Daimler
JF-Expert Member
- Sep 11, 2018
- 556
- 973
Gazeti la Fahari Yetu limeandika tuhuma dhidi ya Mwenyekiti wa CHADEMA na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe, likimhusisha na matumizi ya milioni 800 za ujenzi wa jengo la ghorofa la Ofisi za Makao Makuu ya Chama hicho, Mtaa wa Ufipa, Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Gazeti hilo limedai kuwa, Mbowe alikiuka Azimio la Kikao cha Kamati Kuu ya Chama na kuamua kutumia fedha hizo kwa matumizi yake binafsi. Inaelezwa kuwa:
- Mbowe alinunua nyumba Dubai kwa fedha za Chama.
- Michango ya watu binafsi kwa Chama kama akina Mzee Sobodo haijulikani zilichukuliwa lini na kwa mfumo gani na hatimaye kutumikaje.
- Fedha zilizopatikana kupitia "Fund Raising Events" mbalimbali kama za Dar na Mwanza hazijawahi kuonekana.
- Malalamiko kwa Mbowe kujilipa fedha kwa mnadai ya kukikopesha milioni Chama milioni 700.
- Malalamiko dhidi ya Mbowe kukiuzia Chama magari chakavu kwa zaidi ya milioni 600 ambapo kabla ya kuyauza kwa Chama, alikuwa akiyakodisha kwa Chama.
- Malalamiko kwa Mbowe kununua LandCruiser V8 VX 2 kwa pesa za Chama na kisha kukiuzia Chama.
- Ripoti ya CAG ya 2016/2017 imeonyesha namna fedha za CHADEMA zinavyotafunwa na wajanja wachache.