Mbowe: CHADEMA hatutaki Ruzuku kwani ni utumwa kwa vyama vya siasa nchini

kweli ruzuku watatumia kulipana posho na kujaza magari mafuta,aache unafiki kwa nini wasiandike barua kwa tendwa aisitishe hyo ruzuku tuone
 
Hatutaki hiyo ruzuku ya kitumwa...
Changia chama kupitia namba hizi
1. M-Pesa (0757755333 na 0763744334)
2.Tigo Pesa (0655783333) and
3.Airtel Money (0684425222)

Namba hizi kazisoma Mh. Mbowe mwenyewe hapa Leganga.
 
Ruzuku kwa vyama vya siasa ni stahili na haki yao sio fadhila kwa vile inatokana na kodi inayolipwa. Nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea hutoa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa. Nchi nyingi za ukanda wa Scandinavia hutoa ruzuku kubwa zaidi kwa vyama vichanga vya siasa ili vipevuke na kukomaa ili kuongeza wigo wa demokrasia. Kwa hiyo Chadema kuchukua ruzuku ni stahili na haki ila wanachama wanaweza kuchangia zaidi ili kupanua uwezo wa kuendeleza shughuli za chama. Siafiki ruzuku hiyo kuachwa hata kama inapatikana kwa judo.
 
kwa sasa ruzuku zipo kisheria chadema hawawezi kuzikataa na Mbowe hajasema eti ni msimamo wa chama ila amesema ruzuku sio nzuri.

Mbona napata kizunguzungu! Siyo kwamba Mbowe amesema CDM imekataa ruzuku? Yaani kasema siyo nzuri halafu basi hivyo tu? Kitu siyo kizuri si unakikataa? Nakaribia kufuta kauli yangu ya hapo juu.
 
Ruzuku kwa vyama vya siasa ni stahili na haki yao sio fadhila kwa vile inatokana na kodi inayolipwa. Nchi nyingi zilizoendelea na zinazoendelea hutoa ruzuku kwa vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa. Nchi nyingi za ukanda wa Scandinavia hutoa ruzuku kubwa zaidi kwa vyama vichanga vya siasa ili vipevuke na kukomaa ili kuongeza wigo wa demokrasia. Kwa hiyo Chadema kuchukua ruzuku ni stahili na haki ila wanachama wanaweza kuchangia zaidi ili kupanua uwezo wa kuendeleza shughuli za chama. Siafiki ruzuku hiyo kuachwa hata kama inapatikana kwa judo.
Mkuu kwa nchi zetu hizi ruzuku ni janga. Watu wanaunda vyama na kuvifanya kama vitega uchumi vyao kwa kujipatia ruzuku. Ukombozi wa kweli utapatikana kwa watu kujitolea kama ambavyo watu walikuwa wakitolea hadi thumuni wakati wa vuguvugu za uhuru. Ningefurahi kama vyama vingekataa ruzuku na kurudi kwa wanachama kuchangia vyama vyao. Hii ingeonyesha committment ya wanachama kwa vyama vyao.
 
Mmmmmmmmm, niwazo zuri sana na nnawapongeza sana chadema ila wasiwasi wangu ni je wataweza kukiendesha kweli chma bila ruzuku kweli?????????!!!!!!!!!!!!

automatically Tendwa atakua hana kazi tena ya kujifanya auditor wa vyama!

Hapo safi sana mnajitofautisha na CCM ambao wanaombaomba hadi kwa David Cameron na kupewa masharti magumu kinyume na maumbile yetu. Good start mkichukua nchi mtaifanya ijitegemee fasta kwa kutumia rasilimali zetu

Dovutwa ataishije?

Hatutaki hiyo ruzuku ya kitumwa...
Changia chama kupitia namba hizi
1. M-Pesa (0757755333 na 0763744334)
2.Tigo Pesa (0655783333) and
3.Airtel Money (0684425222)

Namba hizi kazisoma Mh. Mbowe mwenyewe hapa Leganga.

Inaelekea kuna watu hawajaielewa hii taarifa hii kabisa
Mbowe hajasema hawataki ruzuku, HAPANA
Alichosema Mbowe ni kwamba CDM haita tumia fedha ya ruzuku kugharamia uchaguzi
Hii ikiwa na maana ruzuku itatumika kwa kulipana posho za vikao,safari,mafuta na shughuli za kiofisi tu lakini si kuzitumia kwenye uchaguzi
 
Information kama hii inatakiwa itolewe na Verified user kama vile Mnyika ama Dr. Slaa na siyo mtu awaye yote kwani mwishowe tunaweza kuishia kutumbukiza pesa mifukoni mwa wajanja wachache!
 
japo chadema naipenda lakini kwa hapo watanifanya niwe mzalendo wa chadema....
 
Inaelekea kuna watu hawajaielewa hii taarifa hii kabisa
Mbowe hajasema hawataki ruzuku, HAPANA
Alichosema Mbowe ni kwamba CDM haita tumia fedha ya ruzuku kugharamia uchaguzi
Hii ikiwa na maana ruzuku itatumika kwa kulipana posho za vikao,safari,mafuta na shughuli za kiofisi tu lakini si kuzitumia kwenye uchaguzi

Aaaaaah kuuumbe! Nilikuwa nimefurahi kwamba kwa mara ya kwanza nimepata chama sahihi ambacho kitajengwa kwa thumuni na shilingi za wanachama badala ya hili janga la ruzuku.
 
Ninawasiwasi na mtoa mada kama amesikia vizur! Kuacha kuchukua ruzuku na kutegemea michango tu ya wananchi 100%, watu wenyewe watz, maneno mengi vitendo vichache, tukianzia wana cdm wa humu humu jf, ukipitisha bakur kwa kila mtu, lazima kuna watu wataanza visingizio kibao na kutafuta sababu, NI WAZO ZURI ila kwa tanzania, na cdm kilivyo chama kikubwa na cost za kuendeshea chama ni kubwa, nina wasiwasi na sijui kama cdm ikianzisha mfumo huu kama hakitakufa kwa kukosa hela za kutosa. LABDA IWE "KUACHA KUTEGEMEA RUZUKU" NA SIO "KUACHA KUCHUKUA RUZUKU".
 
Information kama hii inatakiwa itolewe na Verified user kama vile Mnyika ama Dr. Slaa na siyo mtu awaye yote kwani mwishowe tunaweza kuishia kutumbukiza pesa mifukoni mwa wajanja wachache!

Meku nilikuwako wakati anazisoma hizi namba leo, wewe verify before kutuma pesa. Plus kesho nitaweka video hapa, au weza ukatafuta matangazo walorusha star tv live utazisikia. hakuna mtu anataka kukuibia kirahisi hivo.
 
Nyerere ALITETEA uhuru wa watanzania si kwa ruzuku bali ni kwa michango ya watanzania masikin wa vijijin.... Ndio akatuletea Uhuru tunaojivunia leo...Chadema naamin njia hii wakiitumia itakuwa ukombozi mwingine wa kifikra kwa watanzania,,,, Mwananchi atakayetoa mchango wake kukichangia chama atashindwaje kulinda kura yake? Shilingi 500 ya mtanzania masikini ni milion kumi ya fisadi.... Tumeanza na Mungu tutamaliza na Mungu....
 
Swala la ruzuku hili litakuwa pigo lingine kwa ccm .... Maana ishu ya posho wamejifanya kulipangua kwa kukubali kuzifuta.... Haya na ruzuku je? Magamba kazi mnayooo.... Na hapo mafisadi ndipo watakapokiteka chama... Maana wataitaji kuwatumia hao ili waendeleze tabia zao za rushwa... Usishangae wakapotezea hii hoja kwa kutoongea chochote kuhusu ruzuku... Viombo vya habari tunawategemeen kuamsha hoja hii ya ruzuku.... Au kama vipi vyama viwe vinakopenshwa kama wanafunzi wa vyuo vikuu.... Mbona kilimo mlifuta ruzuku?
 
Wana JF CDM walichokifanya Leo ni hususani hili lakuchangia Kampeni ni Kitu cha kutia faraja,sasa Ukombozi utakuja,Kuna watu tena wana CCM wanapesa zao nyingi sana ila wanaogopa kuchangia Chadema Kuogopa kuambiwa watakuwa wanasaliti chama chao,sasa kwa njia Hii tunawaomba wafanye kuichangia Chadema Kwa Njia ya M-PESA,AIRTEL MONEY,na TIGO PESA,Kwa kufanya hivi tutaikomboa Nchi yetu kutoka kwa Magamba.

LINGINE KUBWA NAWASIFU WAMILIKI WA STARTV KUKUBALI KULUSHA MATANGAZO YA MOJA KWA MOJA YA CDM KWASABABU SIO KAWAIDA YENU,NAKUMBUKA KIPINDI CHA UCHAGUZI 2010 MLIKATAA KABISA KUPOKEA MATANGAZO YA CHADEMA,LAKINI SASA MMEJUA DEMOKRASIA YA KWELI,TUNAOMBA MUENDELEE HIVI NA SIKU YA KUFUNGA KAPENI ZA KIJANA WETU MJE ARUMERU TENA KURUSHA,PESA SI TATIZO CHADEMA TUMEAMUA KUCHANGIA CHAMA CHETU KWA HIYO TUTAWALIPA TUUU KAMA TULIVYO FANYA.

!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Huku ni kuwamilikisha wanachama chao siyo kama wanavyosema "CCM in wenyewe" na wenyewe ni mafisadi
 
Kelele nyingi subiri kwenye matumizi ndio utajua wachagga wanajua pesa au wameru?
 
Back
Top Bottom