Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,562
Mwenyekiti wa Chadema anayemaliza muda wake mzee Freeman Mbowe amesema chama chao kinaamini kuwa Umaskini ni laana na kwahiyo wataendelea kuhubiri sera ya utajirisho.

Mbowe amesema kila mwanachadema ni tajiri wa Roho hivyo wanakerwa sana na viongozi wa CCM wanaoukumbatia umaskini.

Mbowe amesisitiza kuwa Chadema inajiandaa kushika dola hivyo wananchi wa Tanzania waachane na Unyonge na kujiandaa kuwa matajiri wa kweli.

Source ITV habari

Maendeleo hayana vyama!


=====

Mbona makatibu wa wilaya na mikoa mnawafanyisha kazi bila malipo yaani mnawatia umasikini!!
Kifupi ni kwamba hamna mipango wala vipaumbele.. kama mngekuwa mnawalipa watumishi wenu na kwa wakati ningewaelewa.

Lakini wengi hawalipi na wanaolipwa wanakaa mamiezi bila malipo halafu mkipata mnaenda kutanua mimi siwaelewi.
Hamna tofauti na yule jamaa anaenunua ndege wakati wanafunzi hawajalipwa fedha za kujikimu wamegeuka makahaba na vibenten kama watumishi wenu
It is shame

Anayoyafanya Mbowe yatatunyima uhalali wa kuikosoa serikali bila kunyooshewa kidole
Opposition was meant to be the best option.. a model.. yaani kioo cha kukitazama serikali na chama tawala.
 
..wananchi hawapaswi kujiona WANYONGE.

..wakishajiona wanyonge kisaikolojia watajisalimisha kwa viongozi na kuvumilia uzembe na hata ukatili wa viongozi waliowachagua.

..waTz tuna tatizo la KUOMBA badala ya KUDAI haki na mahitaji yetu toka kwa viongozi.

..chanzo chake ni viongozi kwa muda mrefu kuwaita wanancho wanyonge mpaka imefika mahali sasa wananchi wanaamini wao ni wanyonge na wanastahili huruma.
 
Alizaliwa Holi la ngombe sio kwa sababu pesa walikuwa hawana Bali nyumba ya wageni ilikuwa imejaa .Kasome Biblia Tena sababu ya Yesu kuzaliwa holini haikuwa sababu ya kuwa wazazi wake walikuwa maskini


Siyo kweli, Yesu alizaliwa kwenye hali Duni kwa sababu maalumu, na ndo maisha yake yote aliishi kama mtu wa kawaida na maisha Duni asiyependa makuu, aliishi na masikini, yule ni Mungu iweje ashindwe kutatua tatizo dogo kama hilo la kukosa nafasi kama alitaka kuzaliwa kwenye Hekalu kama Mfalme?
 
Katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Chama, M/Kiti Mbowe amenukuliwa akisema kuwa "Sera ya CHADEMA ni kuchukia umaskini na kila mwanachama awe na nia hiyo". Yawezekana ikawa dhamira sahihi lakini isiyokuwa na mikakati ya kuondokana na umaskini.

Nalisema hilo kwa sababu, kwa nyakati tofauti, viongozi wote wa chama wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba mikakati ya kiuchumi ya Serikali ya CCM ni ya vitu na si watu.

INAFIKIRISHA kuamini kilichomo kwenye Sera hiyo ya CHADEMA.

Fumbo mfumbie mjinga ...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Siyo kweli, Yesu alizaliwa kwenye hali Duni kwa sababu maalumu, na ndo maisha yake yote aliishi kama mtu Duni asiyependa makuu, aliishi na masikini, yule Mungu iweje ashindwe kutatua tatizo dogo kama hilo la kukosa nafasi kama alitaka kuzaliwa kwenye Hekalu kama Mfalme?
Lete ushahidi Kama Yesu alizaliwa na kukulia Hali duni .Yesu hajawahi zaliwa duni akiwa mtoto mchanga aliletewa zawadi dhahabu na mamajusi .Alianza kumiliki dhahabu akiwa mtoto mchanga.
 
Lete ushahidi Kama alizaliwa na kukulia Hali duni .Yesu hajawahi zaliwa duni akiwa mtoto mchanga aliletewa dhahabu na mamajusi .Alianza kumiliki dhahabu akiwa mtoto mchanga

Kama Yesu alizaliwa na kuishi kitajiri basi inabadilisha kila kitu ninachokifahamu na nilichowahi kufundishwa na kukisikia kuhusu yeye, alichokisimamia na alichokifundisha, hata hivyo mimi siyo Mwanatheolojia ila kwangu nilifikiri ilikuwa ni lazima azaliwe kwenye hali Duni tumwamini, sijui lkn mimi siyo Mtaalamu wa Biblia.
 
Kama Yesu alizaliwa na kuishi kitajiri basi inabadilisha kila kitu ninachokifahamu na nilichowahi kufundishwa na kukisikia kuhusu yeye, alichokisimamia na alichokifundisha, hata hivyo mimi siyo Mwanatheolojia ila kwangu nilifikiri ilikuwa ni lazima azaliwe kwenye hali Duni tumwamini, sijui lkn mimi siyo Mtaalamu wa Biblia.
Kukusaidia tu Yesu alilisha maelfu bure .Lofa hawezi kulisha watu maelfu Kama Yesu alivyofanya.Anayekuambia Yesu alikuwa maskini mwongo mkubwa
 
Kukusaidia tu Yesu alilisha maelfu bure .Lofa hawezi kulisha watu maelfu Kama Yesu alivyofanya.Anayekuambia Yesu alikuwa maskini mwongo mkubwa


Lkn sidhani kama alilisha kwa kununua chakula nafikiri alifanya miujiza kama wavuvi kupata samaki wengi n.k. Isitoshe kama Yesu alizaliwa kwenye Utajiri, huo utajiri ukitokea wapi kwani Baba yake Josefu alikuwa ni Seremala na siyo Mfalme, sasa huo Utajiri ulitokea wapi?
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom