Mbowe ana msongo mkubwa wa mawazo, ni baada ya kutoitwa Ikulu

CalvinKimaro,
tunachojua ni kuwa Mbowe alimwelekeza rais afanye maridhiano na kambi ya upinzani na rais akatii bila ajizi.

tunajua Rais wetu ni egoistic, so hataki kuonekana amemtii Mbowe mbele ya mamilioni ya Watanzania tuliosikiliza ile speech ya Mbowe.

ndiyo maana rais ame mute mwaliko kwa Mbowe ambaye naye katoa condition kuwa hata akialikwa basi ni lazima aende na jopo lake lote la magwanda.

no drama!
Rais wetu ni egoistic, Mheshimiwa Mbowe naye unamuweka wapi????
'Double Standard'
 
Haya ndio mawazo ya middle class wa kitanzania,ambaye anajiona amesoma na ana uelewa wa kusoma to understand,kwa taarifa yako mtoa hoja ;ni kweli Mh.Mbowe aliandika barua ikulu kwa ajili ya kukutana na our no 1(ni haki yake ambayo hata mimi na wewe tunayo,ili mradi tufuate sheria)kukubaliwa kwa ombi ni HAKI ya yule anayeombwa(kumbuka hili mkuu).

Kwa taarifa yako mh.Shariff Hamad alishaandika barua muda mrefu ya kuomba kukutana na president Magufuli na hili alituthibitishia kuwa wakati wa uzinduzi wa kitabu cha President Mkapa,Rais Magufuli alimjibu kuwa anajua anamtafuta na atatafuta muda waonane,kwa hiyo ni ufinyu wa akili yako mtoa hoja kuwa Mh.Hamad hakuomba mwaliko.next time unapotoa hoja ni vema usipindishe ukweli pamoja na mapenzi yako (ambayo nayo ni haki yako).
Umejibu kuustaarabu 100% kiongozi.

WELL SAID!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Swadakta!,maneno kuntu haya
Nimemsikiliza mtani wangu Mbowe akijibu swali ni kwa nini hajaalikwa Ikulu ilihali yeye ndiye aliomba kwa maandishi lakini wamealikwa ambao hawajaomba kualikwa?

Ukimsikiliza utabaini ana kitu Wazungu na Wapare tunaita "psychological disorder". Yaani hitilafu itokanayo na matatizo ya kijamii na kiakili.

Huenda ni mjumuiko wa stress za kuulizwa maswali na wapiga kura, hofu ya uwezekano wa kufungwa au kupoteza ukuu wa kambi mwaka huu. Majibu ya Mbowe ni kiburudisho tosha!

Ikumbukwe mwaliko hauombwi. Huwezi kuomba mtu akualike! Ukishaomba mtu akualike unakuwa umejishusha thamani mno. Huna tofauti na ng'ombe anayetolewa bomani kwenda kuchinjwa. Hata ukialikwa unakuwa mgeni asiye na thamani! Ukifanya kosa la kuomba mwaliko na usialikwe ni busara ukae kimya kulinda hadhi yako.

Lakini pili huwezi kudai walioalikwa hawakuzungumzia hoja zako. Unajua kadi zao za mialiko zilisemaje?
Tatu, ili ualikwe lazima wewe unayetamani kualikwa uwe muungwana na mstaarabu. Usiwe unamzushia uongo unayetamani akualike. Mfano ni kauli ya Mbowe kuhusu Gwajima. Tayari polisi walishamuita kumhoji siku chache nyuma.

Leo Mbowe anamtuhumu anayetamani amualike kuwa ndiye aliyemtuma Gwajima. Anawapigisha ukunga wamama eti washike vichwa na kulia "keleuwiiiii" Mbowe hana hata punje ya ushahidi! Akiitwa polisi atabaki kudai polisi inatumika vibaya. Kwa akili tu ya mtaani, hivi Rais atamwalika mtu sampuli hii? Mtu anayemzushia kila uongo unaokuja kichwani?

Mbowe hapaswi kualikwa hata na DC Sabaya achilia mbali Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Na ukweli ni kuwa asipoalikwa hana chochote cha kufanya zaidi ya kupiga kelele BAWACHA na BAVICHA za keleuwiiiii!

Mbowe anaendelea kujidanganya na nguvu ya umma ambayo ni hewa. Angekuwa nayo asingesusa uchaguzi akaenda kusinzia. Asingekuwa anamuomba Rais uchaguzi urudiwe, angeitumia kulazimisha uchaguzi urudiwe. Ukweli ni huo Mbowe ni ombaomba, hana nguvu ya umma.

Ukichanganya na hoja kuhusu msajili kuvitaka vyama vihakikiwe kabla ya uchaguzi mkuu hutasita kubaini Mbowe ana msongo mkubwa wa mawazo! Hoja anayotoa kuwa vyama vimezuiwa kufanya kazi ni kichekesho. Mfano, Chama chake kimefanya uchaguzi wa viongozi hivi karibuni.

Hata juzi alianza mikutano jimboni mwake sema tu ukaingia mdudu. Hivi alitaka afanye nini kuimarisha Chama chake akazuiwa? Kuna aliyemzuia kusajili wanachama? Kujenga ofisi? Kutekeleza au kusimamia miradi ya maendeleo? Nadhani msajili aanze hili zoezi haraka. Kuna vyama vilishapoteza uhalali.

Vimebaki kuwa vyama vya BBC, DW, Twitter na Press conference tu. Hivi Mbowe ana hofu ya nini kuhakikiwa? Hana wanachama pande zote za muungano? Si huwa anajitapa Chadema imeenea hadi vijijini kupitia operesheni? Hofu ya nini?

Nimalizie kwa kumtakia hukumu njema mtani wangu hapo kesho.

Soma: Mbowe: CHADEMA haikupokea mwaliko wa kwenda Ikulu kuzungumza na Rais Magufuli
 
Correct 100%
Kila zama na nyakati zake.

Alipowekwa ndani mara mbili na wafuasi wake wakala xmass na pasaka vizuri...ndio nilitambua hana huo umma

Umma alio nao wako mitandaoni kwa ID fake, wanaweza kutukana, kukejeli, kukuita msaliti, kamwe hawanaga muda wa kukifanya chama kikue
 
Back
Top Bottom