Mbowe azuiliwa na Mahakama kwenda Marekani licha ya kuruhusiwa na Spika Ndugai

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,915
141,870
Mwenyekiti wa CHADEMA ambaye pia ni mfanyabiashara maarufu mh Freeman Mbowe amezuiliwa na mahakama ya Kisutu kwenda nchini Marekani, Uingereza na Uswisi kwenye shughuli zake za kibiashara.

Mkurugenzi wa uchaguzi CHADEMA John Mrema amesema Mbowe ambaye ni mbunge wa Hai amepewa ruhusa ya kusafiri na Spika wa bunge mh Ndugai lakini Hakimu Thomas Simba na mawakili wa Serikali wamemzuia kusafiri.

Mrema amesema zuio hilo la hakimu Simba ni kinyume kabisa na hukumu ya Mahakama Kuu kuhusu masharti ya dhamana na ni ukandamizwaji wa makusudi wa haki za binadamu.
 
Back
Top Bottom