Mbowe awashukia wabunge wa CCM

Watanzania

JF-Expert Member
Jul 7, 2009
727
42
Mbowe ajigamba adai atamwangamiza Malecela

*ASEMA AKIGOMBEA TU, ATAHAKIKISHA ANAMMALIZA

Na Geofrey Nyang'oro, Dodoma: Mwananchi

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza vita dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Malecela na wabunge wenzake waliokaa bungeni kwa muda mrefu.

Vita hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano wake wa Oparesheni Sangara uliofanyika wilayani Mpwapwa juzi.

Mbowe alisema kwa sasa umri wa Malecela kuendelea kuwa mbunge umekwisha na kwamba akisikia amechukua tena fomu kutetea nafasi hiyo mwaka huu atarusha helikopta katika kata zote za Jimbo hilo kuhakikisha anamng'oa.

"Mimi nazaliwa Malecela namsikia akiwa bungeni, nimesoma elimu ya msingi hadi sekondari, nimefanya kazi BoT, nimeacha kazi na sasa nafanya biashara, nimeingia kwenye siasa nimekwenda bungeni nimemkuta na nimemuacha, hivi huyu mtu amekuwa Sultani?,"alihoji Mbowe.

Alisema uwepo wa viongozi hao aliowaita masultani ndio unakokwamisha demokrasia nchini kwa kuwa hali hiyo ndiyo inayowajengea hofu wakazi wa Mkoa wa Dodoma.

Mbowe aliwataja wabunge wengine wa Mkoa wa Dodoma anaokamia kupambana nao mwaka huu kuwa ni Mbunge wa Mpwapwa, George Lubeleje na Mbunge wa Jimbo la Bahi, William Kusilla.
Mbowe ambaye alisafiri jana kwenda Muleba kuhudhuria maziko ya Balozi Christopher Ngaiza ambaye ni alikuwa kada wa chama chake, alitoa wito kwa wakazi wa Mpwapwa na vitongoji vyake kuacha ushabiki wa vyama badala yake wachague viongozi bora na wenye sifa ya kuongoza.

Kwa mujibu wa Mbowe, utamaduni wa kushabikia vyama umepitwa na wakati kwani vyama vimeundwa na binadamu tofauti na ardhi na watu wake ambao wameumbwa na Mungu.

Kuhusu kukithiri kwa umasikini, Mbowe alisema kumetokana na mfumo wa mbovu wa serikali inayoundwa na CCM.

Alisema mfumo huo umekumbatia mafisadi na kuchana dhana ya mwaasisi wa taifa hili, Mwalimu Julius Nyerere aliyesema chama hicho ni cha wakulima na wafanyakazi.

Alisema Tanzania haina sababu ya kuwa maskini kwa kuwa ina kila aina ya rasilimali ikiwmao madini, mbuga za wanyama na ardhi yenye ruruba.

Kuhusu elimu alisema kuwa ujenzi wa madarasa katika kila kata umechangia kudidimiza elimu hapa nchini kufuatia shule hizo kuwa na upungufu mkubwa wa walimu na vitendea kazi.

Hata hivyo, Mbowe aliwashambulia baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakijinadi kuwa ni makamanda wa kupambana na ufisadi kuwa wameonyesha kutokuwa na uwezo wa kupambana na ufisadi.

"Hoja ya mapambano dhidi ya ufisadi iliasisiwa na CHADEMA, nyinyi ni mashahidi namna wabunge wa Chadema walivyopambana , mara wakajitokeza wenzetu kutoka CCM, kina John Malecela na wenzake na kujinadi ni wapambanaji wa ufisadi, lakini tulijua ngoma hii hawaiwezi na kwamba wangeishia njiani,"alisema.

Tafakuri yangu: sehemu niliyoipenda zaidi katika habari hii ni hapo nilipokoleza wekundu. Wako wapi wabunge wa CCM sheria ya gharama za uchaguzi inapohaririwa nje ya kikao cha Bunge? Mpambanaji halisi bungeni ni yuleyule tangu pale Mwembe Yanga- Dr Slaa.
 
niko ukurasa mmoja na wewe mkuu....Dr.Slaa toka mwembe yanga alisema hayo yote na wakayapinga kwa nguvu zote na mwisho wa siku aibu ikaja kuwa yao.....
 
viva dk slaa,tuwasihi wananchi wa karatu waturudishie huyu mtu mwezi oct. aendelee kututumikia wtz.kwakweli tunahitaji watetezi kama hao sio maboya ya ccm kazi kuzinzia yakiamka usingizini ni kukgonga meza kama wehu

tchao
 
Age discrimination ni criminal offence DJ Mbowe committed.

