Mbowe Anaweza kutuliza hii Gharika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mbowe Anaweza kutuliza hii Gharika

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mbogela, Dec 4, 2009.

 1. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #1
  Dec 4, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 145
  Wakati muda muafaka wa kujadili hoja za maana kulekea 2010, hoja kama kuwa na tume huru ya uchaguzi, hoja kama kupunguza matumizi ya kijeshi/polisi kwenye zoezi la upigaji kura na kutisha wanachi, hoja kama kuwa na wagombea binafsi, hoja ya kupima mafanikio ya serikali iliyopo madarakani toka 2005 na udhaifu wake, naona hoja za kujadili watendaji wa CHADEMA na CHADEMA yenyewe zimeshika kasi. Inawezekana ni msimu lakini ypote yatapita.

  Na mimi naingia katika mkumbo huo wa kuendeleza kujadili watendaji wa CHADEMA na CHADEMA. Kuna swali najiuliza sana, haya maneno yote na mtikisiko tunaosikia huku nje, Je ni kweli huko ndani ya CHADEMA kuko hivyo? Maana watu waliokaribu na uongozi wa CHADEMA mara kadhaa wametokea na kutoa kauli kali zinazoonyesha kutofauatiana kati ya kiongozi na kiongozi na wengine tunaposikia kitu kama hicho tunaaamini kuna ufaa.

  Shida inayoniandama mimi ni kuamua nani ni tatizo (na sio nini tatizo) kati ya Mh. Zitto na Mh. Mbowe? Zitto analaumiwa kwa kusaidia upinzani (NCCR-Mageuzi) kuua upinzani (CHADEMA). Pia kitendo chake cha kutaka kujipima ubavu na m/kiti wake kilimuweka kwenye wakati Mgumu sana na chama chake. Wao wanasema yalihaisha, walishasolve na sasa wanasonga Mbele. Najiuliza haya maneno tunayoendelea kuyasikia huku nje yanatoka wapi?

  Lakini lililonishangaza zaidi ni namna gazeti la Tanzania Daima, gazeti linalomilikiwa na mwenyekiti wa CHADEMA freeman Mbowe linavyozidi kumshambulia Zitto kwa makala zake za hivi karibuni. Waandishi wa Tanzania Dima wapo huru kiasi gani? Je hakuna Influence ya bosi wao yaani mmiliki (Mh. Mbowe)?

  Kwasababu kama kuna influence why Mbowe hawashauri hawa waandishi na wahariri kuachana na habari za Zitto kwani hakitendei haki Chama, kwani wanazidi ku-fuel mgogoro ambao haupo (kwa mujibu wa kauli zaoiongozi waandamizi wa CHADEMA), hata kama mbowe hana uwezo wa kuinfluence Tanzania Daima, kwanini asitoe kauli (msimamo wa wazi) kuonyesha kuwa haungi mkono tabia za kumuona naibu katibu mkuu wake ni msaliti? Haungi mkono matamshi ya baadhi ya watu kukihusisha CHADEMA na kumtuhumu Zitto kushirikiana na mafisadi, Haungi mkono kumuona Zitto ni mchanga wa kisiasa, haungi mkono kumuona Zitto ni mtovu wa nidhamu mpaka hapa baadaye atakapojiridhisha kama mwenyekiti atasema vinginevyo. Kwanini Mbowe hasemi lolote anaacha haya yaendelee??

  Kama kweli Zitto ni tatizo na Mbowe anakubali kuwa Zitto ni tatizo na hachukui hatua zozote za makusudi kumuwajibisha, basi sioni Tofauti kati ya Mbowe na JK. Kwani kama ambavyo JK anawalea wachafu wengi ndani ya chama chake ndivyo Mbowe anavyofanya na Zitto. Kwa vile JK ni m/kiti wa chama na Mbowe vivyo hivyo, basi sioni utofauti wowote wa kiutendaji na kiuwajibikaji kati ya CHADEMA na CCM.

  oooh Mungu wangu watanzania Tukimbilie wapi sasa????? Kama wale wanalea mafisadi na hawa wanalea watovu wa nidham ni kwasababu tu hawa wanaolea watovu wa nidhamu hatujawakabidhi resources, siku tukiwapa dola wakatawala na kucontrol uchumi, basi tutegemee kuona mafisadi wakilelewa kama wanavyokumbatiwa wakati huu pia. Tutegemee kauli za Kibanda (wakati huo akiwa mkurugenzi wa habari Ikulu) zikiwa kali na za kashfa kwa akina MMJJ na watakapoitwa wambeya na wafitini, kauli chafu na zenye dharau kuliko kauli za Salva wa sasa.

  Naamini Mbowe anakosa busara kama anafurahia kuona kifo cha Zitto kisiasa (ambaye naamini kabisa hawezi kufa kirahisi namna hiyo), kwani lazima akubali kuwa Kifo cha Zitto kisiasa kinaweza kisiiue CHADEMA lakini kitaipa majeruhi kiasi Fulani. Na majeruhi haya ukiangalia kwa mwenendo wa siasa za Tanzania huwa hayaponi haraka. Majeruhi haya yatabakiza historia ya kuwa tulikuwa na CHADEMA yenye nguvu kwa wananchi bila wabunge, CHADEMA iliyoimbwa na vijana lakini hawakuiamini kuipa haki ya kushika dola.

  Ni kweli Mbowe huwezi kuamka na kuamuru upepo unaovuma vibaya unaokipiga chombo chako baharini ili ukipindue utulie? Huwezi kusimamisha bahari ili watu unaowatoa kwenye nchi ya utumwa wavuke salama kwenda nchi ya ahadi? huwezi kuliamuru jua kusimama kwani vita unayopigana sio vita yako, ni vita ya watanzania, na nilazima washinde vita kabla jua halijazama maana giza li karibu na likiingia maadui watajificha hatuwezi kuwaona na kuwaangamiza??? Kweli huwezi kabisaaa? Haki ya mungu tena, yaani siamini, Haizwezekani kabisaa kabisa??? Ooooh Mungu wee ni nani ataiokoa nchi hiii??????
   
Loading...