Mbowe awaagiza wabunge wote wa upinzani wasifunge Midomo Bungeni, awapongeza Mdee na Ester Bulaya

Upinzani wamekuwa wavumilvu sana ndani ya Bunge ila bahati mbaya uvumilivu wao umetafsiriwa vibaya na sasa nao inaonekana wamechoka na wanajipinga kukabiliana na hali hiyo vilivyo.

Siku si nyingi huenda tukashuhudia yale ambayo yamekuwa yakitokea katika mabunge mengine duniani kwa watu kurushiana makonde na kutoleana maneno makali.

Binadamu akichoka ni kiumbe hatari sana.
 
Wameshatishwa kwamba wameletewa askari wakali watakuwa waoga kumpinga spika.
 
Unafikiri nani atambishia mfalme..?
CCM wana mfalme wao na Chadema wana mfalme wao pia.
Tofauti yao huyu wa Chadema ni yupo under control tangu mwaka juzi
 
Yaani Ndugai na wabunge wenzake wa Sisiem wamefanya 'kituko' cha mwaka........

Yaani John Mnyika katukanwwa na yule mwanamama wa CCM Show......nzaaa kwa kuwasha mic na kumwita mwizi......

Mheshimiwa Mnyika kaomba mwongozo kwa Spika kuwa kwa mujibu wa kanuni za Bunge Mbunge aliyewasha mic na kumwita yeye mwizi, aidha afute kauli yake au athibitishe wizi wake.

Cha ajabu kupita kiasi Ndugai akadai hakumsikia huyo Mbunge wa CCM mwenzie aliyemwita Mnyika mwizi!

Badala yake akaamua kutumia rungu lake la Uspika kuagiza maaskari wa Bunge wamtoe msobe msobe Mnyika kama kibaka!

Kwa mazingira hayo Ndugai amepoteza completely sifa za kuwa Spika wa Bunge la vyama vingi, kwa kuwa kwake yeye kwa wabunge wenzake wa CCM akina Kibajaj, Msukuma, Mlinga, Shonza na wengineo wakiwatukana wabunge wa upinzani, kwake ni ruksa!

Na inapotokea wabunge wa upinzani wakaprotest uonevu huo wa wazi wa Spika Ndugai, wabunge hao kwake yeye Ndugai anataka wawe treated kama vibaka na wanastahili kupigwa 'ban' ya kutoingia Bungeni kwa kipindi cha mwaka mzima!

Hivi anawezaje yeye kama Spika kuweza hata kuzikiuka kanuni za Bunge lake na kutoa adhabu ambazo ni kinyume na zinazoelekezwa na kanuni za Bunge lake mwenyewe!?

Ingawa Mimi siyo mtabiri lakini naziona dalili za wazi kabisa kuwa in the near future zitapigwa ngumi kavu kavu kwenye Bunge hilo kati ya wabunge wa CCM na wabunge wa upinzani.....

Kwa kuwa wabunge wetu wa upinzani wameitekeleza kwa kipindi kirefu ile principle ya Bwana wetu Yesu Kristo kuwa akupigaye Kofi shavu la kushoto mgeuzie pia shavu la kulia aendelee kukuchapa makofi mengi kadri atakavyo.....

Hata hivyo enough is enough, Inabidi sasa wabunge wa upinzani watafute option nyingine ya kujihami na uonevu huu wa wazi wazi wanaofanyiwa na wabunge wenzao wa CCM.
 
Watu wanatamani zama hizi zirudi.

chadema.jpg



Z-1.jpg


dsc093961.jpg
Chadema iliwapenda lakini CCM iliwapenda zaidi.
 
Kiongozi wa kambi rasmi ya Upinzani bungeni Mh Freeman Mbowe na mbunge wa jimbo la Hai amewaagiza wabunge wote wa upinzani kutokukaa kimya.

Amewapongeza pia Mbunge wa kawe, Halima Mdee na Mbunge wa Bunda Ester bulaya kwa kutoogopa na kisimamia haki bungeni kwa kusema waliyoyaona.

Pia amesema kuna uhuru wa kuhoji viongozi pale wanapokosea na sio kila mara kusifia tu, wabunge wote wa upinzani ni wakati sasa wa kusimamia haki na kutokufunga Midomo tuwapo bunge au nje ya bunge..

Nini maoni yako??

Kim IL Sung kesha sema nani wa kupinga?
 
Kwenye sheria kuna kitu kinaitwa provocation.

Alichokuwa anakifanya Mbunge Lusinde siku ile hadi kusababisha Mbunge Mnyika kutolewa Bungeni utadhani ni kibaka ni provocation.

Yeye Lusinde alidai kuwa wabunge wa Chadema wanawatetea aliowaita wezi wa madini yetu.

Hivi Mbunge Lusinde anajifanya kasahau kuwa wabunge wa upinzani ndiyo kwa miaka mingi sana wamekuwa wakipiga kelele sana Bungeni kuwa mikataba iliyosainiwa na serikali ya CCM inatufanya kama Taifa tuibiwe kwa kiasi kikubwa sana na wawekezaji wa migodi ya dhahabu?

Hao wabunge wa CCM wakati wabunge wa upinzani walipokuwa wakitoa hoja hizo za kuibiwa na wawekezaji wa kigeni, wabunge hao hao wa CCM ndiyo walikuwa wakiwazomea na kuyaita madai hayo ya wabunge wa upinzani kuwa ya uzushi!

Sasa inakuwaje hivi sasa hao akina Kibajaj wawaone wabunge wa upinzani wanatetea wezi wa madini wakati ni wao wabunge wa CCM ndiyo kwa miaka mingi ndiyo wamekuwa wakiwatetea hao wawekezaji wa migodi ya dhahabu kwa kudai mikataba hiyo iko fair?

Sasa ndiyo nimeanza kuelewa hoja ya Anjela Kairuki kuwa qualification pekee ya kuwa Mbunge wa nchi hii ni ONLY kujua kusoma na kuandika!
 
Irekodi kesi ngapi! Wakati Serikali na wananchi kwa ujumla waliingizwa mkenge na kundi fulani kwa zaidi ya miaka kumi kuwa nchi inanuka ufisadi na listi ikatolewa na tukaimanishwa kuwa vielelezo vyote vya kuwatia hatiani vipo. Serikali ikaingia kichwakichwa, chapchap fungua mahakama maalum ya mafisadi ili washughulikiwe chapchap. Mahakama imekamilika, kila mmoja wetu anajua lile genge lililopasua anga kwa zaidi ya miaka kumi juu ya ufisadi lilivyoufyata. Turekodi kesi kutoka wapi?
 
Back
Top Bottom