Tumjaji Malecela kwa utendaji wake sio age. Malecela alikuwa msitari wa mbele kupambana na mafisadi na kuendeleza democrasia hapa nchini. Ni chini ya uongozi wake na Mwinyi waliruhusu vyama vingi.

Dj Mbowe tokea nazaliwa nakusikia unacheza disco baada ya wewe kufeli masomo, mwishowe ukaachiwa uenyekiti wa CHADEMA na mkweo, Madaraka uliyopowa kwa sababau ya kuowa mtoto wa Mtei huo ndio Usultani, tunataka democrasia ya kweli itisha uchaguzi chadema kama hupendi usultani or Uchagism.

Kama Malecela anachapa kazi yake inavyo takiwa na kachaguliwa kwa ridhaa ya wananchi usituletee ubaguzi wako wa kichaga na age

Itisha uchaguzi chadema kama hutaki usultani!!
 
- Freeman anaweza kuongelea usultani baada ya yeye mwenyewe na mkwe wake kumtia kitanzi Zitto, alipotaka Demokrasia anayoililia kutoka CCM ni maajabu ya Musa, kweli ukishangaa ya musa utaona ya firauni, yeye Demokrasia ameikataa kutoka kwa Wangwe lakini leo ana ubavu wa kulaumu CCM hili taifa na unafiki sijui ni nani ametuloga!

- Halafu vipi Ndesamburo na Dr. Slaa kwani hawa ni American Idol? Freeman alizaliwa na hawa?

Respect.

FMEs!
 
Age discrimination ni criminal offence DJ Mbowe committed.

Tumjaji Malecela kwa utendaji wake sio age. Malecela alikuwa msitari wa mbele kupambana na mafisadi na kuendeleza democrasia hapa nchini. Ni chini ya uongozi wake na Mwinyi waliruhusu vyama vingi.

Dj Mbowe tokea nazaliwa nakusikia unacheza disco baada ya wewe kufeli masomo, mwishowe ukaachiwa uenyekiti wa CHADEMA na mkweo, Madaraka uliyopowa kwa sababau ya kuowa mtoto wa Mtei huo ndio Usultani, tunataka democrasia ya kweli itisha uchaguzi chadema kama hupendi usultani or Uchagism.

Kama Malecela anachapa kazi yake inavyo takiwa na kachaguliwa kwa ridhaa ya wananchi usituletee ubaguzi wako wa kichaga na age

Itisha uchaguzi chadema kama hutaki usultani!!
Posti yako imekaaje tena? kwani lazima kuwa na jaziba ukitoa hoja. Nisaidie kujibu yafuatayo:
1.Kusema wazee wastaafu ni ubaguzi?
2.Unafahamu U-DJ unaajili watanzania wangapi hadi unawabagua?
3. Je unafahamu viongozi wa CCM wanaotoka familia moja walio kwenye uongozi
wa serikali achilia mbali kwenye chama chao?
4. Kwa nini unambagua Mbowe? kwani yeye katiba ya nchi haimruhusu
kuchaguliwa kuwa kiongozi?
5. Kwa nini unawabagua wachagga, wao si watanzania?
 
Naomba nikujibu namba 1 na 4 japo kwa kifupi

1.Ndiyo ni ubaguzi...Kwani ni wapi katiba inasema wazee wasigombee?

4.Kwa nini Malecela anabaguliwa na Mbowe?,kwani yeye katiba ya nchi haimruhusu kuchaguliwa kuwa kiongozi?
 
Unajua ni suala la busara tu. Watu kama akina Kingunge walitakiwa kung'atuka siku nyingi sana. Viongozi wenye busara hung'atuka mapema umri ukienda. Mifano ipo ya kutosha. Nitatoa mfano mmoja- Nelson Mandela.

Malecela hajabaguliwa na Mbowe bali ametumika kufikisha ujumbe kwa wazee kutumia hekima zao na kung'atuka. Lakini kumshambulia Mbowe na kabila la Wachagga ni ubaguzi mkubwa, Wachagga ni Watanzania kama wewe na mimi tulivyo.
 
-Nimesharudia katiba yetu ndiyo tatizo

-Mimi naona kosa analofanya Mbowe ni kupambana au kufanya harakati zake sasa zionekane anapambana na watu badala ya kupambana na Mfumo

-CHADEMA tujikite katika harakati za kitaasisi zaidi,hayo ndiyo yatakayoweza ku-reflect image ya mabadiliko ya kweli.Hatuwezi kuleta mabadiliko kwa kupambana na Mtu mmoja mmoja.So napinga moja kwa moja mapambano ya aina hii,nisichukuliwe kama Msaliti wa CHADEMA but the way forward should be aiming high.It's too low and costfully tukianza kuleta mabadiliko kwa kutaka kumbadilisha mtu mmoja mmoja hadi tupate mabadiliko tunayoyatafuta

-so it will be prudent kama tutaelekeza resources zetu za kisiasa katika kupigania mabadiliko ya msingi katika katiba yetu,mifumo ya utawala/uongozi nk

Mabadiliko na uhuru wa kweli hauwezi kuletwa kwa kulenga wigo mwembamba au dhana nyembamba ya mtu mmoja
 
Ben, nilivyomwelewa Mbowe anawakazia macho wabunge wote wa CCM: rejea kichwa cha habari, na pia hitimisho lenye rangi nyekundu kwenye posti ya thread hii. Ujumbe wake ni kwamba ndani ya mfumo wa CCM hakuna anayeweza kupambana na ufisadi, bali nje ya mfumo wa CCM inawezekana. Ndiyo maana aksema ufisadi ni hoja ya Chadema: wabunge wa CCM hawaiwezi sababu mfumo wa CCM unawaziba pumzi.
 
'CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza vita dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Malecela na wabunge wenzake waliokaa bungeni kwa muda mrefu.

Vita hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano wake wa Oparesheni Sangara uliofanyika wilayani Mpwapwa juzi.

Mbowe alisema kwa sasa umri wa Malecela kuendelea kuwa mbunge umekwisha na kwamba akisikia amechukua tena fomu kutetea nafasi hiyo mwaka huu atarusha helikopta katika kata zote za Jimbo hilo kuhakikisha anamng'oa.

"Mimi nazaliwa Malecela namsikia akiwa bungeni, nimesoma elimu ya msingi hadi sekondari, nimefanya kazi BoT, nimeacha kazi na sasa nafanya biashara, nimeingia kwenye siasa nimekwenda bungeni nimemkuta na nimemuacha, hivi huyu mtu amekuwa Sultani?,"alihoji Mbowe. '
 
-Kuna mtu katoa awkward statement inayohusu u-DJ na uchagga,nadhani still elimu ya Uraia inahitajika .DJ ni kazi na kuna watu wanategemea kazi hii katika jamii kujiingizia kipato.So kwako wewe mkuu uliyetoa hii statement unaonekana una dharau sana ,unadharau kundi flani katika jamii kwamba haliwezi kushika madaraka.Huu ni ubaguzi au uelewa mdogo wa elimu ya uraia

Kuhusu Uchagga,mkuu pia huu ni ubaguzi wa hatari sana na nadhani JF kama jukwa namba moja la siasa TZ,naomba nitumie fursa hii kutuma maombi rasmi kwa Admin wa JF kuwe na subforum mahsusi kwa ajili ya kutoa elimu ya uraia kama ilivyo majukwaa ya lugha,afya,nk
 
'CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza vita dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Malecela na wabunge wenzake waliokaa bungeni kwa muda mrefu.

Vita hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano wake wa Oparesheni Sangara uliofanyika wilayani Mpwapwa juzi.

Mbowe alisema kwa sasa umri wa Malecela kuendelea kuwa mbunge umekwisha na kwamba akisikia amechukua tena fomu kutetea nafasi hiyo mwaka huu atarusha helikopta katika kata zote za Jimbo hilo kuhakikisha anamng'oa.

"Mimi nazaliwa Malecela namsikia akiwa bungeni, nimesoma elimu ya msingi hadi sekondari, nimefanya kazi BoT, nimeacha kazi na sasa nafanya biashara, nimeingia kwenye siasa nimekwenda bungeni nimemkuta na nimemuacha, hivi huyu mtu amekuwa Sultani?,"alihoji Mbowe. '
'' Mbowe aliwashambulia baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakijinadi kuwa ni makamanda wa kupambana na ufisadi kuwa wameonyesha kutokuwa na uwezo wa kupambana na ufisadi.

"Hoja ya mapambano dhidi ya ufisadi iliasisiwa na CHADEMA, nyinyi ni mashahidi namna wabunge wa Chadema walivyopambana , mara wakajitokeza wenzetu kutoka CCM, kina John Malecela na wenzake na kujinadi ni wapambanaji wa ufisadi, lakini tulijua ngoma hii hawaiwezi na kwamba wangeishia njiani,"alisema''.

Sina tatizo na hili na ninamuunga mkono Freeman...Ila ninampinga kwa kauli zake hizi hapa chini

'CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza vita dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Malecela na wabunge wenzake waliokaa bungeni kwa muda mrefu.

Vita hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano wake wa Oparesheni Sangara uliofanyika wilayani Mpwapwa juzi.

Mbowe alisema kwa sasa umri wa Malecela kuendelea kuwa mbunge umekwisha na kwamba akisikia amechukua tena fomu kutetea nafasi hiyo mwaka huu atarusha helikopta katika kata zote za Jimbo hilo kuhakikisha anamng'oa.

"Mimi nazaliwa Malecela namsikia akiwa bungeni, nimesoma elimu ya msingi hadi sekondari, nimefanya kazi BoT, nimeacha kazi na sasa nafanya biashara, nimeingia kwenye siasa nimekwenda bungeni nimemkuta na nimemuacha, hivi huyu mtu amekuwa Sultani?,"alihoji Mbowe. '
 
Sina tatizo na hili na ninamuunga mkono Freeman...Ila ninampinga kwa kauli zake hizi hapa chini

'CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kimetangaza vita dhidi ya Mbunge wa Jimbo la Mtera, John Malecela na wabunge wenzake waliokaa bungeni kwa muda mrefu.

Vita hiyo ilitangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe katika mkutano wake wa Oparesheni Sangara uliofanyika wilayani Mpwapwa juzi.

Mbowe alisema kwa sasa umri wa Malecela kuendelea kuwa mbunge umekwisha na kwamba akisikia amechukua tena fomu kutetea nafasi hiyo mwaka huu atarusha helikopta katika kata zote za Jimbo hilo kuhakikisha anamng'oa.

"Mimi nazaliwa Malecela namsikia akiwa bungeni, nimesoma elimu ya msingi hadi sekondari, nimefanya kazi BoT, nimeacha kazi na sasa nafanya biashara, nimeingia kwenye siasa nimekwenda bungeni nimemkuta na nimemuacha, hivi huyu mtu amekuwa Sultani?,"alihoji Mbowe. '
Nakubali kuwa habari huwa ina mambo mengi ndani yake, lakini ujumbe mkuu hubaki kwenye hitimisho. Na hitimisho la habari hii limeonyeshwa mwishoni mwa stori yenyewe ni: '' Mbowe aliwashambulia baadhi ya wabunge wa CCM waliokuwa wakijinadi kuwa ni makamanda wa kupambana na ufisadi kuwa wameonyesha kutokuwa na uwezo wa kupambana na ufisadi.

"Hoja ya mapambano dhidi ya ufisadi iliasisiwa na CHADEMA, nyinyi ni mashahidi namna wabunge wa Chadema walivyopambana , mara wakajitokeza wenzetu kutoka CCM, kina John Malecela na wenzake na kujinadi ni wapambanaji wa ufisadi, lakini tulijua ngoma hii hawaiwezi na kwamba wangeishia njiani,"alisema''
 
I think Jambo ambalo Mr Mbowe anataka kulizungumzia ni Kwamba we need change, tunahitaji Mixed Mind katika Bunge letu, tunahitaji watu wengine ambao wanaweza kufikiri tofauti, We need change. Mtu kama yuko Bungeni kwa Miaka Ishirini na Hatuoni impact yake Bungeni then huyo hafai
 
Ben, nilivyomwelewa Mbowe anawakazia macho wabunge wote wa CCM: rejea kichwa cha habari, na pia hitimisho lenye rangi nyekundu kwenye posti ya thread hii. Ujumbe wake ni kwamba ndani ya mfumo wa CCM hakuna anayeweza kupambana na ufisadi, bali nje ya mfumo wa CCM inawezekana. Ndiyo maana aksema ufisadi ni hoja ya Chadema: wabunge wa CCM hawaiwezi sababu mfumo wa CCM unawaziba pumzi.

Nakubaliana na wewe kimtazamo kuwa Mbowe alikuwa anatahadharisha tatizo lilipo la baadhi ya wabunge wengine kukaa muda mrefu katika viti vyao. Lakini binafsi sioni tatizo la mbunge kukaa muda mrefu katika kiti cha ubunge. Tatizo langu lipo katika ufanisi wa wabunge hao bila ya kujali umri, rangi wala kabila lake.

Tukubaliane jamani kuna wabunge ni wabunge mfu katika bunge letu tukufu. Labda mjadala wetu uelekee huko kuliko kuchafuana hewa wa kwa kuitana majina si ya kistaarabu wala kiungwana
 
SENDER: Freeman Mbowe
to
RECEIVER: John C.Malecela
Re: Its time to go for all old generation;

MESSAGE SENT!!!!!

Namuunga mkono kwa asilimia 199.999% Mwenyekiti Mbowe kwa kusema ukweli..wazee sasa waondoke TUMEWACHOKA BWANA hata mimi toka nazaliwa,nakua,naenda sekondari,naajiriwa kazi(bongo),nachoka na ufisadi naishia ughaibuni ,naoa ,napata watoto!!!!!!Eboooo Malecela,Kingunge et al ,bado wapo tu.
Nooo this time, lazima waondoke tumewachoka sana tuu,tunataka new generation kwenye mustakabali wa uongozi wa nchi yetu. Hii nchi ndo maana haina maendeleo watu wale wale tu juzi,jana,leo na kesho!!!no tumewachoka banahh.Ndo maana na Jk anakuwa mgumu wa maamuzi,Wazee wamemzunguka kila kona Whyyyyy!!WAENDE BANAHH.
Hongera Mbowe,hawa wazee lazima waondoke hawana jipya.
 
Ben, nilivyomwelewa Mbowe anawakazia macho wabunge wote wa CCM: rejea kichwa cha habari, na pia hitimisho lenye rangi nyekundu kwenye posti ya thread hii. Ujumbe wake ni kwamba ndani ya mfumo wa CCM hakuna anayeweza kupambana na ufisadi, bali nje ya mfumo wa CCM inawezekana. Ndiyo maana aksema ufisadi ni hoja ya Chadema: wabunge wa CCM hawaiwezi sababu mfumo wa CCM unawaziba pumzi.

- Mkuu wangu, Freeman alianza vizuri sana huko Dodoma, sasa anaanza kuharibu kwa sababu anajaribu kuendeleza mkakati wa Lowassa na kundi lake la kuwaondoa wale wote wanaowasumbua bungeni, halafu the worst hana hoja hapo, maana ni yeye na mkwe wake Mtei, ndio walituambia kwamba Zitto bado ni kijana mdogo hawezi siasa za Uenyekiti, sasa amegeuka na kudai hataki wazee kwenye uongozi wa taifa, sasa kama Freeman ni mkweli basi angeanza na kuwaondoa wazee kutoka chama chake walioko bungeni,

- And then anakuja na hoja finyu kweli ya Usultani, ambayo yeye mwenyewe ameianzisha kule Chadema, tena bila hata ya aibu akamtumia mkwe wake kuua demokrasia ndani ya Chadema, kwa kumlazimisha Zitto kutema fomu ya cheo chake, ili aendele na usultani sasa leo tena yeye huyo huyo hataki usulatni Mtera, what a political joke!

- Mbunge yoyote anayefaa na asiyefaa tunataka vigezo vya kazi, lakini sio umri hapo Freeman amejishusha sana hadhi, halafu somebody need to tell this guy kwamba siasa za kumn'goa mtu mmoja ndio zimetufikisha hapa tulipo, angelilia siasa za kubadili katiba na mfumo wetu wa uongozi na jinsi wanavyochaguliwa, lakini sio kulilia umri ambao hata kwenye chama chake wapo wazee huko bungeni na tunawahitaji sana kwenye taifa! Sasa kweli Mwenyekiti wa taifa wa Chadema analilia mbunge badala ya sera, hivi kweli mtumzima na akili timamua utasimama mbele ya watu wengine wenye akili timamu na kusema kwamba Tanzania as a nation tuna tatizo moja tu nalo ni viongozi wazee kama watatu ukiwatoa hao basi kila kitu kitakua sawa?

- Freeman vipi mbona anaaza ku-sound kama kina Karamagi, maana hiyo ndiyo agenda yao namba moja ni kuwangoa wabunge wote wanaowatesa bungeni, mimi nilidhani Freeman ata-invest kwenye kuwang'oa Rostam, Lowassa, Chenge, na Karamagi, ambao hata wafadhili wetu wanamlilia Rais wetu kila wakati awang'oe, ndio maana tunaambiwa hivi vyama vya upinzani haviko serious, yaani kweli utatumia resources zote za Chadema, kushindana na mbunge mmoja tu this is incredible! Hili taifa tumelogwa maana haiwezekani tukawa mbumbumbu kiasi hiki!

- Ninamuamini sana Freeman kwamba ni better kuliko Wenyeviti wengi wa vyama vingine vya siasa nchini, lakini hapa ameliokoroga mno ndio maana tunawambia sana wabunge wapiganaji kwamba ni lazima wasimame pamoja, ama sivyo Lowassa na kundi lake hawana mchezo na wako very serious, wapiganaji wana silaha moja tu nayo umoja wao, kama walivyofanya kule kwa Seleli, wakiachana tu wamekwisha maana this Freeman's thing is un imaginable

Respect.

FMEs!
 
SENDER: Freeman Mbowe
to
RECEIVER: John C.Malecela
Re: Its time to go for all old generation;

MESSAGE SENT!!!!!

Namuunga mkono kwa asilimia 199.999% Mwenyekiti Mbowe kwa kusema ukweli..wazee sasa waondoke TUMEWACHOKA BWANA hata mimi toka nazaliwa,nakua,naenda sekondari,naajiriwa kazi(bongo),nachoka na ufisadi naishia ughaibuni ,naoa ,napata watoto!!!!!!Eboooo Malecela,Kingunge et al ,bado wapo tu.
Nooo this time, lazima waondoke tumewachoka sana tuu,tunataka new generation kwenye mustakabali wa uongozi wa nchi yetu. Hii nchi ndo maana haina maendeleo watu wale wale tu juzi,jana,leo na kesho!!!no tumewachoka banahh.Ndo maana na Jk anakuwa mgumu wa maamuzi,Wazee wamemzunguka kila kona Whyyyyy!!WAENDE BANAHH.
Hongera Mbowe,hawa wazee lazima waondoke hawana jipya.

- Freeman kijana alifanya nini bungeni zaidi ya kukubaliana na mafisadi kila siku, ni lini umewahi kumsikia Freeman akishambulia mafisadi au simply akimshambulia Lowassa au Rostam, Freeman hana hoja hapa kama ni wazee basi hata Ndesamburo ni mzee, Dr. Slaaa ni mzeee pia, Freeeman hana hoja siasa za uzee na ujana ni smply a myth ambayo Freeman hana facts za kutosheleza any side iwe ya wazee au ya vijana, yeye kijana amemfanyia nini Zitto kijana mwenzake kule Chadema, mbona hakumpisha kwa vile Zitto ni kijana kuliko yeye?

- Hili taifa mpaka tutakapoamka usingizini ndio tutalinasua kutoka kwenye uongozi mbovu wa vyama vyote, hivi kweli huko Chadema hakuna kiongozi wa kuweza kushika Uenyekiti akaweza kuongea sense kuliko hizi nonsense za Freeman? I mean this is a cry for a new chairman, huwezi sema mbele ya public kwamba utatumia resources zote za chama kumng'oa mbunge mmoja tu this is foolish!

-Inasikitisha sana!

FMEs!
 
Back
Top Bottom