Mbowe awasha moto Mbeya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe awasha moto Mbeya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Dec 22, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,195
  Trophy Points: 280
  Mbowe awasha moto Mbeya

  • Ataka wananchi kuiga mfano wa Tarime

  na Mwandishi Wetu
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema hali ngumu ya maisha inayowakabili wananchi kwa sasa imesababishwa na mipango mibovu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

  Mwenyekiti huyo alisema wakati umefika kwa Watanzania, hususan wananchi wa Mbeya Vijijini, kujiletea ukombozi kama walivyofanya wananchi wa Jimbo la Tarime kuachana na CCM.

  Mbowe alisema hayo juzi wakati akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Mbalizi katika mkutano wa hadhara, uliofanyika baada ya mkutano wa Kamati Kuu ya chama hicho ulioidhinisha jina la Shitambala, kugombea ubunge Mbeya Vijijini.

  Mwenyekiti huyo ambaye alikuwa na viongozi wengine wa kitaifa wa chama hicho pamoja na wabunge wake, alisema nchi inayumba na hali ya maisha ya wananchi imezidi kuwa ngumu kutokana na kupanda kwa gharama za maisha kunakosababishwa na serikali ya CCM kushindwa kuweka mipango mizuri ya kuimarisha uchumi wa nchi.

  “Naomba niwaulize swali, hivi katika kipindi cha uongozi wa Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi na kipindi cha Benjamin Mkapa, kipindi kipi hali ya maisha ilikuwa na nafuu?” Wananchi walijibu wakati wa Mwinyi, na “Je, kipindi cha Mkapa na kipindi hiki cha Rais Jakaya Kikwete, kipi afadhali?” Wananchi walijibu kipindi cha Mkapa.

  “Sasa kwanini mnaendelea kuikumbatia CCM, igeni mfano wa wananchi wa Tarime,” alisema Mbowe.

  Mbowe alisema ugumu wa maisha unaowakabili wananchi ni fundisho kwamba wasiendelee kuing’ang’ania CCM ambayo kimsingi haina mpango wa kuwaletea maendeleo na badala yake viongozi wa chama hicho wamekuwa wakifanya kazi kubwa ya kujilimbikizia mali.

  Alisisitiza kuwa wananchi wa Mbeya Vijijini, wawaige wenzao wa Tarime ambao baada ya kunyanyaswa kwa muda mrefu na serikali ya CCM, wameamua kufanya mabadiliko ya viongozi, akiwemo mbunge ambaye anatoka CHADEMA.

  “Inashangaza kuona Mkoa wa Mbeya ambao una wananchi wengi wenye uelewa mkubwa lakini hakuna hata mbunge mmoja anayetoka chama cha upinzani, wakati ipo mikoa ambayo wananchi wake sasa wameamua kubadilika kwa kuwachagua wabunge kutoka vyama vya upinzani,” alisema Mbowe.

  Aliongeza kuwa hakuna mwananchi asiyefahamu kwamba wabunge wa CHADEMA wamefanya kazi nzuri bungeni ya kutetea masilahi ya nchi ambapo wamewezesha kuwafichua mafisadi walioanza kujilimbikizia mali, huku Watanzania wakiendelea kuwa maskini.

  Alisema chama chake kitamsimamisha mgombea wake Shitambala katika Jimbo la Mbeya Vijijini ili kutoa fursa kwa wananchi wa jimbo hilo kupata mbunge kutoka chama hicho kama walivyofanya wenzao wa Tarime.

  Alisema baada ya Kamati Kuu (CC), kupitisha jina la mgombea ubunge, viongozi waandamizi wa chama hicho wataweka kambi katika jimbo hilo kuhakikisha mgombea wao anachaguliwa.

  Wakizungumza na Tanzania Daima, baadhi ya wananchi waliokuwepo katika mkutano, walisema wamechoshwa na serikali ya CCM na hawafikirii kukipigia kura chama hicho katika uchaguzi huo na uchaguzi mkuu mwaka 2010.

  Walisema Jimbo la Mbeya Vijijini ambalo wananchi wake ni wakulima, linakabiliwa na tatizo la ukosefu wa pembejeo za kilimo kama vile mbolea, lakini serikali ya CCM imeshindwa kutafuta ufumbuzi wa tatizo hilo.

  Mbowe baada ya kumaliza kuhutubia mkutano huo pamoja na wajumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, walirejea jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kupanga mikakati ya kampeni za uchaguzi wa jimbo hilo, zinazotarajiwa kuanza Desemba 28 mwaka huu.

  Jimbo la Mbeya Vijijini liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wake, marehemu Richard Nyaulawa, kufariki dunia Novemba 9, mwaka huu, jijini Dar es Salaam.

  Uchaguzi wa jimbo hilo unatarajiwa kufanyika Januari 25, mwaka huu.
   
 2. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,813
  Likes Received: 83,195
  Trophy Points: 280
  CCM haitaki helikopta Mbeya Vijijini

  • Kamati Kuu yadai ni matumizi mabaya ya fedha

  na Edward Kinabo
  Tanzania Daima~Sauti ya Watu

  ZIKIWA zimebaki siku saba kabla ya kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini kuanza, Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC), imepiga marufuku matumizi ya helikopta katika kampeni hizo kama ilivyokuwa katika Jimbo la Tarime.

  Vyanzo vyetu vya habari kutoka ndani ya CC iliyokutana jana jijini Dar es Salaam chini ya Rais Jakaya Kikwete, ilisema kuwa matumizi ya helikopta katika jimbo hilo lililokuwa chini ya Mbunge wa CCM, marehemu Richard Nyaulawa, aliyefariki dunia, ni matumizi mabaya ya fedha.

  Kwa mujibu wa habari hizo, CCM imepanga kutumia zaidi ya sh milioni 700 lakini gharama zote zisizidi sh bilioni moja.

  "Tarime CCM tulitumia zaidi ya sh bilioni mbili hadi kuagiza helikopta mbili siku za mwisho na bado tukashindwa, safari hii hatutaki tena kutumia gharama hiyo," kilisema chanzo chetu cha habari kutoka ndani ya kikao hicho.

  Suala la gharama za uchaguzi Tarime, liliwahi pia kuzungumziwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Pius Msekwa na kupendekeza namna nyingine bora ya kujaza nafasi zinazoachwa wazi na viongozi wa kuchaguliwa ili kuepuka gharama.

  Katika hatua nyingine, CCM imetaja majina ya viongozi na makada wake watakaongoza kampeni katika uchaguzi huo.

  Baadhi ya viongozi hao ni Makamu mwenyekiti mstaafu, John Samwel Malecela, Makamu Mwenyekiti wa sasa, Pius Msekwa, Mwenyekiti wa UVCCM, Yusuf Masauni na makamu wake, Beno Malisa, Nape Nnauye na Luteni Yusuph Makamba, ambaye atatumika kama mshauri na si kiongozi wa kampeni hizo kama ilivyokuwa Tarime.

  Katibu wa CCM wa itikadi na uenezi, John Chiligati, akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za chama hicho, jijini Dar es Salaam jana, alisema chama hicho kitanzindua kampeni zake Januari 4, 2009, katika uzinduzi utakaofanywa na Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Ali Hassan Mwinyi.

  Alisema baada ya uzinduzi huo, kampeni za kumnadi mgombea huyo zitakuwa zikiendeshwa na kamati ya siasa ya mkoa huo, na ofisi ya Katibu Mkuu wa chama, iliyo chini ya Makamba, itakwenda Mbeya kutekeleza wajibu wa kuziwezesha kampeni hizo, kwa kutoa ushauri utakaokihakikishia ushindi chama hicho.

  Ufafanuzi huo wa Chiligati ulitokana na swali aliloulizwa kuhusu nini utakuwa wajibu wa Makamba katika kampeni hizo, hasa baada ya chama hicho kushindwa katika uchaguzi mdogo uliopita wa Jimbo la Tarime, ambapo alijibu kama ifuatavyo:

  "Si kweli kwamba Makamba alisababisha CCM ishindwe Tarime. 2005 tulishindwa Tarime, Makamba alikuwepo? Mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni. Kile kiti kilikuwa cha CHADEMA sisi tulikuwa tunajaribu tu lakini hatukufanikiwa, tutakwenda tena uchaguzi mkuu wa mwaka 2010, labda watakuwa wamebadili mawazo watatuunga mkono.

  "Kampeni ya uchaguzi Mbeya itafanywa na kamati ya siasa ya mkoa …wilaya na sisi kutoka makao makuu tutakwenda kule kuwa kama ‘facilitators' (wawezeshaji), jukumu letu kubwa litakuwa ni kushauri hapa na pale na kuangalia mwenendo wa kampeni…mikakati ili tushinde."

  Alipoulizwa kwanini kampeni hizo ziendeshwe na kamati ya siasa na Makamba awe mshauri tu, wakati katika uchaguzi mdogo wa Tarime Makamba alikuwa kinara wa kumnadi mgombea wa CCM licha ya kuwepo kamati ya siasa ya Mkoa wa Mara, alisema:

  "Siyo kwamba hatakwenda Mbeya…hapana, atakwenda Mbeya. Yeye ndiye Katibu Mkuu. Kwa katiba yetu yeye ndiye mkurugenzi wa uchaguzi, kwa hiyo hawezi kuacha kwenda Mbeya kwa sababu kampeni zote zipo chini yake. Lakini nimesema yeye atakuwa ni facilitator (mwezeshaji), ambaye atakuwa akishauri na kuhakikisha mambo yote yanakwenda sawa ili tupate ushindi. Kamati ya siasa ndiyo itafanya kampeni zote na tayari wameshajipanga, kuanzia kwenye nyumba kumi kumi na matawi."

  Akimtangaza mgombea wa CCM kwa ajili ya uchaguzi huo, alisema CC ya chama hicho, imemteua Luckson Ndaga Mwanjale (58), kuwa mgombea wa kiti hicho, baada ya kupitia sifa za wagombea wote tisa walioomba kuteuliwa.

  Alielezea sifa zilizomfanya Mwanjale kuteuliwa na chama hicho kwamba ni kuwa na stashahada ya elimu ya ufundi, ameshika nafasi mbalimbali katika uongozi wa CCM, ni katibu wa dhehebu lake la Uinjilisti na ameongoza katika kura za maoni.

  Alisema, Mwanjale aliyepata kura 435, aliwashinda wagombea wengine wanane, akiwamo, Allan Mwaigaga, aliyepata kura 259, Andrea Sayile (229), Generali Robert Mboma (164), Diovita Diyame (162), Petro Mwashusha (28), Flora Mwalyambi (26), Michael Mponzi (23) na Maria Mwambanga aliyepata kura 19.

  Alipoulizwa kwanini CCM imempitisha mgombea huyo ambaye kumbukumbu zinaonyesha kuwa alishaomba kuteuliwa na chama hicho kuwania nafasi hiyo hiyo mara tatu, lakini hakuteuliwa kwa kuwa hana sifa za kuwa mbunge, alisema kuwa katika chaguzi zilizopita ukiwemo uchaguzi wa mwaka 2005, mgombea huyo alijitokeza lakini hakupitishwa kwa sababu alikuwa hajakomaa na ndiyo maana kura zake hazikutosha.

  Alisema kwa sasa wanaamini kuwa mgombea huyo ameshakomaa na ndiyo maana kura zake zimetosha, kwa kuweza kuwazidi wanachama wengine wanane wa CCM walioomba kuteuliwa kuwania kiti hicho.

  Katika mkutano huo, Chiligati pia alitoa taarifa kuhusu uteuzi wa wagombea wa nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (CCM), Mkoa wa Tabora, baada ya kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho kilichoketi Novemba 11, 2008 kuagiza nafasi hiyo itangazwe upya kutokana na kubakia mgombea mmoja tu.

  Alisema baada ya nafasi hiyo kutangazwa upya walijitokeza wanachama wanne, ambapo kati yao, walioteuliwa kugombea nafasi hiyo ni Mwasiti Badru Ngesi, Tatu Mussa Ntimizi na Lucy Kayanda Sekasua.

  Aidha, alisema kamati kuu imempongeza Yusufu Hamad Masauni kwa kuchaguliwa na mkutano mkuu wa taifa wa UVCCM uliofanyika Dodoma hivi karibuni kuwa mwenyekiti mpya wa taifa wa jumuiya hiyo, na Beno Malisa kuwa Makamu Mwenyekiti wake.

  Uchaguzi mdogo wa Mbeya Vijijini, unatarajiwa kufanyika Junuari 25 mwakani.
   
