Uchaguzi 2020 Mbowe atakiwa kuomba radhi baada ya kusema vyama vingine vya upinzani vinashirikiana na CCM

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,480
9,241
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia MAKINI, Ameir Hassan Ameir amemtaka mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe kuwaomba radhi baada ya kauli yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo alisema vyama vya siasa 12 vinafadhiliwa ili kukisaidia Chama cha Mapinduzi CCM na kutafuta maslahi kupitia jukwaa la siasa.

=======

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Amer Hassan amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kuwaomba radhi kufuatia kauli aliyoitoa jana kuwa Chama hiko ni miongoni mwa vyama 12 vya upinzani vinavyofadhiliwa na CCM

Akiongea na Waandishi wa Habari, Freeman Mbowe alisema "Mwenendo wa kampeni unadhihirisha kuwa Uchaguzi huu washindani ni wawili ambao ni CHADEMA na CCM, hivi vyama vingine ni vyama vinasimamiwa na vinakisaidia Chama Cha Mapinduzi kutafuta uhalali"

Amer amesema kauli hiyo sio ya kiungwana, ni tata na imewachafua kwa sababu kila Chama kina haki ya kufuata Sheria na taratibu. Amemtaka kushughulika na Kamati ya Maadili kuhusu adhabu aliyopewa Tundu Lissu ya kutofanya kampeni

Ameongeza kuwa, Mbowe amewadharau na kuwavunjia heshima kwani amejiona kwamba Chama chake ndicho kina haki ya kufanya siasa nchini.
 
Hili suala si geni, kuna vyama ambavyo ni mapandikizi na watanzania wanavijua kwa sura na kwa tabia. Hivi ndivyo vinatega miba kwenye njia yetu ya kuelekea kwenye UHURU, HAKI, na Maendeleo ya watu.

Ila safari hii - kinakwenda kueleweka tu.
 
Useme mumezidiwa mapandikizi. Nyie wawili CCM 12. Mapandikizi wenu ACT na CHAUMA utopolo.
 
Chama cha Demokrasia Makini Wapeleke malalamiko Tume ya maadili officially kwa hicho mbowe alichotamka ili Chadema wachukuliwe hatua officially ikiwemo kuzuiwa kufanya kampeni kama chama nchi nzima
 
Mbowe kaongea kama official msemaji mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini hilo swala pelekeni kamati ya maadili Chadema wachukuliwe hatua na mtaungwa mkono na vyama vyote vya upinzani kasoro Chadema

Msiogope Iandikieni tume ya Maadili inayoshirikisha vyama vyote for action
 
Mbowe apige magoti harakasana.
Kama huyu? NEVER!
IMG_20201001_031244.jpg
 
8 Reactions
Reply
Back
Top Bottom