Mbowe: CHADEMA ilianzishwa na watu waliopinga ukandamizwaji kiuchumi na kijamii

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,858
2,000
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema yeye na wenzake walianzisha chama hicho ili kupinga sera za ujamaa na kujitegemea zinazotumiwa na Chama cha Mapinduzi.

Akizungumza katika mwendelezo wa mahojiano yanayoitwa ‘Speaking with Tundu Lissu’ yaliyorushwa na Podcast ya Nadj Khamis, Mbowe amesema chama hicho kilianzishwa na watu wenye mtazamo wa soko huria waliopinga ukandamizwaji kiuchumi na kijamii uliokuwa umeshika kasi.

Alisema vuguvugu la mabadiliko lilikuja wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, aliyerejesha uhuru wa kibiashara na hivyo watu wakatamani kuwa na mabadiliko kwenye nyanja ya kisiasa.

“Wakati biashara zimeruhusiwa kukawa na vuguvugu la kisiasa. Kukawa na harakati za kina Mzee Fundikira (Abdallah), harakati za Mzee Mapalala (James), kule Chuo kikuu, harakati za kina Marando (Mabere) na wengineo,” alianza kueleza Mbowe, ambaye kwa muda mrefu sasa amekuwa kinara kwenye siasa za Tanzania.

Ametaja makundi matatu ya mageuzi yaliyoibuka kuwa pamoja na kundi la wasomi na waliofanya kazi serikalini, akiwataja aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, Edwin Mtei, aliyewahi kuwa Naibu Gavana, Bob Makani na wengineo.

“Kundi la pili lilikuwa na wafanyabiashara ambao waliona kasi za kufanya baishara haziendani na sera za ujamaa. Kwa hiyo tulitaka kujadili sera za uchumi wa soko. Kundi la tatu lilikuwa ni la wasomi wazuri, wengine wako vyuoni, mashirika ya umma na serikalini,” alisema.

Alisema katika kundi la kwanza ndilo lililoanzisha Chadema na walimwomba Mzee Mtei kuwa Mwenyekiti wake mwaka 1991.

“Baadaye ile sheria ya vyama vingi ikapitishwa Julai 1992, wakati huo tumeshaanza kukutana. Wengi walioanzisha Chadema walikuwa watu wazima,” alisema.

“Kwa hiyo sisi tulianzisha chama tukiwa na clear policy (sera mahsusi) tunataka nini. Tulikuwa kabisa hatutaki siasa ya ujamaa. Waasisi wengine walirudi CCM, lakini kilichotuunganisha sisi tulikuwa hatukubali sera za kijamaa.

“Kwa upande mwingine, vyama vingi vilivyoanzishwa vilikuwa na sera za kijamaa, ikiwamo NCCR -Mageuzi. Ila walikuwa wanatofautiana na CCM ilikuwa ni utekelezaji wa sera,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 

Elitwege

JF-Expert Member
Jun 4, 2017
4,127
2,000
Hivi karibuni imezuka tabia ya kukwepa majukumu ambayo inapaswa kupingwa kwa hali na mali ndani ya nchi yetu.

Vyama vya upinzani hasa Chadema kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati rais Magufuli.

Chadema wamesambaza mitandaoni vijana wa kumtetea Mbowe.

Kazi yao ni kuwapumbaza wanachama na wananchi kwa ujumla waone tatizo la chadema ni Magufuli wakati Magufuli hayupo na hakuwahi kuongoza chadema. Kila uzi humu JamiiForumS lazima vijana wa Mbowe wataje na kutukana mwendazake!

Mwenyekiti na aliyekabidhiwa usukani wa kuiongoza Chadema ni Mbowe lakini hawataki aulizwe chochote!

Kutokana na Chadema kufa kila mahali kwa kupoteza mvuto na kukimbiwa na madiwani na wabunge ,viongozi wamebuni mbinu ya kukwepa aibu hii kwa kujificha kwa hayati rais Magufuli!

Viongozi wa Chadema wakihojiwa kwa nini chama hakina ofisi watakujibu tatizo ni Magufuli.

Tundu Lisu akiulizwa kuwa yeye ni makamu mwenyekiti wa Chadema lakini kwa nini hafanyi kazi za Chadema? Bavichaa watakujibu chanzo ni Magufuli!

Bavicha ukiwauliza kwa nini kamati kuu ya Chadema wanafanyia vikao vyao kwenye hoteli za kitalii na kuacha ukumbi wa ufipa ? Utajibiwa tatizo ni hayati Magufuli!

Chadema wakiulizwa kwa nini kwenye uchaguzi mliwatosa makada wenu waliokipigania chama, mkabadili gia angani na kutuletea mgombea urais ambaye yupo kwenye list of shame (orodha ya chadema ya mafisadi wakuu wa nchi)?
Utajibiwa tatizo ni mwendazake!

Bavicha na vijana wote mliosambazwa mitandaoni kumtetea Mbowe, tambueni anayepaswa kuulizwa kuhusiana na mabaya na mazuri ya Chadema ni Mbowe na Tundu Lissu hao ndio viongozi wenu mliowapa ridhaa ya kuwaongoza kwa sasa.

Hayati Rais Magufuli hakuwahi kuwa kiongozi wa chadema, hivyo kukaa mnamhusisha na kuporomoka kwa chama chenu ni kupoteza muda na kuonyesha uzwazwa wa hali ya juu.