 3. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2008
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,508
  Likes Received: 2,750
  Trophy Points: 280
  Hizo million 700 au billion 1 bora wangezipeleka kwenye maendeleo. Kweli CCM hawana periorities. Sasa pesa yote hiyo itaenda kwenye pilau na pombe.
   
 4. M

  MPadmire JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2008
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 2,633
  Likes Received: 905
  Trophy Points: 280
  Safari hii nitaenda Mbeya kuchukua fungu langu, siachi hizo pesa.

  Hizo pesa ni kodi za watanzania, au unabisha....?

  KWani ccm Ina mradi gani wa kuingiza pesa?

  Kwani kama ni magari wanayo, kinachohitajika ni hela ya mafuta ya magari na accommodation za wajumbe na allowance. kama millioni 200 tu zinatosha.

  Kwa hiyo hizo million 800 wangejenga barabara ya changarawe ambayo inapitika muda wote. Au wajenge Madarasa au dispensari

  Sasa wananchi wakiona maendeleo huna haja wa kuwapa Tshirti au pilau.

  " Mchana nilikuwa mahali mgahawani nakunywa soda mara akaja mtu wa makamu kidogo akakaa akaagiza soda nae akaanza kunywa. Kama kawaida akapita muuza magazeti, tukaona kichwa cha habari kwamba Makamba apigwa chini, halafu watatumia billioni moja kwenye kampeni. Du wote tulihamaki, tukasema Hospitali hazina dawa, walimu hawajalipwa, wanafunzi chuo kikuu wapo majumbani halafu PEsa za kampeni zipo!!!??? Basi akasema Mimi ni mwanachama wa CCm lakini sitawapigia kura 2010, ni upuuzi. akasema ni Bora niwape upinzani au asipige kura kabisa. Sasa nimegundua kumbe ccm ina wanachama wengi lakini ni wanachama mfu. So Matendo ya ccm inawaangamiza"
   
  Last edited: Dec 22, 2008
 5. Bowbow

  Bowbow JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2008
  Joined: Oct 20, 2007
  Messages: 545
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kimsingi CCM watakuwa wanatumia 23.3m to 33.3M kwa siku. Hizi ni hela nyingi sana wazee nadhani ndio maana kuna mafisadi wengi sana ndani ya CCM.

  Assume kuna delegation ya watu 60 na wote wanalipwa high flat rate ya 100,000/day all inclusive(ni sawa 6m/day), Mafuta ya magari 30 kwa siku wakitembea 200KM kwa fuel consuption tuseme 4km per 1litre (ni sawa 50X30X1500= 2,250,000/day) garama za majukwaa vifaa vya music, matarumbeta n.k very high 2million/day, Garama zinginezo kama simu, stationary n.k say 2million/day. Ndugu zangu pamoja na hayo makisio ya juu kwa siku ni kama 12Million/day kwenye budget yao ni 23m to 33million per day. Je CCM iweke wazi hizo hela zao zinatumika Vipi??????? Kama Kununua Ticket kadi za kupigia kura tujue, Kama kutoa takrima pia tufahamishwe.

  Hatuoni huo mtindo wao wa kuiflate gharama ili kujinufaisha ndio maana hata serikalini gharama za manunuzi, allowance, miradi, n.k zimekuwa juu tofauti na hali halisi kutokana na tabia hii ya CCM????

  TRA Mkae mkao wa kupata nyngeza ya kodi. Ni wajibu wenu kufuatilia na kuhakikisha mnapata kodi isiyopungua 200m (20%) kutokana na wale wote wanaolipwa kutoka kwa CCM

  Vyombo vya usalama ni wajibu wenu sasa kuangalia inflow ya income ya wakuu wote wataokuwepo kwenye kampeni ikiwa ni pamoja na kumonitor matumizi yao kuona kama yanaendana na vipato vyao na vipato vyae vinandana na mapato halali wanayostahili kupewa kulingana na sera na taratibu ya vyama husika
  ni hayo tu
   
 6. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #6
  Dec 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Mungu wa Ibrahim , Isaka na Yakobo , Mungu aliye waangamiza wa misri na kuisha Isarael bahari ya sham , Mungu mwenye nguvu kushinda watawala wote na hata wale watumiao mapesa haramu kama CCM atawapa kichaa CCM na watapayuka na kupelekea Chadema kushinda uchaguzi huu .Ukombozi ni huu na Mbeya wana nafasi sasa kuonyesha kwamba wao ni zaidi ya pilau .
   
 7. K

  Koba JF-Expert Member

  #7
  Dec 22, 2008
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  .....OK,Tarime wamechagua Chadema lakini akiulizwa Tarime ina tofauti gani na mbeya baada ya uchaguzi atajibu nini? anyway nafikiri upinzani hawana watu makini wa kupiga kampeni na kushinda,siamini kama CCM wako strong kiasi hicho cha kuwa na 90% ya viti bungeni,wananchi wengi najua wamechoka na CCM ila sometimes hawaoni alternative kutoka upinzani,mfano jimboni kwangu nasikia mbunge wa upinzani aliyesimamishwa alikuwa hawezi hata kujieleza chochote zaidi ya kutukana CCM tuu,hakuwa na strategy yeyote,hakuwa na pesa na alikuwa muda mwingi anapiga kampeni kwa baiskeli ili aonekane mtu wa watu na kaja siku za mwisho mwisho za uchaguzi na miaka yote hata home alikuwa haendi anaishi Dar tuu,kibaya zaidi namjua personally jamaa njaa tupu na hana kazi mjini alienda tuu kubahatisha ulaji lakini na kuvurunda kote kule aliambulia 30%,imagine angekuwa kichwa kizuri,then unajiuliza kuna sababu gani ya kuwa na upinzani wenye character kama za huyu jamaa? naamini watu makini wakiingia upinzani, CCM watayeyuka haraka sana
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2008
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145  Koba bwana unakuwa mtu wa ajabu sana. Samahani kwa kukudhani hivi lakini ulitaka watu waendao upinzani watoke Mbinguni ama ni wewe na mimi kuacha siasa za hapa JF na kwenda front ? Siasa za nyumbani hapa ni ngumu na usione watu wanapiga kelele .Zitto na wenzake kwenda public namna ile wana sacrifice mambo mengi .Zitto leo hawezi kupata kazi kwenye public sector kirahisi ama serikali kwa kuwa ni cancer .Leo hata mambo ya jimboni kwako huyajui tena umesema umesikia hayo na unasema wapinzani hawana watu makini .Nani aende awe makini kama si wewe kuamua kuja na kuongeza watu makini kwenye upinzani ?
   
 9. M

  Mtarajiwa JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2008
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 440
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Naungana na Koba.Ukiacha tshirt na kanga lakini bado hatujapata wapinzani wazuri wa kutuwakilisha kwenye majimbo ya uchaguzi na ndiyo maana CCM inashinda kiurahisi.Na mimi haya niliyashuhudia mwenyewe katika uchaguzi wa mwaka 2005.Wananchi wengi wa jimbo lile walikuwa wamechoshwa na Mbunge wao ambaye alikuwa ameshawawakilisha kwa miaka 10 na mbaya zaidi mtu waliyemtaka kutoka hukohuko CCM aliondolewa kwenye vikao vya juu baada ya kupitishwa katika mchujo wa chini.Yani hapa alikuwa anapelekwa mpinzani ambaye ni mbunge material basi CCM ilikuwa kwisha kazi.Badala yake chama kimoja cha upinzani ambacho ndicho kilikuwa mbadala kwa wananchi wengi kikaleta jamaa mmoja mchovu na mtupu kwa kila kitu.
  Kusema hivi haina maana wapinzani watoke mbinguni.Wapinzani hawana sababu ya kung'ang'ania kugombea urais huku wakijua wazi kuwa mgombea wa CCM atashinda.Wapinzani wangehamishia nguvu zao kwenye ubunge.Watu kama Lipumba,Mbowe,Mbatia,Mvungi,Baregu,Mrema nk wakienda kwenye majimbo ni lazima watashinda tu.Wakishaliteka bunge hata kushinda urais inakuwa rahisi!
   
 10. SaidSabke

  SaidSabke JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2008
  Joined: Sep 28, 2006
  Messages: 1,969
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  Kwa mbeya vijijini wapinzani hawana bao labda SISIM wafurunde wao lakini inaelekea Tarime walipata somo zuri.
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2008
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  "Dua la kuku halimpati mwewe"
   
Loading...