Mbowe atangaza operesheni ''Kata Funua''

MsemajiUkweli

JF-Expert Member
Jul 5, 2012
13,172
23,974
Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.

Chanzo:Mwananchi.
 
We have been here before!

Are we still heading where Albert Einstein once said, insanity is doing the same thing over and over again, but expecting different results.

Mwaka 2008 CHADEMA iliibuka na operesheni samaki mkubwa (maarufu kama Oparesheni Sangara).

Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, kuliibuka matembezi ya maandamano.

Mwaka 2012 ikaanzishwa operation ya mabadiliko yaani Movement for Change (M4C).

Mwaka 2016, wameibuka na operesheni Ukuta (Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania) ambao wengine waliita Ukuta wa mabua na kabla ya jua kuzama, tunaambiwa kuna operesheni Kata Funua.

Halafu maneno Kata Funua ni kama ya kihuni huni au ubabe ubabe wakati siasa ni mazungumzo. Au anataka kupambana na vyombo vya dola?

Haya ndio moja ya mapendekezo ya kikao cha Kamati Kuu kilichokaa juzi! Serious?

Buckle up dude and get ready for the ride of a misfiring lifetime!
 
"Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembea kanda zote"

1. Hapa anaongelea kiongozi yupi?, wa chadema ama wa dola?

2. Kama wa chadema, ina maana kuna migomo miongoni mwao?

3. Kama wa chadema, mbona mwenyewe kaishakwamisha tayari?

4. Kama wa dola, Mbowe na group lake hawana ubavu wa kumuondoa yeyote.
 
1. Operation Sangara
2.Operation M4C tukachanga na pesa zetu chalii
3.Operation vua gamba vaa gwanda chalii
4.Operation washa taa mchana chalii
5.Operation UKUTA 01/09 chalii
6.Operartion UKUTA 1/10 chalii
7.Operation BAVICHA kuwazuia CCM wasifanya mkutano wao Dodoma Chalii
8.Operation kata funua huu ulaji mwingne
 
Baada ya kuanzisha na hatimaye kukwama kuitekeleza operesheni ya Umoja wa Kupinga Udikteta Tanzania (Ukuta), Chadema imekuja na nyingine itakayokwenda kwa jina la ‘Kata Funua’.

Operesheni hiyo mpya imetangazwa na Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ikilenga kukipa chama hicho mafanikio katika uchaguzi wa Serikali za mitaa na ule mkuu ujao.

Mbowe amesema hayo katika kikao cha uchaguzi wa mwenyekiti wa kanda wilayani Masasi mkoani Mtwara.

“Kiongozi yeyote atakayeonyesha nia ya kutukwamisha hatutamvumilia, tutamuondoa ili tuweze kuendelea na safari yetu na kumaliza kutembelea kanda zote,” amesema.

Amesema ziara hizo ndizo zitakazoipa nafasi chama hicho kuchukua maeneo mengi zaidi hasa katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2019.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema, Edward Lowassa amesema umoja na mshikamano ndiyo msingi imara utakaowasaidia kuweza kufikia malengo.

“Ili kufanikiwa lazima kuwe na umoja imara baina ya viongozi wa chama. Mtu yeyote atakayekuwa na nia mbaya na umoja huu achukuliwe hatua mara moja ili kuepuka kutokea kwa migogoro,” amesema.

Naibu Katibu Mkuu wa Chadema – Zanzibar, Salum Mwalimu amemshukuru Rais John Magufuli kwa kukipa fursa adhimu chama hicho kutokana na kuzuia mikutano ya kisiasa majukwaani jambo ambalo limewasaidia kujipanga vizuri katika uchaguzi ujao.

“Safari hii ni fursa kwetu, tumejipanga kiuhakika na si kwa kubahatisha tunapoelekea katika uchaguzi wa serikali za vijiji, vitongoji, mitaa mwaka 2019 na baadaye uchaguzi wa wabunge na Rais ifikapo 2020,” amesema.
Chanzo:Mwananchi.
Nimegundua kitu ndo mana CDM kupewa nchi ni ngumu sabb chama kimekaa kihuni sana sasa "kata funua" ndo nn....aisee nahsi mkipewa mtatuuza nyinyi acha nitaisoma namba hukuhuku niliko
.
.
.
Kyenekyaka mkighanile une
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom