Mbowe anapwaya sana kama kiongozi wa upinzani

Bwahahahaaaaa......sijawahi kuwa mwanamagamba hata siku moja. Nachukia wanafiki na nauchukia unafiki. Mlitaka mbowe aseme nini leo bungeni? Mbona hamjibu hilo?

Unataka mpka nicopy michango yako kwenye thread zangu ndo ujue tuna takwimu??????????
 
Kwa kuwa siyo Kiongozi wa Kambi, kazi hiyo tunataka aifanye yeye. Acheni kuassume mambo. Hatufanyi hivyo CDM only CCM
Dont criticize if you dont have alternalives. Ukiishi kwa kukosoa kosoa tu kila siku utablock kufikiri kwako. Na ndio athari niionayo kwako. Mbowe ameuliza ishu ya umeme leo kwa sababu wana ccm na wasio wana ccm wanaathirika sana. Nyie mnasema kwa kuuliza hilo swali amepwaya ndio nikauliza mtu anapwaya kwa kuuliza maswali tu? Hamjajibu, nikauliza tena, mlitaka aulize swali gani, hamjibu mnaandika porojo tu. Nendeni mkajiandae mje na hoja iliyoshiba sio mnaleta hoja ambazo hata nyie wenyewe kuzitetea mnashindwa
 
Nadhani tuchukue historia ya CDM ndipo tutathmini uwezo wake. Sidhani kama maswali bungeni yanaweza kuleta tofauti sana hasa yanapotolewa na upande wa upinzani. Mbowe alipoanza kuwa mwenykiti wa CDM ilikuwa katika hali gani? Vipi ubunifu wake wa Operation Sangara ulifanukiwa kiasi gani? Maendeleo ya CDM chini ya uongozi wake yamekuwaje? Je ni mikiki mikiki mingapi amekutana nayo katika uongozi wake na ameishinda?

Kwangu mimi CDM tuna mwenyekiti imara, jambo ambalo wana magamba wasingependa kulisikia, CDM iko juu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Mambo ya mjengoni si tahmini ya kweli ya utendaji wa Mwenyekiti wetu.

MBOWE songa mbele baba mpaka kieleweke.
 
Anarudia kuuliza kuhusu swala la umeme kwa sababu umeme tanzania umekua janga la taifa na bado halijapatiwa solution. Sasa kama utakua ujajivua ufahamu ni lazima uone umuhimu wa maswali ya Freeman.
Think critically.
 
Dont criticize if you dont have alternalives. Ukiishi kwa kukosoa kosoa tu kila siku utablock kufikiri kwako. Na ndio athari niionayo kwako. Mbowe ameuliza ishu ya umeme leo kwa sababu wana ccm na wasio wana ccm wanaathirika sana. Nyie mnasema kwa kuuliza hilo swali amepwaya ndio nikauliza mtu anapwaya kwa kuuliza maswali tu? Hamjajibu, nikauliza tena, mlitaka aulize swali gani, hamjibu mnaandika porojo tu. Nendeni mkajiandae mje na hoja iliyoshiba sio mnaleta hoja ambazo hata nyie wenyewe kuzitetea mnashindwa

Tatizo unreflect situation ya leo. Refer tokea Bunge limeanza. We need Mbowe wa wakatim wa Campiagn siyo huyu tunayemwona Bungeni
 
Nadhani tuchukue historia ya CDM ndipo tutathmini uwezo wake. Sidhani kama maswali bungeni yanaweza kuleta tofauti sana hasa yanapotolewa na upande wa upinzani. Mbowe alipoanza kuwa mwenykiti wa CDM ilikuwa katika hali gani? Vipi ubunifu wake wa Operation Sangara ulifanukiwa kiasi gani? Maendeleo ya CDM chini ya uongozi wake yamekuwaje? Je ni mikiki mikiki mingapi amekutana nayo katika uongozi wake na ameishinda?Kwangu mimi CDM tuna mwenyekiti imara, jambo ambalo wana magamba wasingependa kulisikia, CDM iko juu sasa kuliko wakati mwingine wowote. Mambo ya mjengoni si tahmini ya kweli ya utendaji wa Mwenyekiti wetu.MBOWE songa mbele baba mpaka kieleweke.
Mkuu kitufe cha senksi kingekuwepo ningekugongea hata mara hamsini. Wapuuzi wanam-evaluate kiongozi kwa maswali anayouliza. Huo ni wehu tu! Ndio mwanzoni kabisa mwa thread nilisema kama wanataka kubalance stori wawe wanaevaluate na majibu anayoyatoa na kwakuanza waanze na JK. Mtu mzima ukitumiwa jitahidi kuendesha harakati zako wenye akili wasikushtukie unatumika. Ukishtukiwa ni aibu! Sasa hawa waungwana washashtukiwa kuwa wanatumika...njooni na hoja nyingine hii isha bounce
 
Tatizo unreflect situation ya leo. Refer tokea Bunge limeanza. We need Mbowe wa wakatim wa Campiagn siyo huyu tunayemwona Bungeni
hebu toa mfano amepwaya wapi? Toa mifano mitatu tu. Ukizungumza jumla jumla utakuwa unapiga majungu. Come with hard evidences kama ipo. Jamaa amekueleza ubunifu tu na impact ya Operation sangara, sasa kama kweli unafahamu sifa za kiongozi huwezi kubisha kuwa ubunifu ni sifa moja wapo. Sasa njoo na evidence ya wapi amepwaya!
 
Phd,acha ushabiki usio na tija,kwa sasa tatizo la umeme ni janga la kitaifa,kukosekana kwa umeme ni hatari sana kwa uchumi wa nchiunataka aulize swali gani?kama kwako tatizo la umeme sio nyeti basi napata shaka na uwezo wako wa kufikiri
 
you may do so if you wish but honestly mmi sio Gamba

Good lets not get there, Unamtazamaje Mbowe na Hoja anazozitoa? Kama Kiongozi wa Kambi ya Upinzani anapaswa kujua kanuni. Kama pia ulitazama Kipindi cha Tuongee Asubuhi Jumanne Kilichokuwa kinaendeshwa na Yahya Mohamed...Hoja alizouliza Lema Juzi na Mbowe leo zote zilijitokeza na wakati PM anamjibu Lema aliltolea Ufafanuzi hili hivyo hapakuwa na sababu ya Kiongozi wetu kutoitumia vema nafasi hiyo kutoa Hoja nyingine kwa kuwa kwa sasa hoja zote za Wizara ya Nishati na Madini zimesimamishwa hadi hapo siku 21 zitakpokuwa zimekamilika.

Nafasi hiyo ni nyeti sana kuibana serikali kwa kudai mambo mengine ya msingi na siy kufundishwa kanuni na PM.

Tatizo la mtoa thread ni hilo na mie nasimamia hapo kwamba imefika wakati hakuna haja ya ZITO kubeba Hoja mabzo nyingi zinaonekana kama ni kujijengea umaarufu badala ya kuiinua kambi na upinzani.

Imefika sasa wakati hoja nzito azibebe kiongozi wa Kambi na wao waje nyuma kama backup. Approach hii wanaitumia CCM walimpnga sendeka kupasua jipu la Jairo bahati mbaya Shelukindo akaidandia kwa kusaka umaarufu ambao alifanikiwa.

Political science is a process Mkuu
 
wewe ni mamliki tu, sasa jenga hoja, ungekuwa wewe ndio kiongozi wa upinzani ungeuliza nini leo kwa PM?

mzito kabwela utakufa kwa kihoro cha kumtetea mbowe kila mara hata mahali anapoonesha mapungufu, maswali kwa waziri mkuu ni sehemu very sensitive na kwa kuwa kiongozi wa upinzani bungeni ndiye anakuwa wa kwanza kuuliza ni muhimu hoja inayotolewa ikawa critical na inayoreflect matatizo ya msingi ya wananchi sio kikosi kazi cha umeme kila siku.

kuna mambo sensitive kama yafutayo,
  • tatizo la njaa miongoni mwa watanzania
  • kujiimarisha kiulinzi na silaha kwa kenya na uganda nini tafsiri yake kwa watanzania
  • kuvamiwa mipaka yetu maeneo ya kagera na warundi na wanyarwanda
  • madhara ya uchimbaji uranium
 
Na Gladness Mboma, Dodoma

SPIKA wa Bunge, Bi. Anne Makinda amemtaka Waziri wa Fedha na Uchumi, Bw. Mustafa Mkulo kuyataja bungeni kampuni 97 zilizonufaika na mpango wa kunusuru uchumi wa Tanzania kutokana na msukosuko wa fedha duniani.

Spika Makinda amelazimika kutoa kauli hiyo baada ya Naibu Waziri wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Bw. Pereila Ame Silima kushindwa kujibu maswali ya Mbunge wa Hai, Bw. Freeman Mbowe na mbunge wa Viti Maalumu, Bi. Leticia Nyerere waliotaka kutajiwa kampuni hizo.

Katika swali la msingi, Bi. Nyerere alitaka kujua ni kampuni ngapi, kwa majina na kiasi gani cha fedha zilizotumika kwa ajili ya kunusuru uchumi wa Tanzania katika kipindi cha mtikisiko wa uchumi wa dunia na fedha hizo zilitoka wapi na kiasi gani kwa kila chanzo.

Pia mbunge huyo alitaka kujua kama kampuni hizo zilipewa mkopo au msaada; na kama ni mkopo ni lini zitaaza kulipwa.

Pia alihoji fedha kiasi gani zimetumika hadi kufikia Desemba mwaka jana na kwa kuwa ni fedha za umma zinazokaguliwa na CAG, ukaguzi wake utafanyikaje kwa kuzingatiwa kuwa fedha hizo zilitolewa kwa kampuni binafsi.

Akijibu maswali hayo, Bw. Silima alisema hawezi kuyataja makampuni hayo kwa kuwa ni kuvunja utaratibu kwa kuwa ni siri kati ya benki na mteja.

Katika swali lake la nyongeza, Bw. Mbowe alihoji ni kwa nini kampuni hizo zisitajwe ikiwa zimenufaika na mamilioni ya fedha katika mpango huo, na baadaye Spika Makinda akamtaka Bw. Mkulo kutaja kampuni hizo bungeni, lakini hakueleza ni lini atatakiwa kufanya hivyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali kwa mwaka 2009/10, fedha dola milioni 48, ambazo ni sehemu ya sh. trilioni 1.7 zilizopitishwa na bunge mwaka 2008, kwa ajili ya mpango wa kufufua uchumi, hazijulikani ziko wapi, ambapo alisema wazi kuwa aliomba taarifa juu ya fedha hizo akanyimwa.

Baada ya kutoa taarifa hiyo na kuiwasilisha katika mkutano wa bunge la Aprili, suala hilo liliibuliwa bungeni, ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Bw. Kabwe Zitto, alimuuliza swali la nyongeza Waziri Mkuu Bw. Mizengo Pinda juu ya mahali zilipo fedha hizo, na kujibiwa kuwa kuwa wakati huo hakuwa na taarifa, huku Spika Anne Makinda naye akimtetea kuwa hastahili kulijibu.

Awali, akijibu swali la msingi la Nyerere, Bw. Silima alisema kupitia mpango huo kampuni 97 zilinufaika kwa kusaidiwa kufidia hasara waliyopata wakati wa msukosuko wa uchumi.

Alisema mpango huo ulikisiwa kugharimu sh. trilioni 1.7 kutoka vyanzo vya ndani na nje ya nchi.

Alivitaja vyanzo hivyo kuwa ni mikopo ya ndani sh bilioni 828 ili kufidia pengo la mapato na sh. bilioni 436.2 zikiwa ni mkopo nafuu kutoka Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) na sh. bilioni 428.3 zilitengwa ndani ya bajeti ya serikali kwa ajili ya kulinda ajira, kipato, kuwezesha utoaji mkopo na uwekezaji katika miundombinu na kuongeza kuwa urejeshwaji wa mikopo hiyo utafanywa kwa mujibu wa mikataba iliyoingiwa.

“Kutokana na kanuni za kibenki, si sahihi kutoa taarifa za mteja mmoja mmoja kwa umma kama ambavyo swali la mbunge lilivyotaka,” alisema.

Alisema hadi kufikia Desemba mwaka jana fedha zilizokuwa zimetumika chini ya mpango huo zilifika sh. trilioni 1.4535 pengo likiwa ni sh bilioni 239.

“Pengo hili lilitokana na kukosekana kwa fedha kutoka katika baadhi ya vyanzo pamoja na wafadhili mbalimbali. Kwa kuwa fedha hizi ziliingizwa kwenye bajeti ya serikali zitafanyiwa ukaguzi na CAG kama ilivyo kwa fedha nyingine za umma,” alisema
 
Phd,acha ushabiki usio na tija,kwa sasa tatizo la umeme ni janga la kitaifa,kukosekana kwa umeme ni hatari sana kwa uchumi wa nchiunataka aulize swali gani?kama kwako tatizo la umeme sio nyeti basi napata shaka na uwezo wako wa kufikiri
Pm wakati anajibu alisema ' Nakuheshimu sana Mh. Mbowe na sitaki kukupuuza' sasa hivi wapuuzi wanaleta siasa
 
acheni ushabiki usio kuwa na msingi, ishu ya kuunda kikosi kazi kutatua tatizo la umeme, aliuliza mbowe last wiki leo tena kauliza kitu kile kile bila kufafnua kikosi kazi kitatekeleza hadidu zipi za rejea kwa dharura, nachojaribu kueleza hapa ni kuwa kama kiongozi wa upinzani bungeni anatkiwa kuuliza jambo lenye hoja kwa suala ambalo ni very burning katika Taifa kwa sasa na anatakiwa kujenga hoja kwa mapana yake, kimsingi mbowe hana uwezo mkubwa wa kuunda hoja ili kumtikisa waziri mkuu. tujadili bila ushabiki
Kwako wewe hoja yenye mashiko kwa sasa ni ipi? You guys just don't get it! You can keep on posting things like this as long and as frequent as you wish, but the actual fact remains : THERE ARE INTELLIGENT PEOPLE WHO ARE CAPABLE OF RATIONAL REASONING AND INDEPENDENT THINKING. Enzi za kushikiwa akili zimekwisha. Kalaga baho!
 
afadhali ya huyo DJ, kuliko huyo mkwerè wenu sound sana bila vitendo, kila siku mkwerè anatubadilishia masong tu!

Tatizo lenu Magwanda, nyie kila kitu ni kupinga tu , hata vile vilivyo fanywa vizuri. Ngojeni Arusha wawaonyeshe sasa !
 
Maswali anayouliza kwa waziri Mkuu hayana mbele wala nyuma na anarudia kikosi kazi cha umeme kila siku hana ubunifu, ni dikteta kwa kumsikiliza lema ili madiwani Arusha wafukuzwe, naanza kuuona mwisho wa CHADEMA na kinaenda kuingia kwenye mgogoro mkubwa wa kiuongozi na kichama like NCCR na TLP
Ukweli ni kwamba Hakika watu hawajui ndani ya CDM kuna nini,chama kinamilikiwa na watu wachache sana ,hakuna mtu chadema anaweza kumpinga mbowe akastawi chadema,mimi nawashaangaa sana wa tz,Slaa angalau lakini na yeye anazidiwa nguvu,wanamuogopa sana,hata wabunge hawawezi kufurukuta kwa jamaaa,
 
Kwanza kabisa mleta hoja mimi namwona kama anachuki binafsi na Mh Mbowe. pili watu mmeanza kujijadili nyie badala ya kujadili mada,

Msimamo wangu ni kwamba Mbowe hajapwaya na yupo makini kuliko Hamad ambaye kunatuhuma alikuwa akimpatia PM Maswali kabla hayajaulizwa.

Pia Mh Mbowe ameshamaliza kazi kubwa pale aliposoma mpango wa kambi ya upinzani baada ya ile ya PM, utaona jinsi alivyoichoma serikali na kuamsha mambo mazito, na mpaka sasa kinachotokea bungeni sote tunashuhudia, watu wanacheza music wa Chadema.

Kuhusu Chama kufa hiyo wala haipo, ni sawa na mke na mume kutofautiana katika issue na kizuka mjadala na hata ugonvi then watu wa pempeni waanze kusema hapa ndoa itavunjika, mtasubiri ivunjike milele.

sasa wanaotabiri kifo cha chadema ni sawa na midume mikware inayoshabikia ugonvi wa wanandoa ili ipate nafasi ya kumrubuni mwanake, tafakari upya.

Umeme ndio tatizo la Pili kwa ukubwa TZ, tatizo la kwanza ni ufahamu wa VIongozi na wananchi pia (yaani Mind set, kwa wataalamu wa lugha wanaweza kuliweka sawa) so Mbowe hata arudie swali mara kumi ndio msingi wa uchumi wa nchi.
 
I can humbly sum up that the incumbent president of Tanzania is hopeless and spineless ! We need a radical changes otherwise the country will never ever end corruptions. Karne hii tupo gizani lol!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom