Mbowe, Dr Slaa kulitikisa Jiji la Dar Jumamosi Ijayo

Ukabila, Ukanda ndo unavyo viwaza katika kichwa chako hata kutizama kalenda tu kufahamu Tar. 26/05 ni siku ya Jmosi umeshindwa! Acha kukurupuka

Msamehe tu mkuu hajitambui huyo....
 
waungwana ingekua nzuuurii sana kama nayo hiyo ingerushwa ili na sisi wa mbali tuone live kuliko kusubiri kwenyee taarifa ya habari ucku ambapo inakua imechakachuliwa mnooo...
 
Viongozi wakuu wa CDM wakiongozwa na Mwenyekiti Freeman Mbowe na Katibu Mkuu Dr Wilbroad Slaa Jumamosi ijayo tarehe 26/05/2012 watalitikisa jiji kuu la Dar kwa kufanya mkutano mkubwa wa hadhara katika viwanja vya Jangwani.

Mkutano huo utakuwa ni maalum kuzungumza na kuwaelimisha wananchi kuhusiana na Katiba mpya. Pia viongozi hao wanatarajiwa kulaani uamuzi wa halmashauri kuu ya CCM kutenga mambo kadhaa na kuwaamuru wananchi kutoyajadili kwani yanapaswa kubaki kwenye katiba kama yalivyo.

Mkutano huo pia utahudhuriwa na Naibu katibu mkuu Zitto Kabwe, Mnadhimu mkuu wa upinzani Tundu Lissu, Mwanasheria maarufu Mabere Marando,wabunge wote wa chama hicho na wajumbe wote wa kamati kuu.

Itakumbukwa mara ya mwisho CDM kufanya mkutano mkubwa kama huo Dar ni siku ya uzinduzi wa kampeni za mgombea urais wa chama hicho mwezi Agosti mwaka juzi.

Mkutano huo unatarajiwa kulitikisa jiji la Dar na Taifa kwa ujumla kwani Maelfu ya wana-CCM wanatarajiwa kuvua Gamba na kuvaa Gwanda.

Source: John Mnyika-CDM[/QUOTE

Watayarishaji na waongozi lazima waweke miundo mbinu ya walemavu.

Hawa husahaulika sana na mimi nafahamu sana hawa ni wapenzi wenu wakubwa. Wasikilizaji wote wapewe fursa sawa
 
Angalizo kwa Chadema pale jangwani kuna ujenzi wa mradi wa mabasi yaendayo kasi wangetafuta uwanja mwingine pale kwa sasa sidhani kama panafaa...ni ushauri tu.

Heshima kwako. Ingekuwa vema kama hata ungependekeza uwanja mbadala
 
Ukonga huku vua gamba vaa gwanda inaendelea kama ilivyopangwa yupo henche,suzan kiwanga na wengineo
 
Shibuda akae upande wa wasikilizaji, asije tuchafulia hali ya hewa.
Mkuu molemo magwanda yanapatikana wapi?
 
Back
Top Bottom