Kuporomoka kwa CCM wataulizwa SAMIA na Dr Nchongolo na lazima watoe majibu kwa sababu wao ndiyo viongozi wa ccm kwa sasa.
Kwa nini nyinyi hamtaki kupata majibu kwa Mbowe badala yake mnataka majibu yatoke kwa Magufuli.
 

hydroxo

JF-Expert Member
Oct 19, 2015
1,680
2,000
Alisema vuguvugu la mabadiliko lilikuja wakati wa utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, aliyerejesha uhuru wa kibiashara na hivyo watu wakatamani kuwa na mabad
Tuseme ukweli tu.

Waislamu wakitawala kunakuwepo na uhuru wa kutosha wa biashara na mambo mengine.

Ila upande wa pili sasa wakiwa wao balaa tupu.

Alichotufanyia mwendazake ni somo tosha.
 

imhotep

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
29,972
2,000
Magufuli alikuwa muuaji na muharibifu WA kila aina ikiwa hukubaliani na hilo jinhonge.

Sasahivi ananuka huko aliko alijua atabakia maisha katika dunia hii baada ya kuona ana kila aina ya ulinzi.
😂😂😂🤣🤣
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
47,024
2,000
Ngoja tuone!

Ni kweli Chadema iliasisiwa na mabwanyenye akina Mtei, Bob Makani, Tuntemeke Sanga, Mwaikambo nk. nk!
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Magufuli alikuwa muuaji na muharibifu WA kila aina ikiwa hukubaliani na hilo jinhonge.

Sasahivi ananuka huko aliko alijua atabakia maisha katika dunia hii baada ya kuona ana kila aina ya ulinzi.
kifo cha magufuli ni pigo kubwa kwa waovu wengi waliokuwa wanamshabikia. halafu kilikuwa ghafla Ili Mungu kutulipa Machozi yetu.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
CHADEMA, Sera na misimamo ya chama hichi imenifanya nifuatilie sana siasa, CDM kitabaki pasua kichwa kwa CCM wakati wote, wanakuja vibaraka, mapandikizi na kila aina ya wachawi wanajaribu kukifuta ila wanafutika wao, Salute Kamanda Mbowe.
Kwa ufipi Chadema imepaMbana na Dola na Jeshi na bado ipo hai. Hilo chama kina nguvu za ajabu sana.
 

Mr Dudumizi

JF-Expert Member
Sep 9, 2020
1,234
2,000
Ukiona mgonjwa wako anaongea kila mara bila break ujue anakaribia kufa. Huyu mwenyekiti hakuwa muongeaji ongeaji, sasa sijui kimempata nini mpk kaanza kuwa msemaji wa chama na sio mwenyekiti tena.

Huenda amesha notes kuwa chama kinaelekea kumfia mikononi, kutokana na wanachama wengi wakiwemo viongozi kadhaa kuonesha wazi wazi kuunga mkono uongozi wa bimkubwa.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Hivi karibuni imezuka tabia ya kukwepa majukumu ambayo inapaswa kupingwa kwa hali na mali ndani ya nchi yetu.

Vyama vya upinzani hasa Chadema kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati rais Magufuli.
Tunashukuru yuko kuzimu anaoza analipa madhambi aliyofanya. Haya mengine ni porojo tu.
 

Pythagoras

JF-Expert Member
Feb 24, 2015
17,376
2,000
Ukiona mgonjwa wako anaongea kila mara bila break ujue anakaribia kufa. Huyu mwenyekiti hakuwa muongeaji ongeaji, sasa sijui kimempata nini mpk kaanza kuwa msemaji wa chama na sio mwenyekiti tena. Huenda amesha notes kuwa chama kinaelekea kumfia mikononi, kutokana na wanachama wengi wakiwemo viongozi kadhaa kuonesha wazi wazi kuunga mkono uongozi wa bimkubwa.
Kama alivyokuwa anaongea magu akafa kwa aibu na fedheha
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,584
2,000
Tuseme ukweli tu.

Waislamu wakitawala kunakuwepo na uhuru wa kutosha wa biashara na mambo mengine.

Ila upande wa pili sasa wakiwa wao balaa tupu.

Alichotufanyia mwendazake ni somo tosha.
Pana ukweli kwenye udadavuzi wako.

Mama atakuwa kakomelea pointi yako na nyundo akiweka pia mazingira ya kupatikana kwa katiba mpya katika kipindi chake.

Mola akampe ujasiri.
 

secret file

JF-Expert Member
Sep 10, 2019
5,206
2,000
Magufuli alikuwa muuaji na muharibifu WA kila aina ikiwa hukubaliani na hilo jinhonge.

Sasahivi ananuka huko aliko alijua atabakia maisha katika dunia hii baada ya kuona ana kila aina ya ulinzi.
Aisee kweli atakuwa alikuharibu vibaya huyu
 

brazaj

JF-Expert Member
Jul 26, 2016
12,584
2,000
Hivi karibuni imezuka tabia ya kukwepa majukumu ambayo inapaswa kupingwa kwa hali na mali ndani ya nchi yetu.

Vyama vya upinzani hasa Chadema kila wanapopata matatizo kisingizio chao ni hayati rais Magufuli!....
Poleni sana wafiwa. Kufiwa na mzazi haijawahi mwaacha mtu bila msongo wa mawazo.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom