosema naomba ni withdraw maandiko yangu hapo juu.Duuh siasa za bongo nimenyoosha mikono,ni zaidi ya kuishi kwenye nyumba ya vioo.
   
 9. Lyangalo

  Lyangalo JF-Expert Member

  #9
  Dec 15, 2009
  Joined: Sep 10, 2009
  Messages: 681
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 45
  wewe menyewe ndo wahovyohovyo, umetumwa na mafisadi
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Waweza kuta wewe ndo wa hovyo hovyo kwa kukurupuka na kumtuhumu mtu anayetuletea taarifa kutoka gazeti la Tazama kuwa katumwa na Mafisadi..

  Habari nzuri sana hii, hujui tu
   
 11. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #11
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Yani mnanikumbusha msanii mmoja maarufu Tanzania aliandikwa hapa JF kuwa aache kujifananisha na msanii mkubwa mwingine maarufu Marekani... Basi ikamkera kweli, akasema JF inamsema vibaya, akasema JF si sehem inayomtakia mema, kama tunataka ajisajili JF basi tufute hiyo topic atajisajili, nikamwambia USIJISAJILI KAMWE na haifutwi...

  Haikuishia hapo, mheshimiwa flani toka BoT kabla issue yake haijalipuka tena haijaingia kwenye magazeti ikiwa mbichi kabisa na ndio kwanza inaipuliwa JF, akasema JF mnanidhalilisha na familia yangu kwa uwongo na uzandiki wenu kwa uwongo mtupu mliojitungia bila utafiti, nikamwambia mheshimiwa kuna evidence zaidi na nikamtumia baadhi kwenye mail yake, akasema si sahihi ni wivu wa kike tu, akasema tutachemsha tu na wala hatishiki... Kwa sasa hana nafasi ya kazi tena pale na kesi yake ilishasikilizwa Kisutu....

  Namaanisha, si vema kupuuza mambo mnayodhania ni madogo, si vema kupuuza chembe ya alerts hata kama ni ndogo... Penye wengi hapaharibiki neno...! Tunaweza kwa pamoja kuidadavua hii na kuonesha wapi penye ukweli na uwongo wa habari yenyewe upo wapi!

  Watunzi wa hadithi husika hubaki midomo wazi endapo ukweli unaanikwa mapema kabla issue haijawa screwed zaidi, amka, stuka!
   
 12. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #12
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Hii kama Zilipendwa vile maana naona Wangwe anatajwa kama bado ni Mzima
   
 13. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #13
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Maneno mazito sana haya mkuu
   
 14. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #14
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,090
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  They know what they're intending to do...
   
 15. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #15
  Dec 15, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Kwa maneno haya sasa najiuliza ni nani aliye msafi na ni nani atakayeweza kusimama aseme kuwa yeye ni msafi.Kama wale tuliowaona kuwa ni wanaharakati wa kweli kabisa katika mageuzi nao wana kashfa kwenye vijihela vya ruzuku, je wakikabidhiwa nchi na mijihela yote hiyo si ndio watatuuza kabisa?
   
 16. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #16
  Dec 15, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Ukiangalia the body of the habari inawatuhumu the top layer ya CHADEMA lakini heading yake Mh!
   
 17. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #17
  Dec 15, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,321
  Likes Received: 1,037
  Trophy Points: 280
  Kweli kabisa mkuu,inaonekana ni Zilipendwa mnoo,maana yaonesha iliandikwa kipindi Wangwe akiwa hai..Mleta mada ana maana yake i think,kuna kitu kinaendelea hapa(Uzandiki???)..Ngoja tujadili tu na ukweli utajulikana...Kimsingi kuna mengi ya kujadili kutokana na habari hiyo hapo juu
   
 18. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #18
  Dec 16, 2009
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu Invisible, are you thinking what I am thinking ? Nakubali ni gea kubwa lakini je yaweza ku boomerang ? If one reads between the lines, one very obvious fact comes to mind - the timing of the post. Alliances of convenience and subsequent maneuvering were well forecast - but how many of us did take note ! Another fact is the subjects mentioned -waliopo na wasiokuwepo !
   
 19. b

  bigilankana Senior Member

  #19
  Dec 16, 2009
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 143
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  si kila neno linalowekwa hapa ni kweli. Kuna mengi ya kutunga tu kama mashairi. Hata wewe waeza kutunga yako na utapata watakaokuamini. Hii ni ngonjera tu hamna lolote
   
 20. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #20
  Dec 16, 2009
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Wakali wa habari,

  Mwenzenu nimetoka nje. Hii inakuwa kama unaangalia ile FILM ya LOST.

  Nashindwa kuelewa kuwepo kwa Marehemu Wangwe na KUKOSEKANA kwa Zitto.

  Ngoja nisubiri PICHA maana kama huelewi litaishaje, ndiyo UNAFAIDI ZAIDI.
   
Loading...