Kamanda Francis
JF-Expert Member
- Nov 30, 2013
- 834
- 140
Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ambaye pia ni Kiongozi Wa Kambi rasmi ya Upinzani Bungeni na Mbunge Wa Jimbo la Hai Mkoani Kilimanjaro, akiwahutubia Wakazi zaidi ya Elfu Kumi na Mbili wa Jiji la Mwanza na Kanda ya Ziwa Magharibi Katika Uwanja wa Shule ya Msingi Nyamalango, Chuo Kikuu Cha SAUT Malimbe, Mh. Mbowe aliwakumbusha Watanzania Kote Nchini Kuwa, Kitendo cha CCM Kukosa Mbinu za Kumnunua ili aimalize Chadema Kama Walivyofanya Kwa Baadhi ya Watu ndani ya Chama Kinazidi Kuwaumizia Akili na Kuwafanya Wazidi Kukata tamaa Kila Kukicha.
Hapa anasema "Ndg. zangu Makamanda, napenda Kuwadhibitishia Kwamba Mbowe hafiki bei na Mbowe hanunuliki Kwa Bei yoyote, Kitendo cha Mbowe Kutofika Bei Kinawaumizi akili na Kuwafanya Waendelee Kukata tamaa Kila Kukicha, Isipokuwa anayefika Bei yao aende huko Kwetu ni aibu Kuwa naye ndani ya Taasisi hii ya Umma Watanzania, Safari hii Ilianza Zamani Kabla yetu Sote, hivyo Wapo Watakaopanda na Wapo Watakaoshuka Kwa Sababu tofauti tofauti, Kilichopo hivi sasa ni Kuufikia Mwisho Wake"
---------------------------
[h=2]Dr Slaa hanunuliki kwa Gharama yoyote - Mbowe[/h]

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa Freeman Mbowe ametoa siri nzito inayohusiana na Katibu Mkuu wake Dr Wilbroad Slaa ambaye ni kati ya wanasiasa wenye mvuto mkubwa nchini.
Akizungumza na wanafunzi wa vyuo vikuu DSM na Mwanza kiongozi huyo alisema wanachama wa CHADEMA walipomuomba kuwa Mwenyekiti wa chama hicho mwaka 2004 alitoa masharti mazito ili kukubali nafasi hiyo.
Moja ya Masharti aliyotoa ni kwamba Dr Wilbroad Slaa akubali kuwa Katibu Mkuu wa CHADEMA.Mbowe alisema alikubali kuwa Kiongozi mkuu wa chama hicho baada ya sharti hilo kukubalika.
Pia Mbowe akizungumza katika mkutano wa hadhara Mwanza Jumapili alisema CCM wanatapatapa kwa sababu hawawezi kumtenganisha na Katibu Mkuu wake kutokana na Ukweli kwamba Dr Slaa hanunuliki kwa gharama yoyote.
Itakumbukwa mwaka jana mchambuzi mmoja wa maswala ya kisiasa aliandika Makala yake inayosema Ushirika wa Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa ni 'THE BEST COMBINATION EVER' kutokana na mafanikio makubwa walichokipatia chama hicho.