Mbowe atoa ruhusa kwa TAKUKURU kuwachunguza Lowassa, Sumaye na Nyalandu juu ya Ufisadi

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,991
144,326
Maneno ya Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe akiwa Mbeya kuendelea na ziara ya kuwanadi Wagombea wa Udiwani katika uchaguzi mdogo.

Mbowe akiwa jukwaani amesema “Nimemsikia Waziri mmoja, Waziri Kigwangalla……. anatoa maelekezo kwa TAKUKURU wamshughulikie Lazaro Nyalandu aliekua Waziri wao ambae sasa hivi fresh ndani ya CHADEMA“

“Wakasema CHADEMA mlisema Lowassa alikua fisadi tukawaambia sawa tulisema kwa wakati wake, kwenye siasa hauna Rafiki wa kudumu wala Adui wa kudumu lakini tumeshtuka kwamba huo ufisadi wake hamjaweza kuudhihirisha, mpelekeni Mahakamani…….. hawana cha kupeleka Mahakamani”

“TAKUKURU wanasema wameshapewa malalamiko kwahiyo wanayafanyia kazi tunawaambia CHADEMA hatuogopi Mahakama na kiongozi yeyote ndani ya CHADEMA mnaetaka kumchunguza akiwemo Mbowe anzeni leo hatuogopi”

“Awe ni Lowassa mchunguzeni, awe ni Sumaye mchunguzeni… awe ni Nyalandu mchunguzeni, awe ni Sugu mchunguzeni”

My take
:
Haya sasa sijui watakuja na kisingizio gani wakati wao ndio wenye dola.
 
Mimi si mfuasi wa chama chochote, ila kwa speech ya KUB Mbowe Jana, ilikuwa nzuri , si ya kubeza kisa kasema mpinzani..hata ivyo jamaa yuko smart ktk kudadavua issues... Kuna watu huwa wanambeza sana, sioni ubutu wake kimaarifa.
 
Asingetoa ruhusa wasingehojiwa?
Au maana ya ruhusa huko siasani INA maana nyingine?
 
  • Thanks
Reactions: a45
Asingetoa ruhusa wasingehojiwa?
Au maana ya ruhusa huko siasani INA maana nyingine?
Ila mbona wakipelekwa mahakamani kunakuwa na malalamiko kuwa members wetu wanafunguliwa kesi? Kama tunawaruhusu watushitakie makamanda wetu tuwe tunakaa kimya na tuache mahakama zifanye kazi zake. Naona kama tunajichanganya sana wakati mwingine na kuwapa nafuu wapinzani wetu
 
Mafisadi yamejibanza kwenye banda la CCM yanakula upepo mwanana.
Kuna lingine lilichomoka huko kwa bahati mbaya nasikia limerudi "pahala salama" aka "pepo ya mafisadi" hivi majuzi. Ukiyakuta yametulia huko hayana hata wasiwasi; yanalindwa kwa nguvu zote as long as they are loyal kwa chama.
 
kwa siku unapost Mara ngapi? maana kipindi kile cha mwenyekiti kwenda sana Nairobi , post zako zilipungua sana ila sasa ivi naona umerud kwa kasi yawezekana umeanza kuingiziaa tena pesa
 
Wanaosema king lowassa ni fisadi ni wakumbavu
Wasemaji wakuu hawa hapa
tapatalk_1469821199593.jpeg
 
Ni fisadi?!
Wewe u mgeni mjini hapa? Huna habari za a very high profile ex-official aliyerudi "peponi"; nahisi kama alishashtuka Mwenyekiti angetoa order wote waliokimbilia huko wachunguzwe. Jamaa kaona isiwe tabu, kaamua kubwaga manyanga karudi "nyumbani".
 
Kuna lingine lilichomoka huko kwa bahati mbaya nasikia limerudi "pahala salama" aka "pepo ya mafisadi" hivi majuzi. Ukiyakuta yametulia huko hayana hata wasiwasi; yanalindwa kwa nguvu zote as long as they are loyal kwa chama.
Tibaijuka, Kinana, Chenge, Geleja, Kagageshi, Rostam, Maige n.k
 
Tibaijuka, Kinana, Chenge, Geleja, Kagageshi, Rostam, Maige n.k
Yaani wametulia tuli "peponi" hao. Hakuna hata wa kuwauliza chochote as long as kadi la kijani kila waendapo wanalo; ndio ufunguo wa kuishi katika "mji ule".
 
Back
Top Bottom