Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,480
- 9,241
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia MAKINI, Ameir Hassan Ameir amemtaka mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe kuwaomba radhi baada ya kauli yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo alisema vyama vya siasa 12 vinafadhiliwa ili kukisaidia Chama cha Mapinduzi CCM na kutafuta maslahi kupitia jukwaa la siasa.
=======
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Amer Hassan amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kuwaomba radhi kufuatia kauli aliyoitoa jana kuwa Chama hiko ni miongoni mwa vyama 12 vya upinzani vinavyofadhiliwa na CCM
Akiongea na Waandishi wa Habari, Freeman Mbowe alisema "Mwenendo wa kampeni unadhihirisha kuwa Uchaguzi huu washindani ni wawili ambao ni CHADEMA na CCM, hivi vyama vingine ni vyama vinasimamiwa na vinakisaidia Chama Cha Mapinduzi kutafuta uhalali"
Amer amesema kauli hiyo sio ya kiungwana, ni tata na imewachafua kwa sababu kila Chama kina haki ya kufuata Sheria na taratibu. Amemtaka kushughulika na Kamati ya Maadili kuhusu adhabu aliyopewa Tundu Lissu ya kutofanya kampeni
Ameongeza kuwa, Mbowe amewadharau na kuwavunjia heshima kwani amejiona kwamba Chama chake ndicho kina haki ya kufanya siasa nchini.