Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 13
FFU wamimina mabomu ya machozi Msafara wa Freeman Mbowe Busanda
2009-04-22 21:49:48
Na Joseph Mwendapole
Polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), wamefyatua mabomu ya machozi kuwatawanya mamia ya watu waliojitokeza kumlaki Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, kwenye stendi ya mabasi ya Kataro, Jimbo la Busanda mkoani Mwanza.
Tukio hilo lilitokea majira ya 12:30 jioni juzi kilomita mbili kabla ya kufika eneo la stendi hiyo, ambako wakazi hao walisukuma gari la Mbowe, lakini mwenyewe alilazimika kuteremka na kutembea kwa miguu umbali wa kilomita moja.
Huku wakiimba kibwagizo cha `Mbowe, Mbowe,` umati mkubwa wa watu ulizidi kumiminika katika stendi hiyo, hali ambayo iliwafanya polisi kuwataka wakazi hao watawanyike huku wakifyatua mabomu ya machozi kwa lengo la kuwatawanya.
Polisi walikuwa wakiwataka wakazi hao kutawanyika kwa vile hapakuwa na mkutano wa hadhara ulioruhusiwa kufanyika.
Hata hivyo, wakazi hao waligoma kutawanyika, hadi watakapomwona Mbowe.
Akiwa jukwaani, Mbowe aliwaambia polisi kwamba hawakuwa na lengo la kufanya mkutano, isipokuwa walitaka kuwasalimia wananchi waliofurika kuwapokea.
Akiwasalimia wananchi hao, Mbowe alisema Jimbo la Busanda litakuwa kama lilivyokuwa Jimbo la Tarime, ambalo Chadema kilishinda katika uchaguzi mdogo wa ubunge na kukibwaga Chama Cha Mapinduzi (CCM) kilichokuwa mshindani wake mkubwa.
Wakati akitoa salamu hizo, mamia ya wananchi walikuwa wakiitikia kwa sauti kubwa ya ndiyo, ndiyo kama ishara ya kumuunga mkono, huku wengine wakiimba CCM imeuza jimbo hilo.
Mbowe alisema mchuano wa Chadema na CCM katika jimbo hilo ni kama timu za mpira za Manchester United na Liverpool za Uingereza.
Aidha, aliwataka polisi kufanya kazi kwa mujibu wa sheria na kanuni za jeshi hilo na sio kuisaidia CCM katika harakati zake za kuwania ubunge katika jimbo hilo.
SOURCE: Nipashe

Last edited by a moderator: