Mbowe awashangaa watanzania... Uwanja wa Ndege Kilimanjaro unakodishwa kwa Dola 1,000 kwa MWAKA!

ASUBUHI HII KAMA DKK KUMI ZILIZOPITA MUHESHIMIWA MKUU WA UPINZANI FREEMAN AIKAEL MBOWE KATIKA MASWALI KWA WAZIRI WA UCHUKUZI AMEULIZA KUHUSU KUSIKITISHWA NA MKATABA WA KIA KATI YA SERIKALI NA KIDCO AMBAPO KAMPUNI HIYO INATENGENEZA MABILIONI NA KUILIPA SERIKALI DOLA 1000 KWA MWAKA

OLESENDEKA AMESHAURI SERIKALI IWACHUKULIE HATUA KALI WOTE WALIOINGIA MKATABA HUO

WAZIRI KAKATAA KASEMA SASA NI UTEKELEZAJI TUUU

aibu kubwa kwa serikali ya CCM na JK

Hapo kwenye Nyekundu:

Inakuwaje mimi ambaye ni mfanyakazi(muajiriwa) kodi yangu kwa mwaka(PAYE) ni zaidi ya dola 3500 na wakati sifanyi biashara? Ina maana pato langu ni kubwa kuliko la Kampuni hiyo?

Hivi ni nani walioingia mkataba huo? na je, ni nani aliyewapa jukumu hilo? Mkuu wao ni nani na je, analijua hili?

Hivi hili nalo linaweza kujadiliwa kishabiki (Kichama) huko Bungeni? Hongera Mh. Ole Sendeka, kwani wewe si kama wale wengine.

Hivi nchi hii inao viongozi kweli!

Dola 1000 kwa mwaka!!!
Au mwandishi amekosea alimaanisha dola milioni 1000??

Hii Ni kweli nilishawahi kuisikia kwa mfanyakzi 1 pale KIA alikuwa anasema hivyo nikamuona kama muongo lakini ilipo fuatilia kwa undani ikapata jibu ni ukweli. Tukiendelea kucheka na CCM watazidi kuifilisi hii nchi kwani wengi wao katika CCM ni mahayawani

KWELI HATA MBINGUNI TUTAULIZWA TULIIFANYIA NINI NCHI YETU WAKATI MUNGU ALITUPA KILA KITU.....SISI KILA MWEZI TUNALIPA TAKRIBANI 2.5m KADCO IT MEANS TUNALIPA KARIBIA 30M PER YEAR KWA LANDING FEES TU. LAKINI WENYEWE WANALIPA 1000$ = 1,550,000 PER YEAR HAYA NI MATUSI MAKUBWA KWA WATANZANIA ETI NA SISI TUPO NA KASI MPYA ARI MPYA NA NGUVU MPYA......TUFIKIE MAHALI TUKUBALI YAMETUSHINDA

dola 1000 kwa mwaka!!!
Au mwandishi amekosea alimaanisha dola milioni 1000??

hakuna lililokosewa hapo kaka... Ni kweli na inashangaza sana bungeni sijui wanatafuta nini badala wazunguke kutafuta mapato ya serikali wao wanabishana posho,.......

Nipata kumsikia Profesa Lipumba, akisema ukiwa na uwezo wa kununua mabeberu 100, ya mbuzi kila mwezi, basi wewe una uwezo kukodisha uwanja wa KIA kwa mwezi

KAMPUNI HIYO INATENGENEZA MABILIONI NA KUILIPA SERIKALI DOLA 1000 KWA MWAKA

Hapo bold ni kweli au umekosea tarakimu?

Hebu fafanua !

Mkuu na mimi nilitaka kuuliza swali hilo hilo!!! Hiyo figure ya USD 1,000 kwa mwaka ni sahihi? Mleta habari hebu angalia vizuri halafu utujuvye. Kama ni kweli, basi nchi hii kwa ufisadi ni zaidi ya tujuavyo!!!

Tiba

Ifike mahali sisi Watanzania lazima tukubali kwamba sasa Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake. Kama wananchi wa kawaida walipopoteza imani na Polisi na Mahakama na kuamua kutoa hukumu zao huko huko mitaani kwa Vibaka, mimi naona kama tunamfahamu mtu aliyetuingiza kwenye mikataba ya kijinga kama hiyo naye ni sisi wananchi sasa ni wakati wa kuchukua sheria mikononi na kuwauwa tu kama wanavyofanyiwa wezi wa kuku.

Nafikiri tuanzie hapo maana hapa hatuna Serikali wamejaa wezi tu huko serikalini

haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa!, hii ni dharau, vitu vingine vinatia hasira, hebu washughulikiwe haraka hao watu wanatutia umaskini tu, kumbe elimu bure inawezekana vitu hivi vikidhibitiwa, hapo ni KIA tu.

Tatizo kubwa kabisa linalo ikabili hii Nchi ni Watu na Wabunge wenyewe kutokujua majukumu yake nakwakufanya hivyo kamwe hatutasonga mbele.Kazi ya Bunge nikutunga Sheria nakuisimamia Serikali.

Bunge letu Baadhi ya Wabunge vibaraka na wabunge wote wa ccm wamejigeuza sehemu ya Serikali ndomana Mawaziri ambao ndo Serikali yenyewe hawawajibiki, Bunge limegeuka kazi kubwa nikuwapigia makofi Mawaziri badala yakuhoji utendaji wao katika kuwaletea Wananchi Maendeleo, kwa wale wanaofuatilia Bunge la Kenya pale ndo unaona kazi ya Bunge na kazi ya Serikali hakuna Longolongo Waziri anabanwa ile mbaya na hakuna Mtu anayemshangilia coz ndo kazi yake, Jamaa anamshangilia Sendeka ile ndo kazi yake na Wabunge wote.

Ukifuatilia Bunge la Kenya utaona hiyo sio issue.

POSHO kaka, nchi hii imeshaliwa tayari na wewe ukipata chance komba tu, kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake. Inafikia hadi mwakilishi wa wananchi maskini naye anaomba rushwa duh .....

Itatugharimu sana kurudisha tunu za taifa hili zilizokuwepo enzi za mwalimu.

Bado sikushauri uchukue uamuzi wa kuiba eti kwa sababu wengine wanaiba. Tunapambana usiku na mchana kuhakikisha kuwa vizazi vyetu vinaondokana na ufedhuli huu.

Please endelea kuwa mzalendo katikati ya manyang'au ya CCM na pambana kuondoa uozo uliopo.

Serikali ndo inajipanga kusomesha wanasheria wabobee kwenye sheria za mikataba!!! lol, huu ni upuuzi ajabu ni kwamba wanasheria wetu wamekuwa makini sana kuwatetea wachache wanaotaka kunufaika na mikataba hii

Ama kweli nchi hii ni kichwa cha mwenda wazimu yaan bilioni kwa dola 1000 hakuna hata simple ratio na wanazidi kutuambia wanadhamira ya dhati ya kutuondolea matatizo watz hawa viongozi wetu kweli ni machizi.

Hapo kwenye Nyekundu:

Inakuwaje mimi ambaye ni mfanyakazi(muajiriwa) kodi yangu kwa mwaka(PAYE) ni zaidi ya dola 3500 na wakati sifanyi biashara? Ina maana pato langu ni kubwa kuliko la Kampuni hiyo?

umetonesha pachungu ndugu, PAYE inatumaliza wengi na hata kama unafanya biashara TRA hawakuachi kodi kubwa kubwa

Ni kweli mwekezaji ni mkaburu aliyewekwa kama ushahidi ila nyuma ya pazia ni kigogo mkubwa aliyekuwa awamu ya tatu na mkewe ndio wanaokula kiulaini.

SERIKALI imetangaza kusitisha mkataba wa uendeshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA) na sasa inamiliki hisa asilimia 100.

Waziri wa Uchukuzi, Omar Nundu ametangaza hivyo leo bungeni mjini Dodoma wakati anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe (Chadema), kuhusu mkataba kati ya Serikali na Kampuni ya Kilimanjaro Airport Development Company (KADCO).

“Baada ya Serikali kuona mkataba huu ulikuwa haukidhi haja zilizotakiwa katika mkataba, ilisitisha mkataba huo na hivi tunavyoongea sasa, tumechukua hisa zote asilimia mia moja,” amesema Waziri Nundu.

Awali, akijibu swali la msingi la Mbowe, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Athumani Mfutakamba alisema KADCO iliingia mkataba na Serikali wa miaka 25 wa kuendesha na kusimamia kiwanja hicho tangu kibinafsishwe mwaka 1998.

Amesema, kwa mujibu wa mkataba huo, KADCO ilipewa masharti ya kuboresha na kuendeleza miundombinu ya KIA; kuboresha huduma za usafiri wa anga katika kiwanja hicho na hivyo kukuza utalii na kilimo hususan kilimo cha maua na mboga.

Mengine ni kukigeuza kiwanja hicho kutoka chombo kinachoendeshwa kwa hasara kuwa chombo kinachoendeshwa kwa faida na kutafuta wawekezaji katika maeneo mengine ya biashara kama vile hoteli na hivyo kukifanya kiwanja kuwa lango la utalii katika Kanda ya Kaskazini.

“Kwa kipindi cha 1998 hadi 2009, KADCO iliwekeza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro Dola za Marekani milioni nne. Fedha hizo zilinunua mitambo ya kuimarisha usalama na kukarabati barabara ya kutua na kurukia ndege,” amesema Naibu Waziri wa Uchukuzi.

Amesema,vyanzo vikuu vya mapato kwa Kampuni ya KADCO ni ada ya tozo mbalimbali kutoka kwa watumiaji wa kiwanja kama vile ada ya kutua na kuegesha ndege na kodi kwa wapangaji na tangu kampuni hiyo ianzishwe, imepata Sh bilioni 56.94.

Mfutakamba amesema, pia tangu KADCO ianzishwe, imelipa kodi kwa Serikali zinazofikia Sh bilioni 3.072 hadi kufikia mwaka 2010, na Halmashauri ya Wilaya ya Hai ilipata Sh milioni 84.13 hadi mwaka jana, wastani wa Sh milioni 7.01 kwa mwaka.

Hata hivyo, Mbowe alitaka mwongozo wa Spika baada ya kudai kuwa Naibu Waziri pamoja na nyongeza ya majibu ya Waziri Nundu yalikuwa na upungufu mkubwa.

Alidai kuwa, kauli ya Naibu Waziri kuwa, KADCO iliwekeza fedha Sh bilioni sita kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya kutua na kurukia ndege wakati fedha hizo zilitolewa na Benki ya Dunia na mradi kutekelezwa na kampuni nyingine.

Alihoji kama Naibu Waziri atakubali kufuta jibu lake juu ya mwekezaji huyo wa KIA kwa sababu hakusema ukweli.

Hata hivyo, Spika Anne Makinda alisema ni vizuri Mbowe apeleke maelezo yake kwa maandishi ili kuwa na ushahidi na Serikali ipeleke maelezo yake yalinganishwe na kuona jibu sahihi ni lipi.

Nachelea kusema kuna mikataba ambayo serikali ilishatangaza kuwa imevunjwa au kusitishwa only to find that bado wawekezaji wanaimiliki!

Sometimes unakuta whatever way is ok, for what ever way woote wananyakua cha juu kwa kukomba...

Back
Top Bottom