Uchaguzi 2020 Mbowe atakiwa kuomba radhi baada ya kusema vyama vingine vya upinzani vinashirikiana na CCM

LIMBOMAMBOMA

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
9,116
2,000
Mbowe kasema ukweli mchungu tupu, haiwezekani waungane na ccm kumhujumu mgombea wa ukweli wa upinzani wa kweli lissu.
 
mbinguni

JF-Expert Member
Jan 2, 2013
2,513
2,000
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia MAKINI, Ameir Hassan Ameir amemtaka mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe kuwaomba radhi baada ya kauli yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo alisema vyama vya siasa 12 vinafadhiliwa ili kukisaidia Chama cha Mapinduzi CCM na kutafuta maslahi kupitia jukwaa la siasa.

=======

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Amer Hassan amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kuwaomba radhi kufuatia kauli aliyoitoa jana kuwa Chama hiko ni miongoni mwa vyama 12 vya upinzani vinavyofadhiliwa na CCM

Akiongea na Waandishi wa Habari, Freeman Mbowe alisema "Mwenendo wa kampeni unadhihirisha kuwa Uchaguzi huu washindani ni wawili ambao ni CHADEMA na CCM, hivi vyama vingine ni vyama vinasimamiwa na vinakisaidia Chama Cha Mapinduzi kutafuta uhalali"

Amer amesema kauli hiyo sio ya kiungwana, ni tata na imewachafua kwa sababu kila Chama kina haki ya kufuata Sheria na taratibu. Amemtaka kushughulika na Kamati ya Maadili kuhusu adhabu aliyopewa Tundu Lissu ya kutofanya kampeni

Ameongeza kuwa, Mbowe amewadharau na kuwavunjia heshima kwani amejiona kwamba Chama chake ndicho kina haki ya kufanya siasa nchini.
Upinzani Tz ni chadema na act wazalendo basi.

Sent using Jamii Forums mobile app
Na Chaumma ya Hashim Rungwe nao ni wapinzani wa kweli
 
sweettablet

JF-Expert Member
Nov 16, 2014
7,450
2,000
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia MAKINI, Ameir Hassan Ameir amemtaka mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Freeman Mbowe kuwaomba radhi baada ya kauli yake aliyoitoa mbele ya waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam ambapo alisema vyama vya siasa 12 vinafadhiliwa ili kukisaidia Chama cha Mapinduzi CCM na kutafuta maslahi kupitia jukwaa la siasa.

=======

Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia Makini, Amer Hassan amemtaka Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe kuwaomba radhi kufuatia kauli aliyoitoa jana kuwa Chama hiko ni miongoni mwa vyama 12 vya upinzani vinavyofadhiliwa na CCM

Akiongea na Waandishi wa Habari, Freeman Mbowe alisema "Mwenendo wa kampeni unadhihirisha kuwa Uchaguzi huu washindani ni wawili ambao ni CHADEMA na CCM, hivi vyama vingine ni vyama vinasimamiwa na vinakisaidia Chama Cha Mapinduzi kutafuta uhalali"

Amer amesema kauli hiyo sio ya kiungwana, ni tata na imewachafua kwa sababu kila Chama kina haki ya kufuata Sheria na taratibu. Amemtaka kushughulika na Kamati ya Maadili kuhusu adhabu aliyopewa Tundu Lissu ya kutofanya kampeni

Ameongeza kuwa, Mbowe amewadharau na kuwavunjia heshima kwani amejiona kwamba Chama chake ndicho kina haki ya kufanya siasa nchini.
Tumeishasema sana humu Chadema ni cha watu wabinafsi, wana roho mbaya, wajinga, wapumbavu na watu wanaofikiri wao tu wajuaji. Ikitokea wakaota wanatawala nchi hii, tutakuwa zaidi ya Belarus!!
 
GeoMex

JF-Expert Member
Jan 10, 2014
5,362
2,000
CHAUMA pia tuko jikoni tunaandaa tamko.

#ubwabwa kwa wote.

Aiseee utawasema wapinzani uchwara wooote ila usimuweke kwenye hilo kundi mzee Rungwe

Yule chama chake ni cha kikatuni tu na kwamba anapenda kuonekana kwenye ballot paper ila hawezekani kuwa kundi moja na CCM kamwe
 
900 Inapendeza zaidi

JF-Expert Member
Nov 19, 2017
3,952
2,000
Chama cha Demokrasia Makini Wapeleke malalamiko Tume ya maadili officially kwa hicho mbowe alichotamka ili Chadema wachukuliwe hatua officially ikiwemo kuzuiwa kufanya kampeni kama chama nchi nzima
kuna kitu mnakitafuta kwa chadema na Lisu nahuyo mahera wenu na hamtakipata hadi siku ya oct28 tutakapowafurumusha kupitia box la kura
 
kamtesh

JF-Expert Member
Jul 26, 2014
1,396
2,000
Mbona ipo wazi jameni? Kuna mambo watanzania tunakua wanafiki kweli? Macho nyanaona lakini kwa maksudi tunajifanya sio kweli? Pretenders!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom