Mbowe atangaza UKAWA kutokuwa na Imani na Naibu Spika, hawatohudhuria vikao vitakavyoongozwa nae

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
[/QUOTE]

UKAWA yatangaza kutokuwa na Imani na spika, Inaandaa mchakato wa kupiga kura ya kumuondoa madarakani.

Yatangaza kususia vikao vyote atakavyo visimamia.
Kiongozi wa upinzani bungeni, Freeman Mbowe amesema naibu spika ameonyesha udhaifu mkubwa katika kuongoza bunge na tangia kipindi chote aanze kuwa mbunge yeye ndio anayefanya maamuzi ya vituko kuliko spika yoyote.

Amesema sio kwamba hawaheshimu kiti cha Naibu spika bali wanamtaka aheshimu kanuni za bunge, aheshimu mawazo ya bunge na aheshimu taratibu za kuliongoza bunge.
 
Kwani hoja ya UKAWA ni ipi hasa?

Serikali ijibu kuhusu hao wanafunzi?

Mjadala uruhusiwe Bungeni?

wanafunzi warudishwe nyumbani?

Au wanafunzi hao ambao hawana sifa za kuwa walimu wa sekondari serikali iwapeleke wapi?
Hawa wanafunzi walipelekwa chuo kwa Mujibu wa sheria na Taratibu zilizoasisiwa na bunge kamahujui uliza kwanza
 
Huyu mama aheri akae pembeni tunategemea akina Filikojombe wapya wakisign hizo karatasi apigwe chini
 
Kutoka Ujaji Kiongozi ambae ni Msaidizi Mkuu wa Chief Justice hadi ujaji wa Mahkama ya Rufani Katumbuliwa kidizaini kama ile ya DPP Feleshi kupewa Ujaji wakati wa Baba Ridh, japokuwa kwny front page itaonekana kapanda kutoka Mahakama Kuu mpaka ya Rufaa
Sidhani kama katumbuliwa
 
Yaani tatizo lililowaathiri moja kwa moja wanafunzi zaidi ya 7000, na kusababisha wengine kunusurika kubakwa, Serikali inakuja kulitolea jibu lisilozidi dakika 2..! Tena jibu ambalo limeacha maswali mengi kuliko majibu..! Huyu naibu ataleta shida sana..
 
Yaani tatizo lililowaathiri moja kwa moja wanafunzi zaidi ya 7000, na kusababisha wengine kunusurika kubakwa, Serikali inakuja kulitolea jibu lisilozidi dakika 2..! Tena jibu ambalo limeacha maswali mengi kuliko majibu..! Huyu naibu ataleta shida sana..
CCM imefeli haraka sana kwenye mambo mengi tena nyeti sana
 
Back
Top Bottom