Mbowe: CHADEMA tunaamini kwamba umaskini ni laana na kila mwanachadema ni tajiri rohoni mwake

Umeongea kweli tupu!
Maisha ya yesu yalikuwa yakawaida sana, ndo maana walimdharau aliishi maisha ya chini ili awaokoe wanadamu sasa mbowe anasema umaskini nilaana wakati yesu anesema nivigimu tajiri kuingia ufalme wa mbingu bali nirahisi ngamia kupenya tundu la sindano. Ndo maana anatumbua pesa za wanachama wa chadema maskini wanaofanya kazi kwa malipo ya furana na bila ofice hafu unawaambia umaskini ni raana dharau kuu kabisa
 
Lkn siyo kosa kuzaliwa masikini, kwani hauchagui pa kuzaliwa wala wa kukuzaa.
Sawa lakini usifurahie umaskini ukisha kuwa na akili. Pambana ili na wewe usizae mtoto katika hali uliyozaliwa wewe, maana utakuwa umeshaona madhara ya kuzaliwa katika familia maskini.
 
..Mwalimu NYERERE alisema Tz ina MAADUI watatu ambao wanapaswa kupigwa VITA, na moja ya maadui hao ni UMASIKINI.

..Katika suala hili Mzee Mbowe anafuata wasia aliotuachia Baba wa Taifa kwamba tukatae na tuupige vita umasikini.
Hivi CCM ya Nyerere ilifia wapi? Maana ile CCM ya Nyerere ilisema kabisa kwamba UMASKINI ni adui hatari tena ni wa kupambana naye kwa nguvu zote. Ila CCM ya Chato inakumbatia umaskini ili iwe inatembea na hela mfukoni na kuwagawia watu barabarani. Kwa nini usiweke mazingira mazuri ya mtu kutafuta hela yake kuliko hii ya kupewa barabarani?
 
Sawa lakini usifurahie umaskini ukisha kuwa na akili. Pambana ili na wewe usizae mtoto katika hali uliyozaliwa wewe, maana utakuwa umeshaona madhara ya kuzaliwa katika familia maskini.


Siyo rahisi kihivyo kwa kila mtu, mtoto wa Mtaani ana chance gani ya kupambana katika mazingira haya? Kuna watu Dunia inawapa mazingira magumu na hawawezi kuchomoa peke yao na siyo kosa lao, fikiria kijana miaka 13 ana wadogo zake 4, Wazazi wameshafariki ni yatima ana chance gani za kupambana?
 
Eti wanachama wanahoji kwanini chama kimeenda kutumia mamilioni ya fedha kukodi ukumbi wa Mliman City na kuacha kumbi nyingine za bei nafuu halafu Mbowe anajibu kwamba CHADEMA ni watu wa viwango na wanachukia umasikini halafu watu wanashangilia.

Iko wapi tofauti kati ya Magufuli anayenunua ndege na Mbowe anayepeleka Kamati kuu pale Mlimani City kwenye ukumbi wa mamilioni?

Ndege zinaponunuliwa watu wanahoji kwamba zina faida gani kwa mwananchi wa hali ya chini ambaye hana uwezo wa kupanda ndege?

Sasa na mimi nataka kuhoji kwamba kufanyia Mkutano pale Mlimani City kwenye Ukumbi wa mamilioni kuna faida gani kwa mwana CHADEMA wa kawaida au kiongozi wa CHADEMA kwenye ngazi ya shina au tawi ambaye siyo Mjumbe wa kamati kuu? Hivi haya mamilioni si yangeweza kuwajengea ofisi ya Chama hawa viongozi wa mashina na Matawi katika kata zao? Hivi hayo mamilioni yangeweza kujenga ofisi ngapi za Wilaya au Mkoa?

Yaani kweli chama kisicho na ofisi kinaenda kukodi ukumbi wa Million 130 wakati hakina hata jengo moja la ofisi? Yaani chama kinakodi ndege ya kuwapeleka kina Lema CCM Kirumba kwenye sherehe za Uhuru wakati chama hicho hicho hakina hata jengo moja la ofisi halafu wanachama wanashangilia tu kama Majuha?

Kweli nimeamini CHADEMA kuna wajinga na Malofa.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu comment yako hii nikama nakuona, mimi nilishangaa yaliposhangiria!!!! Baadae nilikasirika sana wanachadema wanadai kuwa ndege za air tanzania hazina faida huku yenyewe yanatafuna fedha kwa anasa !! Nimeambiwa T-shirt zimecost sh. 89ml. Ukumbi na huduma zte 240ml. Ndege ya kwenda mwanza kikundi cha watu wachache 76ml. Harafu watu wanashangiria!! Nikweli Majuha.
 
Angaria uchaguzi. 1.mwenyeiti na makam wake madume yte + katibu mkuu na makamu wao wote madume+ hivi chadema hakuna wanawake ??? Wanaotaka nao kula rudhuku? Kwenda mwanza napo mlienda wenyewe tu na ndege kwapesa zachama , jamani hao wanawake mlio nao ndani ya chama kazi yao niipi?. Amkeni wanachadema mnaibiwa..
 
Siyo rahisi kihivyo kwa kila mtu, mtoto wa Mtaani ana chance gani ya kupambana katika mazingira haya? Kuna watu Dunia inawapa mazingira magumu na hawawezi kuchomoa peke yao na siyo kosa lao, fikiria kijana miaka 13 ana wadogo zake 4, Wazazi wameshafariki ni yatima ana chance gani za kupambana?
Sasa katika hali hii ya kusikitisha wewe mwenyewe umethibitisha madhara ya umaskini. Sasa kwa nini chama chetu hakipambani na huyu adui na badala yake kinafurahia umaskini?
 
Duuh kweli hapa ndo ule msemo wa ujuzi hauzeeki unaonekana.. yan Maneno hayo Ni dhahiri kabisa yanafanana na Ya DJ na Mbowe Ni DJ by professional..

Juzi tu hapa alisema Tanzania Ina raia masikini wasio weza kumudu gharama za ndege kwahiyo ndege siyo kipaumbele Cha wananchi.
Harafu leo tu Anataka kutuaminisha kuwa Watanzania Ni matajiri.

Daaah Kwa akili hizi CCM itaendelea kubaki madarakani kwa miaka mingi Sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbona Mzee wako anasema kila siku kuwa Tanzania ni tajiri na inapaswa kukopesha wengine?
 
Angaria uchaguzi. 1.mwenyeiti na makam wake madume yte + katibu mkuu na makamu wao wote madume+ hivi chadema hakuna wanawake ??? Wanaotaka nao kula rudhuku? Kwenda mwanza napo mlienda wenyewe tu na ndege kwapesa zachama , jamani hao wanawake mlio nao ndani ya chama kazi yao niipi?. Amkeni wanachadema mnaibiwa..
Kwanza tutajiie safu ya uongozi ya CCM Tafa ndipo tuendelee na mjadala. Anza na mwenyekiti, makamu mwenyekiti, Katibu Mkuu, Jumuiya ya wazazi na ya vijana,
 
Mkuu comment yako hii nikama nakuona, mimi nilishangaa yaliposhangiria!!!! Baadae nilikasirika sana wanachadema wanadai kuwa ndege za air tanzania hazina faida huku yenyewe yanatafuna fedha kwa anasa !! Nimeambiwa T-shirt zimecost sh. 89ml. Ukumbi na huduma zte 240ml. Ndege ya kwenda mwanza kikundi cha watu wachache 76ml. Harafu watu wanashangiria!! Nikweli Majuha.
Kwani CCM haipati ruzuku? Mbona hamhoji matumizi yake?
 
Kama sisi tunavyomshangaa mbowe anataka wanachama wake wawe na mawazo ya kitajiri wakati hata banda la kuku tu la makao makuu ya chama ameshindwa kujenga.

Sent using Jamii Forums mobile app
Sasa ulitaka kwa vile tu hawajajenga ofisi nzuri aseme umaskini ni mzuri? Kwa hiyo wewe kabla hujajenga nyumba utaendelea kusema nyumba siyo kitu? Unatakiwa useme kweli na ukubali uzuri wa kitu hata kama huna kwa wakati huo. Ninyi ndio huwa hamsomeshi watoto wenu kisa eti wewe hukusoma.
 
Kumbe yale aliyoyasema Lema ndio sera ya CHADEMA?


Laana ipi hiyo? kama ile iliyozungumziwa kwenye biblia.... Jeremiah 26:2-6


haya na mengine ni kati ya mafundisho waliyopata kutoka kwa Mabeberu.?
 
..wananchi hawapaswi kujiona WANYONGE.

..wakishajiona wanyonge kisaikolojia watajisalimisha kwa viongozi na kuvumilia uzembe na hata ukatili wa viongozi waliowachagua.

..waTz tuna tatizo la KUOMBA badala ya KUDAI haki na mahitaji yetu toka kwa viongozi.

..chanzo chake ni viongozi kwa muda mrefu kuwaita wanancho wanyonge mpaka imefika mahali sasa wananchi wanaamini wao ni wanyonge na wanastahili huruma.

Katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Chama, M/Kiti Mbowe amenukuliwa akisema kuwa "Sera ya CHADEMA ni kuchukia umaskini na kila mwanachama awe na nia hiyo". Yawezekana ikawa dhamira sahihi lakini isiyokuwa na mikakati ya kuondokana na umaskini.

Nalisema hilo kwa sababu, kwa nyakati tofauti, viongozi wote wa chama wamekuwa wakitoa maoni yao kwamba mikakati ya kiuchumi ya Serikali ya CCM ni ya vitu na si watu.

INAFIKIRISHA kuamini kilichomo kwenye Sera hiyo ya CHADEMA.

Fumbo mfumbie mjinga ...

Sent using Jamii Forums mobile app

sera zao ni zipi sasa?

Huwa sitishwi na slogan za wahuni wanaotumia maneno ya mvuto kuwakamata wapumbavu.

Najua ili uwe tajiri. Fanyakazi
Hakuna hiyo sera ya Utajirisho wa roho. Kama angekuwa nayo angeanzia alizonazo kuwapa wasio na kitu, lkn ndio nakopesha cdm na kujipa baadae, so what?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hawa juu walitoa michango yao.....wasome kwa taarifa....tafakari
 
Back
Top Bottom