Mbowe atoa mwaliko wa mkesha siku ya kupiga kura

EasyFit

JF-Expert Member
Jul 4, 2011
1,269
1,082
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mikutano ya kumnadi mgombea wake Joshua Nassari juzi na jana, ametoa mwaliko kwa wanachama na wafuasi wote wa chama hicho kwamba wafike kwenye mkesha wa kusubiri matokeo ya uchaguzi huo eneo la Leganga, jirani na Halmashauri ya Meru.

Mbowe alisema mara baada ya kubandikwa kwa matokeo katika vituo vyao, wapiga kura kwa pamoja wanapaswa kuelekea katika eneo la Leganga kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mulala, Kata ya Songoro nyumbani kwa mgombea wa chama hicho, Nassari, Mbowe alisema: "Naomba mara baada yakupiga kura, utakaa mita 103 kutoka kwenye kituo, hadi matokeo ya kituo chako yatakapobandikwa, chukua kanga, baiskeli, punda, gari au usafiri wowote tukutane Usa River ambapo tutafanya mkesha wa kusubiri matokeo."

Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kuna shinikizo la kumtaka Msimamizi ya Uchaguzi, Kagenzi atangaze matokeo tofauti hata kama Chadema watakuwa wameshinda.

"Ndugu zangu msigope kitu, tutakwenda kulala wote Usa River kusubiri matokeo yetu na kama wakitubia haki ya Mungu safari hii hatutakubali," alisema Mbowe. Mbowe aliwataka polisi siku ya uchaguzi kuwaacha Chadema na CCM wachuane wenyewe kwani kazi yao ni kulinda amani na siyo kuilinda CCM.

Mapema Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliwataka wakazi wa jimbo hilo, wasiwena hofu ya wingi wa polisi katika maeneo yao akisema haijawahi kutokea hata siku moja bunduki ikazidi nguvu ya umma.

"Makamanda jitokezi kupiga kura kuanzia saa 12:00 jioni mkimaliza msubiri matokeo na baada ya hapo tukutane Usa River na hapo kutakuwa na makada wenzenu kusubiri matokeo."

Katika mkutano huo, Viongozi wawili wa CCM, akiwemo Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Tawi la Mulala, Eribariki Manjeka alirudisha kadi ya CCM na kujiunga na Chadema pamoja na William Nassari ambaye aliwahi kuwa Katibu Mwenezi na Itikadiwa CCM katika kata hiyo.

Mwananchi.
 
Nzuri hii,nimependa. Lakini njia yao cdm pekee ya kuhakikisha "hawaibiwi" ni kukusanyika hapo tu?
 
Maji ya shingo CCM, wamegeuka kikosi cha kutukana wakisubiri kudra za tume kushinda!!

Halafu mbona huku katika mikutano yao hawasemi watu wangapi wamerudisha kadi kama inavyokuwa sehemu nyingine?
 
Mkesha ni lazima kujihakikishia ushindi! Ole wako kagenzi ukitangaza ndivyo sivyo kwa shinikizo la magamba
 
Waende na maji ya kutosha kwa ajili ya kunawa nyuso zao FFU wakifika. Wakati huo Mbowe & Co wako lodge wanakula kipupwe
 
Kwenye huu mwaliko wa Mbowe naona kashindwa kuambia waalikwa tukishindwa kwa halali mwaliko utakuaje, yeye kawaalika kukesha wakisubiri ushindi au ndio mwaliko wa mapambano.
 
Kwenye huu mwaliko wa Mbowe naona kashindwa kuambia waalikwa tukishindwa kwa halali mwaliko utakuaje, yeye kawaalika kukesha wakisubiri ushindi au ndio mwaliko wa mapambano.
Wanaenda kuhakikisha haki inatendeka. Hatutaki mambo ya Karagwe, Shinyanga mjini, Segerea, etc, yajirudie.
 
Hivyo hivyo ulivyoelewa.........gambar
Kwenye huu mwaliko wa Mbowe naona kashindwa kuambia waalikwa tukishindwa kwa halali mwaliko utakuaje, yeye kawaalika kukesha wakisubiri ushindi au ndio mwaliko wa mapambano.
 
Hakika hapatatosha hakika narudia hapatatosha.......tumejiandaa vya kutosha siri anayo mungu.
Mkesha ni lazima kujihakikishia ushindi! Ole wako kagenzi ukitangaza ndivyo sivyo kwa shinikizo la magamba
 
Mwenyekiti wa CDM kwa mara nyingine anachochea fujo, uchaguzi ni gemu kuna kushinda na kushindwa sasa anawahakikishia wanachama ushindi si kutafuta vurugu gu jamani.
Enyi polisi tunawategemea sana wakifa watatu kama ilivyokuwa ARUSHA sio mbaya maana watz tupo zaidi ya milion 45.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akihutubia mikutano ya kumnadi mgombea wake Joshua Nassari juzi na jana, ametoa mwaliko kwa wanachama na wafuasi wote wa chama hicho kwamba wafike kwenye mkesha wa kusubiri matokeo ya uchaguzi huo eneo la Leganga, jirani na Halmashauri ya Meru.

Mbowe alisema mara baada ya kubandikwa kwa matokeo katika vituo vyao, wapiga kura kwa pamoja wanapaswa kuelekea katika eneo la Leganga kusubiri matokeo ya uchaguzi.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Mulala, Kata ya Songoro nyumbani kwa mgombea wa chama hicho, Nassari, Mbowe alisema: “Naomba mara baada yakupiga kura, utakaa mita 103 kutoka kwenye kituo, hadi matokeo ya kituo chako yatakapobandikwa, chukua kanga, baiskeli, punda, gari au usafiri wowote tukutane Usa River ambapo tutafanya mkesha wa kusubiri matokeo.”

Alisema uamuzi huo umechukuliwa baada ya kuwepo kwa taarifa kwamba kuna shinikizo la kumtaka Msimamizi ya Uchaguzi, Kagenzi atangaze matokeo tofauti hata kama Chadema watakuwa wameshinda.

“Ndugu zangu msigope kitu, tutakwenda kulala wote Usa River kusubiri matokeo yetu na kama wakitubia haki ya Mungu safari hii hatutakubali,” alisema Mbowe. Mbowe aliwataka polisi siku ya uchaguzi kuwaacha Chadema na CCM wachuane wenyewe kwani kazi yao ni kulinda amani na siyo kuilinda CCM.

Mapema Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema aliwataka wakazi wa jimbo hilo, wasiwena hofu ya wingi wa polisi katika maeneo yao akisema haijawahi kutokea hata siku moja bunduki ikazidi nguvu ya umma.

“Makamanda jitokezi kupiga kura kuanzia saa 12:00 jioni mkimaliza msubiri matokeo na baada ya hapo tukutane Usa River na hapo kutakuwa na makada wenzenu kusubiri matokeo.”

Katika mkutano huo, Viongozi wawili wa CCM, akiwemo Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) wa Tawi la Mulala, Eribariki Manjeka alirudisha kadi ya CCM na kujiunga na Chadema pamoja na William Nassari ambaye aliwahi kuwa Katibu Mwenezi na Itikadiwa CCM katika kata hiyo.

Mwananchi.

Kamata mwizi men!
 
Mkuu, Tume ya Uchaguzi si ipo tatizo ni nini mpaka mkakeshe?

Sasa kama ipo na huo mkesha unakuogopesha nini? Safari hii mkilazimisha damu lazima imwagike. Na tayari tumeagiza waangalizi wa kimataifa!
 
Mwenyekiti wa CDM kwa mara nyingine anachochea fujo, uchaguzi ni gemu kuna kushinda na kushindwa sasa anawahakikishia wanachama ushindi si kutafuta vurugu gu jamani. Enyi polisi tunawategemea sana wakifa watatu kama ilivyokuwa ARUSHA sio mbaya maana watz tupo zaidi ya milion 45.

Acha kupotosha. Mbowe anamaasisha wananchi wajitokeze kulinda kura. Tatizo lenu CCM mnaogopa sana umma wa wananchi. Arumeru is another TARIME ya 2008!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom