Mbowe anasaka "Kiki" kwa jina la Zitto?

Dotto C. Rangimoto

JF-Expert Member
Nov 22, 2012
1,986
1,282
kiki,.jpg

Hivi tafasiri sahihi ya neno kufilisika ni kudaiwa au kushindwa kulipa madeni kwa ukosefu wa fedha? Kama kudaiwa ni kufilisika basi hata Marekani imefilisika.

Zitto anayedaiwa na Mbowe aliyetupiwa virago kwa kushindwa kulipa deni NHC nani kafilisika? Hivi, Mbowe anayeshindwa kuwalipa wafanyakazi wake wa Tanzania Daima mishahara na Zitto nani aliyefilisika???? Mbowe aliyeuza chama kwa Lowassa na Zitto wetu nani aliyefilisika?

Ama kufilisika ni kukosa mbinu au wazo jipya katika kuongoza taasisi? Kama ndivyo, kati ya Mbowe anayeishi na kuongoza chama kwa kutegemea "kiki" kama Shilole na Zitto anayekiongoza chama kichanga na chini yake kimepata mafanikio makubwa kuliko hata vyama vikongwe nani kafilisika???

Mbowe sasa anaishi kwa kutegemea "kiki" tu, lakini hana jipya na juhudi zake zimefikia ukomo, Mbowe kafilisika si kifedha tu, lakini pia kimawazo, kiakili na kimbinu.

Kwa juhudi zake CHADEMA imepaa, hakuna abishaye hili, na kwa kufikia ukomo wa upeo wake CHADEMA inaporomoka,

Niseme tu, hili si langu, ni sayansi, kila mtu ana upeo na uwezo wake, na vyote hivyo vina ukomo wake, mtu akifikia ukomo kinachofuata ni kushuka na hatimaye hufa kabisa!

CHADEMA imekuwa kwa uwezo wa Mbowe, lakini sasa Mbowe kafikia ukomo wa kimaono na kufikiri, na kwakuwa kafikia ukomo hana kitu kipya, na kwakuwa hana kipya atajitutumua tu, ili aonekane bado wamo, kumbe wapi, jua liko magharibi na lataka kuzama. Hivi walioweka kitu kinachoitwa ukomo wa kuongoza walikuwa wajinga? Hapana, kuna wakati tasisi inahitaji mawazo na fikra mpya, ingawa misingi ya taasisi itabaki ileile.

Mbowe anaishi kwa "kiki"? CHADEMA sasa yaishi kwa "kiki"? CHADEMA imekosa fikra na mawazo mapya? Jawabu ndio, Mbowe anaishi kwa "kiki" na CHADEMA yastiriwa na "kiki" haina kitu kipya!

*Kumchafua Lowassa ilikuwa "kiki"

Walimchafua Lowassa kwa miaka minane kwa minajili ya kupata "kiki" na wakamsafisha Lowassa kwa siku moja kwa minajili ya kupata "kiki" pia. Hawa watu wanaishi kwa "kiki" hawana jipya!

*Kumchukua Lowassa ilikuwa "kiki"

Chama kinapojiandaa kwenda kwenye uchaguzi mkuu kinaenda chini ya mpango mkakati wa chama. Uchaguzi wa mwaka 2015 aidha CHADEMA haikuwa na mpango au uliwacha mpango wake wa uchaguzi na kufuata "kiki"

Ni hatari kwa chama kwenda katika uchaguzi bila ya mpango madhubuti, lakini ni hatari zaidi kwa chama kuacha mpango wake inaoujua, kuuandaa na kutekeleza kwa muda mrefu na kisha kufuata "kiki" badala ya mpango wake!

CHADEMA ilimchukua Lowassa ili ipate "kiki" ya kutajwa na kuzungumzwa sana. Mbowe anaamini, jina la CHADEMA likiwa katika kurasa za mbele za magazeti basi ndio kukua kwa chama hata kama litatajwa vibaya!

Kubadili gia angani ilikuwa ni kuacha mpango wa chama na kisha kushobokea "kiki" na jambo hili hufanywa na mtu aliyefilisika tu!

*Walimkorofisha Slaa pia kwa kusaka "kiki"

Pamoja na kwamba Slaa alishiriki katika mazungumzo ya kumpokea Lowassa, lakini aliweka masharti na utaratibu mzuri kabisa ambao usingeupa chama gharama ya kumsafisha Lowassa, utaratibu ambao ungekifanya chama na viongozi wake wasivae joho la unafiki!

Taratibu hizo ni pamoja na Lowassa kuitisha mkutano wa vyombo vya habari kabla ya kujiunga na CHADEMA na kusema kinagaubaga jinsi asivyo husika na Richmond, ajabu, Lowassa hivyo hakufanya na Mbowe akajivisha kibwebwe cha kumpokea Lowassa huku akiimba nyimbo za kumsafisha, yenye kibwagizo cha "nendeni mahakamani"

Wakiulizwa jamani vip kuhusu Richmond, wote kwa ukali, Lowassa na Mbowe, wanajibu huku wakibana pua "mwenye ushahidi aende mahakamani" . Hivi kwa miaka nane mfululizo waliposema Lowassa fisadi, Mbowe na watu wake walikuwa hawajui mahakama zilipo? Walikuwa wanajua sana zilipo, ila walichokuwa wanakifanya kwa miaka yote nane ilikuwa ni "kiki".

Slaa akajiuzulu ukatibu mkuu, na akafanya press, na kwa kufanya hivyo, aidha kwa kujua au pasina kujua, akawa amefanikisha lengo la Mbowe aliyefilisika, si lingine, bali ni "kiki" Naam, ni "kiki" siku hiyo ya press na siku zilizofuata mitandaoni na magazeti yote ni habari ni CHADEMA.

Wiki hizi zote za mwisho wa mwezi uliopita na mwanzo wa mwezi huu, vyombo vya habari zinapambwa na habari Makonda, Magufuli, Hapi, Gambo, na habari za Faru John.

Mbowe akaona ujinga, akawaza "mbona chama hakitajwi na mimi siandikwi sana huko mtandaoni na kwenye magazeti" Alichofanya sote tunakijua. Kafanya mambo mawili makubwa.

Pili, akaenda kumsulubu Sosopi na kumteua Msigwa kuwa Mwenyekiti wa kanda. Sababu alizozitoa kwa wehu alioufanya ati "Tumekata jina la Sosopi kwa maslahi mapana ya chama, na tumeweka jina la Msigwa apigiwe kura ya ndio/hapana kwa maslahi ya mapana ya chama"

Maslahi gani zaidi ya kutaka chama chake kiwe ajenda kwenye mitandao na magazeti? Au kuwa ajenda katika mitandao ni maslahi?

Kando ya hayo, kama Msigwa ni maslahi kwa chama kanda Nyasa kwanini walimuacha Sosopi na wengineo wachukue fomu na wajiandae kwa uchaguzi? Kwanini wasingesitisha uchaguzi kwa maslahi ya chama? Kumbe yote hii ni "kiki", naam ni "kiki" Mbowe mzee wa "kiki" kafilisika hana jipya!

*Sakata la Lema na Mkewe pia "kiki"

Nani asiyejua? Na nani mwenye kubisha kuwa siasa za Arusha sasa hivi amezitawala Mrisho Gambo? Jina la Lema linapotea, na Mrisho hatafuti "kiki" bali anachokifanya wananchi wanaona na wanakikubali, na sasa wananchi wa Arusha wanajua kuwa CHADEMA hawana jipya zaidi ya VURUGU na MATUSI!

CHADEMA wakaona kuwa Gambo ataimarisha nguvu ya CCM Arusha, na badala waje na mbinu mbadala kama chama, kama kawa, chini ya uongozi wa mtu aliyefilisika, asiyekuwa na kipya, wakalala, kisha wakaamka na "kiki" ipi? Rais Magufuli atakufa! nimeota! sijui nimepata maono, anajua mwenyewe huyo

Kwakuwa chama kinaamini juu ya "kiki" Lema akaambiwa na Mbowe amtabirie kifo rais, kama haitoshi mke wa Lema akaambiwa amtukane Mkuu wa mkoa wa Arusha kwa kumuita "shoga" Sasa hivi ni habari za Lema na Mkewe na CHADEMA kwa ujumla kuhusu kesi hiyo ndio zinabamba katika siasa za Arusha.

Walivyo wajinga sasa, wakati Gambo atajwa kwa mazuri Arusha, wao wanatajwa kwa lugha za chafu na zisizo na maadili huko Arusha, watu hawa wako tayari hata wafanye mapenzi hadharani ili mradi tu wapate "kiki". Kwani Mbowe kumnyonya mate mke wake hadharani ilikuwa nini kama si "kiki" pia?

MWENYEKITI WA CHADEMA AMLA DENDA MKEWE! hapo wameshatajwa, ikawa jioni, ikawa asubuhi, siku ikapita!

Kumsakama Zitto pia ni "kiki"

Gazeti Tanzania Daima ni gazeti la Mbowe na halina tafauti na gazeti la Uhuru. Kumsema Zitto kafilisika ni maelekezo ya tu ya Mbowe katika kale kamtindo chake cha kusaka "kiki"

Wanataka Zitto ajibu, wanataka Zitto aitaje CHADEMA, wanataka Zitto amtaje japo mwenyekiti wao, wanatafuta "kiki" kupitia jina la Zitto. Uzuri Zitto huwa hawapi watu "kiki" sababu yeye hujibu masuala ya msingi na katu hawezi kujitia katika malumbano yenye lengo la kusaka "kiki" Zitto Z Kabwe anajua, "kiki" hutumiwa na watu waliofilisika kisiasa au wasanii muziki na filamu ili wapate soko za kazi zao.

MWISHO.
Nimeandika haya, najua watakuja huku wamebana pua, "ACT inashambulia upinzani" yaani hawa watu ni halali kwao kutusema na kutusakama sisi, ila sisi tukiwajibu si sawa kisa wao ndio wapinzani,

Tabia ya kukandamiza demokrasia ni tabia ya CCM, sasa inapofanywa na chama cha upinzani ni sawa kukiita chama hicho kama chama upinzani? Nafikiri jina linalowafaa ni muhimili wa SHETANI.

Kila kitu "K" hata "kiki" nayo "K"

Dotto Rangimoto Chamchua.
Call/whatspp 0622845394 DSM
 
View attachment 450924

Umetumia nguvu kubwa sana kumtetea Zitto sidhani hata kama ni mwanafamilia yako ungeweza kutumia hata robo ya nguvu hii kumtetea
 
Dotto Rangimoto unatafuta "kiki" kwa kumsema Mbowe? Haya bwana! Nasikia Mchange ameshawakimbia? Mpka mbaki wakuhesabu kwenye vidole vya mikono!
 
Mzungumzieni na Nassari.....kunya anye kuku akinya bata kahara
 
kwanini umeshindwa kuangalia legacy ya gazeti ukaitofautisha na mbowe as a person?
kwani kila kinachofanyika ktk gazeti kina mkono wa mbowe?
Tanzaia Daima ni chombo chenye utaratibu wake wa ufanyaji kazi na wahariri wake, sasa inakuwaje kila kitu umemtwisha mbowe kama vile yeye ndiye mhariri mkuu.
kuwa mmliki haina maana ya kuwa ndio mtendaji. Hapo mbowe hausiki, umemuonea bure
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom