Mbowe avuka lengo kuchangia msikiti, asisitiza amani, upendo na mshikamano

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Mbowe ataka siasa za amani, upendo zitawale

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema siasa za amani, upendo, mshikamano na zenye hofu ya kumuogopa Mungu, ndizo zinazohitajika Tanzania. Mbowe aliyasema hayo wakati akizungumza na wananchi wa Jimbo lake la Hai kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Lambo uliopo jimboni humo.

Aidha, alisisistiza suala la wananchi kujitoa katika shughuli za maendeleo ya kijamii pasipo kujali itikadi za kisiasa na kiimani.
Mbowe, ambaye pia ni Kiongozi wa Kambi ya Upinzani bungeni, alisema yeye kama kiongozi wa wananchi anapendezwa sana na siasa za amani na daima atahubiri amani na mshikamano. Alifafanua kuwa maendeleo ni suala muhimu linalomgusa kila mwananchi, hivyo inapofikia wakati wa kuangalia itikadi za kidini na vyama, itakuwa ni ngumu kuleta maendeleo ya wananchi pale inapohitajika suala la kuchangia au kushiriki katika shughuli za ujenzi wa taifa.

Katika harambee hiyo, Mbowe alichangia Shilingi milioni tano na Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, aliahidi kukamilisha paa la msikiti huo pamoja na mazulia yenye thamani ya Sh. milioni 4.5 na kufanikisha kupatikana kiasi cha Sh. milioni 30 kiwango ambacho kilivuka lengo la kukusanya Sh. milioni 15. Awali, kabla ya harambee hiyo, Mbowe alifungua ofisi ya shirika lisilo la kiserikali la Hai Kilimanjaro Development Initiative (Hakidi) ambayo ilianzishwa kwa lengo la kutoa ajira kwa vijana kupitia sekta ya utalii.
Akizungumza na wakazi wa mji huo wakati wa kupanda miti 10,000 na kufanya usafi katika maeneo hayo, Mbowe aliwataka wananchi hao kufanya usafi katika makazi yao na kupanda miti ili kusaidia upatikanaji wa maji.

Katika risala yake, Meneja wa shirika hilo, Mohamed Mbowe, alisema shirika lake linakusudia kuajiri vijana takribani 5,000 ambapo kwa kuanza watoa ajira kwa vijana 145 katika sekta ya utalii na wanakusudia kupanda miti milioni tatu kwa kipindi cha miaka minne ijayo.
Katika uzinduzi huo, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama, alitakiwa kuwa mgeni rasmi, lakini hakutokea kutokana na kwenda kulipokea kundi lililoshuka kutoka Mlima Kilimanjaro.

Source: IPPMedia

Big up Mheshimiwa Mbowe kwa kuonyesha mwelekeo wa CHADEMA chama cha ukombozi Tanzania!!!!!!!!!
 
Habari hii ni wizi wa mchana na uzushi mkubwa,mleta mada amesema source ni majira wakati mi ninalo gazeti hilo apa mkononi habari hiyo haipo,na ninayo magazeti ya majira ya tangu jumamosi. jamani mbona jamii forum inazidi kupoteza dira na mwelekeo?
 
Tangu lini mbowe akaingia msikitini wakati kwenye uchaguzi mkuu alimpiga kofi mwangalizi wa uchaguzi wa kiislam.Au mzee ndo kujisafisha?au amewaomba lini msamaha waislam? Yangu macho.
 
Kwanza asante kwa kunishtua kidogo. Sahihisho: Chimbuko la habari hii ni Gazeti la Nipashe. Cha msingi ujumbe umefikishwa kwenye audience. Thanks again kwa lugha yako ya ustaarabu.
 
Tangu lini mbowe akaingia msikitini wakati kwenye uchaguzi mkuu alimpiga kofi mwangalizi wa uchaguzi wa kiislam.Au mzee ndo kujisafisha?au amewaomba lini msamaha waislam? Yangu macho.

