mwengeso
JF-Expert Member
- Nov 27, 2014
- 9,227
- 6,666
Leo 4/2/17 Gazeti la Mwananchi lenye habari yenye kichwa "Kauli ya JPM yaibua mjadala mzito".
Habari yenyewe ni kauli ya Rais kuhusu watu wanaowatetea wahalifu na kwamba Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) kimeingiliwa kisiasa.
Wanasheria wanaoingiza siasa kwenye chama hicho wanataka kigeuzwe kuwa na mtazamo wa kisiasa ili kiweze kupambana na Serikali, kwa kisingizio cha ati kulinda Katiba ya JMT. Kuna wanasheria wanaongoza jambo hilo na wanaandaa kufanya mapinduzi katika uongozi wa Chama.
Hayo nawaachia wanachama wenyewe wa TLS, maana Rais amelibainisha hilo na hakusita kulikemea na kutoa maagizo lichunguzwe.
Lakini, mada yangu ni kuhusu neno la Mh Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, M/kiti wa CHADEMA, chama kikuu cha upinzani, mtetezi mkuu wa mabadiliko, yakilenga kuondoa ufisadi, dhuruma na maovu katika jamii!!!!
Mh Mbowe amenukuliwa katika hilo Gazeti kuwa kasema "Kumruhusu Rais kuendelea kutoa matamko ambayo ni kinyume cha sheria ni jambo la hatari sana katika kujenga utawala bora na utawala wa kidemokrasia"!
Maswali yafuatayo nayaelekeza kwake Mh Mbowe (naamini anasoma ya JF) na wapambe wake:
1) Hivi ni kweli Rais Magufuli anatoa matamko na hayo matamko ni kinyume cha sheria?
i) Ni sheria zipi zinavunjwa?
ii) Ni demokrasia gani Mh Mbowe abaizungumzia? Naamini si inayowapa wachache kuamua hatima ya haki katika jamii!!!
2) Rais kama Kiongozi na Amri Jeshi Mkuu, anapaswa kutoa matamko gani, wakati wanaopaswa kulinda, kutetea na kutoa haki, hawafanyi hivyo ipasavyo? Arejee kisa cha mjane alitejitokeza kwenye huo mkutano.
3) Mh Mbowe, ni njia na jinsi gani ya kushughulikia maovu, pamoja na kwamba kuna vyombo na taasisi zenye dhamana hiyo?
4) Mh Mbowe, je, unakumbuka matamko ambayo umekwisha kuyatoa yenye kukanganya na kufitinisha jamii?
HAKUNA MTU MWOVU KAMA MNAFIKI NA HASA AKIWA KIONGOZI WA NGAZI KAMA MH MBOWE.
Hongera Rais Magufuli kwa ujasiri wa kuwakemea hadharani watu wanaojifanya wako juu ya sheria. Kauli zako siyo zinalinda haki za wanyonge, ambazo zinachezewa na vyombo vilivyopo kikatiba, pia zinawapa changamoto wahusika katika vyombo hivyo.