Mbowe angefungwa zamani sasa hivi Upinzani Ungekuwa Umeshakufa. Na hii ndio namna Bora ya kutumia Akili kuzuia Jambo kuliko nguvu

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
Kama Mbowe angekuwa nje huo Moto wa Katiba Ungekuwa mkubwa sana na sijui nani angeuzima.

Mbowe ndie kiongozi pekee anayeweza kuubeba upinzani. Kwanza anabusara, Anaweza kuvumilia wanachama wake wanaokosea. Alishamtetea Zitto Mara kaadhaa.

Kuongoza upinzani Afrika na ukasimama ni zaidi ya kuwa Raisi. Unaongoza wasaliti, Viburi na wakosoaji haswa. Ukiteleza kidogo wanakumwaga. Muulize Mrema, Jemsi Mapalala, Sheif Sharif au Mabele Malando. Utawala uliopita ulikosea kutaka kuufuta upinzani wakati kiongozi wao yupo nje.

Hii ni hatua muhimu.
 
Kwa tafsili hii kusitegemee Mbowe kuachiwa ivi karibuni na hii itakuwa ndo mipango ya kuudhohofisha upinzani hapa nchini.....🤔

Siamini ila ngoja tuone maana siasa ni mchezo mchafu.
 
Kama Mbowe angekuwa nje huo Moto wa Katiba Ungekuwa mkubwa Sana na sijui Nani angeuzima.

Mbowe ndie kiongozi "PEKEE" anayeweza kuubeba upinzani. Kwanza anabusara, Anaweza kuvumilia wanachama wake wanaokosea.

Kama haya unayoongea ni kweli kuwa Mbowe ndio kiongozi "PEKEE" anaeweza kuubeba upinzani. Hii inamaana kuwa kina Lisu, Mnyika, Prof Safari, Mwalim na viongozi wengine hawana uwezo wa kuongoza chama au upinzani, pia hawana busara na uvumilivu kama alio nao Mbowe. Yani wao wapo kwa ajili ya kuongozwa tu na Mbowe miaka yote.
 
Kwa tafsili hii kusitegemee Mbowe kuachiwa ivi karibuni na hii itakuwa ndo mipango ya kuudhohofisha upinzani hapa nchini.....🤔

Siamini ila ngoja tuone maana siasa ni mchezo mchafu.....
☺️☺️☺️
 
Mbowe atafungwa na upinzani utaendelea kuwepo.

Walikuwepo kina:
Masumbuko Lamwai
Mabere Marando
Bob Makani Dr. Silaa
Warid Kabourou
Waitara
Silinde
Lijuakali
Lwakatare
N.k
Wote hawa hawapo na upinzani upo.

Upinzani upo kwenye mioyo ya watu.

Wakati wa kampeni Tundu Lisu alienda Chato na akapokelewa kwa kishindo. Magufuli hakuamini macho na masikio yake!
 
Kuna kitu atafanya Chief Hangaya week hii kuhysu Mbowe tusiache maombi
 
Kama haya unayoongea ni kweli kuwa Mbowe ndio kiongozi "PEKEE" anaeweza kuubeba upinzani. Hii inamaana kuwa kina Lisu, Mnyika, Prof Safari, Mwalim na viongozi wengine hawana uwezo wa kuongoza chama au upinzani, pia hawana busara na uvumilivu kama alio nao Mbowe. Yani wao wapo kwa ajili ya kuongozwa tu na Mbowe miaka yote.
Mwalimu mwenyewe kaishasanda, wanaopatanisha Bei wamekamilisha Kazi zamani uongozi upinzani NI kipaji. Yuko wapi Julius Mtatiro
 
Mbowe atafungwa na upinzani utaendelea kuwepo.

Walikuwepo kina:
Masumbuko Lamwai
Mabere Marando
Bob Makani Dr. Silaa
Warid Kabourou
Waitara
Silinde
Lijuakali
Lwakatare
N.k
Wote hawa hawapo na upinzani upo.

Upinzani upo kwenye mioyo ya watu.

Wakati wa kampeni Tundu Lisu alienda Chato na akapokelewa kwa kishindo. Magufuli hakuamini macho na masikio yake!
Na ujue tu bila Mbowe sasaivi UPINZANI ungashaisha. Wote uliowataja walizimwa Kama taa ya umeme ndo. Ila Mbowe kaanzia nyuma Hadi Leo yupo juu
 
Infact ni kuwa Mbowe amekuwa nguzo muhimu ya utulivu na amani ya nchi hii.

Kumuondoa Mbowe ktk equation, ni kuweka ombwe linaloweza kujazwa. na nguvu hasi wasiyoweza kuithibiti.

Mbowe alikuwa anastaafu next two years, kwa hiyo Chadema ingeendelea tu bila hata uwepo wake
 
Kwa tafsili hii kusitegemee Mbowe kuachiwa ivi karibuni na hii itakuwa ndo mipango ya kuudhohofisha upinzani hapa nchini.....🤔

Siamini ila ngoja tuone maana siasa ni mchezo mchafu.
Hakuna siku moja anayolala mbowe ndan ambayo watoto wa aliefumbiaacho hatolala siku 5
 
Kuna mambo ya kukubali tu katika uzi huu, ni kweli Mbowe amekuwa ni mmoja kati ya wanasiasa wenye busara katika bara la Afrika, aliamini katika siasa za makaratasi, tofauti na wanasiasa wengine pindi matokeo yakitangazwa na chi zinaharaibika, tukubali tu kuwa ana busara ya aina hiyo hata kama tupo tofauti nae kisiasa.
Utofauti wa kisiasa bado hamnyimi mtu hadhi yake ya kupewa sifa anayostahili
 
Kama Mbowe angekuwa nje huo Moto wa Katiba Ungekuwa mkubwa sana na sijui nani angeuzima.

Mbowe ndie kiongozi pekee anayeweza kuubeba upinzani. Kwanza anabusara, Anaweza kuvumilia wanachama wake wanaokosea. Alishamtetea Zitto Mara kaadhaa.

Kuongoza upinzani Afrika na ukasimama nI zaidi ya kuwa Raisi. Unaongoza wasaliti, Viburi na wakosoaji haswa. Ukiteleza kidogo wanakumwaga. Muulize mrema, Jemsi Mapalala, Sheif Sharif au Mabele Malando. Utawala uliopita ulikosea kutaka kuufuta upinzani wakati kiongozi wao yupo nje.

Hii NI hatua muhimu.5
Wewe katekeleze msemo wa aliekua Dc wa Iringa then njoo tena, yani KWa fikra zako Mbowe akifungwa na upinzani unakufa?

Sikia Chadema imepika watu na ina watu na ipo Sana kuliko jana, nyakati hazipo upande wa CCM Hata mkimfunga
 
Kama Mbowe angekuwa nje huo Moto wa Katiba Ungekuwa mkubwa sana na sijui nani angeuzima.

Mbowe ndie kiongozi pekee anayeweza kuubeba upinzani. Kwanza anabusara, Anaweza kuvumilia wanachama wake wanaokosea. Alishamtetea Zitto Mara kaadhaa.

Kuongoza upinzani Afrika na ukasimama nI zaidi ya kuwa Raisi. Unaongoza wasaliti, Viburi na wakosoaji haswa. Ukiteleza kidogo wanakumwaga. Muulize mrema, Jemsi Mapalala, Sheif Sharif au Mabele Malando. Utawala uliopita ulikosea kutaka kuufuta upinzani wakati kiongozi wao yupo nje.

Hii NI hatua muhimu.5
Kosa kubwa wanalolifanya makada wa CCM ni kudhania ya kuwa kudhoofisha vyama makini vya ushindani ndiyo salama pekee kwao kubakia madarakani. Leo hii wanaona ni fahari sana kupindisha sheria na hata kutumia vibaya vyombo vya dola ili kuthibiti shughuli za vyama vya kisiasa ndiyo njia muafaka kwao kupata mafanikio.

Hawatambui kuwa wimbi la mabadiliko siku zote huletwa na watu wala si vyama vya kisiasa. Watu hawa wanaweza wakawepo ndani ya CCM yenyewe na kutoridhishwa na jinsi mambo yanavyokwenda ndani ya chama chake na serikalini, ama wakatoka nje ya CCM.

Suala ni kupatikana kwa mtu sahihi na mwenye kuaminika ambaye anaweza kuanzisha na kuhamasisha "renaissance" mithili ya hili hitaji la wakati la katiba mpya. Itafika tu wakati vyombo vya dola vitajitenga na CCM, nayo itajikuta haina hoja mbele ya umma wa Watanzania isipokuwa lawama kedekede dhidi yake.

Itakuwa ni kama nguvu ya Man United pale ilipokuwa chini ya Sir Ferguson, na sasa imegeuka kuwa kibonde na hata kula mkono kutoka kwa wapinzani wao Liverpool. Hata watani zangu Simba a.k.a mikia wanajua ukweli ya kwamba meza hupinduliwa
Screenshot_20211025-072250.jpg
 
Kama Mbowe angekuwa nje huo Moto wa Katiba Ungekuwa mkubwa sana na sijui nani angeuzima.

Mbowe ndie kiongozi pekee anayeweza kuubeba upinzani. Kwanza anabusara, Anaweza kuvumilia wanachama wake wanaokosea. Alishamtetea Zitto Mara kaadhaa.

Kuongoza upinzani Afrika na ukasimama nI zaidi ya kuwa Raisi. Unaongoza wasaliti, Viburi na wakosoaji haswa. Ukiteleza kidogo wanakumwaga. Muulize mrema, Jemsi Mapalala, Sheif Sharif au Mabele Malando. Utawala uliopita ulikosea kutaka kuufuta upinzani wakati kiongozi wao yupo nje.

Hii NI hatua muhimu.5
Mawazo ya kijinga kabisa.
Huwezi mnyamazisha mtu mmoja na wengine wakanyamaa.
Mawazo ya kipolisi haya!
 
Kama Mbowe angekuwa nje huo Moto wa Katiba Ungekuwa mkubwa sana na sijui nani angeuzima.

Mbowe ndie kiongozi pekee anayeweza kuubeba upinzani. Kwanza anabusara, Anaweza kuvumilia wanachama wake wanaokosea. Alishamtetea Zitto Mara kaadhaa.

Kuongoza upinzani Afrika na ukasimama nI zaidi ya kuwa Raisi. Unaongoza wasaliti, Viburi na wakosoaji haswa. Ukiteleza kidogo wanakumwaga. Muulize mrema, Jemsi Mapalala, Sheif Sharif au Mabele Malando. Utawala uliopita ulikosea kutaka kuufuta upinzani wakati kiongozi wao yupo nje.

Hii NI hatua muhimu.5
Kwani Hayati Mandela alipofungwa na makaburu miaka 27, ANC ilikufa?
 
Back
Top Bottom