We ni mmoja wapo katika kundi lile linalotetea uozo kwa nguvu zote bila kujali amani na utulivu wa nchi yetu. Hakuna mtu mwenye utashi wa kweli kwa nchi yetu atakayekuwa na mtazamo wako katika masuala yanayohusu utaifa. Kesho Mbowe akichangia mpagani na mkana dini utasema si mdini, kumbuka kiongozi ni kwa wananchi wote bila kubagui.
 
Habari hii ni wizi wa mchana na uzushi mkubwa,mleta mada amesema source ni majira wakati mi ninalo gazeti hilo apa mkononi habari hiyo haipo,na ninayo magazeti ya majira ya tangu jumamosi. jamani mbona jamii forum inazidi kupoteza dira na mwelekeo?
Usipende KUKURUPUKA mjomba,soma line kwa line,neno kwa neno.Mtoa mada mwishoni kabisa amesema source ni IPP MEDIA,sasa Majira imetoka wapi?Au Majira inatoka Ipp siku hizi?
 
Tangu lini mbowe akaingia msikitini wakati kwenye uchaguzi mkuu alimpiga kofi mwangalizi wa uchaguzi wa kiislam.Au mzee ndo kujisafisha?au amewaomba lini msamaha waislam? Yangu macho.

Hivi yule aliyemtia mzee Mwinyi kibao hakuwa muislam? Mimi sijui, kwani uchaguzi mkuu uliopita uliendeshwa 'kiislam'? Napata taabu kuelewa ulichotaka tuelewe.
 
We ni mmoja wapo katika kundi lile linalotetea uozo kwa nguvu zote bila kujali amani na utulivu wa nchi yetu. Hakuna mtu mwenye utashi wa kweli kwa nchi yetu atakayekuwa na mtazamo wako katika masuala yanayohusu utaifa. Kesho Mbowe akichangia mpagani na mkana dini utasema si mdini, kumbuka kiongozi ni kwa wananchi wote bila kubagui.
Afu wanankeraga hawa wanaochanganya siasa na dini...wamesahau tz hatuna udini wala ukabila....mimi naamini huyo msimamizi alichapwa makofi sio kwa sababu ni mwislam, alichapwa kwasababu alifanya ndivyo sivyo na hata angekuwa mkristu akafanya kama huyo makofi yangemuhusu pia..
 
kama anachangia kweli.tutamuona katika harambee ya redio IMANI

Hakuna hata siku moja harambee ya kuchangia radio Iiman bali kuna kila mwenye swadaka yake katika kuboresha na kukuza coverage ya Radio hiyo basi na atoe pasi na kujinadi ametoa kiasi gani.

Lakin cha msingi ni kuwa Radio Iman kuanzia taarih 15 Dec 2011, inaingizwa katika satellite na kuweza kusikika dunia nzima kwa njia ya mtandao. Inaunganisha na Satellite ya http://www.lyngsat.com/intel906.

Hongera sana Nahdi kwa maendeleo makubwa ya radio hiyo

Habari hii ni wizi wa mchana na uzushi mkubwa,mleta mada amesema source ni majira wakati mi ninalo gazeti hilo apa mkononi habari hiyo haipo,na ninayo magazeti ya majira ya tangu jumamosi. jamani mbona jamii forum inazidi kupoteza dira na mwelekeo?
TABIA ya magamba ni kujifanya wanaona kumbe ni vipofu "Source ni ippmedia"
 
Ngoja tumuone Barubaru hapa na narration zake za hadith............

Washachangiwa msikiti sasa, kama Barubaru na wenzake hawataki, basi wakashtaki mahakama ya kadhi huko kenya.

maneno meeeengiiiiii.................hovyo kabisa. tuliwaambia muache kelele, harambee itafanyika na michango itatolewa, na msikiti utajengwa, na waumini wataswali.............
 
Back
Top Bottom